Salaam Wakuu,
Kama mtakumbuka, mwezi Februari mwaka huu, TRA walitangaza nafasi za Kazi kwa Watanzania wenye SIFA. Na takribani Watanzania laki moja na kitu, waliomba zile nafasi, na baada kufanyiwa Usaili uliofanyika tarehe 29 & 30 Mwezi Machi. Baada ya Usaili, Matokeo yalitoka Mwezi April na Watanzania wote waliona matokeo ya Usaili ule wakiwemo walioomba. Baada ya Hapo mwezi Mei waliofanikiwa kupita usaili wa Kuandika na hatimae ulifanyika Usaili wa Mahojiano.
Jambo la kushangaza sana ni kuwa TRA wametoa tangazo la watakaoitwa kwenye nafasi za Kazi watattumiwa Barua Pepe kujulishwa na kutakiwa kuripoti kazini Mara. Malalamiko yangu, kwa nini watumie barua pepe na wasitumie utaratibu uliozoeleka na inawezekana unaojulikana wa kutoa Taarifa ya Majina kwa UMMA kama ambavyo imekuwa ikifanyika Miaka yote na kwenye Taasisi zote za UMMA? Kwa kufanya hivi, hakutakuwa na upendeleo wa kutumiwa email watu ambao hawakuomba kazi? Taasisi kama Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wametoa tangazo la kuitwa kazini kwa Umma, inakuwaje TRA wafiche?