TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

Hili la TRA kuhamishia account za kenya commercial bank KCB toka bank ya kitanzania NMB jamani limekaa vipi? Jambo kama hili wakati wa magufuli lisingewezekana kabisa. Inaelekea mbinu za kifisadi wakenya kuhodhi uchumi tanzania zimeanza kufanikiwa tena. Watanzania hawana imani na wakenya. Ni jambo la kustaajabisha wananchi kuona mamlaka ya fedha TRA kuacha bank za nchini na kutumia bank ya kenya. Serikali ina hisa NMC na bank hiyo ni kubwa na yenye uwezo ila mbinu za hila za wakenya ndio zinawezesha uamuzi wa mamlaka kubwa ya serikali kama TRA kuweza kuacha kutumia bank ya nchini na kutumia bank ya nje. Jambo hili inafaa waziri wa fedha aingilie mara moja vinginevyo ataendelea kuwaudhi wananchi ambao wana wasiwasi juu ya uwezo wake.
Kama ulikuwa unanufaika kwa nanna yeyote,wakati zikipitiamo sasa connection imeparaganyika,jipange upya update tena,connection huko ziliko hamia,usije kujiliza humu.
 
Ni ya kweli hayo? Kama ni kweli nafikiri litafanyiwa kazi maramoja.
 
Kama ni kweli, inaanza kuyapa nafasi yale maneno ya chini chini juu ya wakenya.
 
Yaani mapato ya serikali kupokewa kupitia bank ya kigeni?
Masikini si wanajua ujasusi mwingi unaweza kufanyiwa kupitia haya mabenki?
Au Marais waliopata walikuwa hawana uelewa kuliko huyu wa Sasa? Lol masikini.
 
Tuna safari ndefu sana. Mabenki ni wakusanyaji tu wa mapato ya TRA yanayopelekwa BoT. Huko kwenye taasis za kifedha zinapita tu.

Hapo chini kwenye kiambatanishi inasoma to
Commissioner of customs and excise
TRA
BoT

Sasa hapo KCB analaumiwa kwa lipi?
Tukiambiwa malipo yote yafanyike kwa bank moja hizo foleni na ucheleweshwaji tutauvumilia?

Kama sijaelewa vizuri naomba kueleweshwa.
Huyu jamaa ni kilaza sana hawa ndio walishikwa akili za udanganyifu wa mzee wanadhani kila kinachofanyika watu wanapiga dili.

Sent from my VFD 600 using JamiiForums mobile app
 
Sikia ndugu, serikali ina hisa 100% kwenye benki ya serikali iliyoitwa TPB bank (Tanzania Postal Bank) au Bank ya Posta ambapo kwa sasa inajulikana kama TCB (Tanzania Commercial Bank), sasa swali la kizushi ni kwamba kwanini huduma nyingi za kiserikali hazipitii bank hii ya serikali mfano mishahara ya watumishi wa umma na malipo mengine kadha wa kadha?
Soko huria mzee

Sent from my VFD 600 using JamiiForums mobile app
 
Kama ulikuwa unanufaika kwa nanna yeyote,wakati zikipitiamo sasa connection imeparaganyika,jipange upya update tena,connection huko ziliko hamia,usije kujiliza humu.
We ni mkenya?
 
Maoni ya wadau wengi katika huu uzi unaonesha ni jinsi gani upotoshaji umetamalaki vichwani mwa mwa watu...
Elimu ya miamala ya TRA kwenye mabenki ni duni.

Mtoa mada pengine hujawahi kufanya malipo ya TRA na benki tofauti ya NMB,ndio maana hili kwako unaona ni jipya.
 
Hivi mtaendelea kuzungumzia na kumfanyia rejea aliyetangulia mbele za haki mpaka lini?? Kwanza hata yeye huko aliko anawashangaa kwamba bado amewashika akili hata huko aliko.
 
Ww ndio hujui kitu, Tanzania Government ina NMB shares 31.8%. Next time kama hujui kitu, nyamaza!

Usiwe unakusanya takataka huko wikipedia na kutuletea humu. Soma hapo chini uijue vizuri NMB

History​

NMB Bank is one of the largest commercial banks in Tanzania, providing banking services to individuals, small to medium sized corporate clients, government services, large businesses and agriculture lending.

NMB Bank was established under the National Microfinance Bank Limited Incorporation Act of 1997, following the break-up of the old National Bank of Commerce, by an Act of Parliament. Three new entities were created at the time, namely: (a) NBC Holdings Limited (b) National Bank of Commerce (1997) Limited and (c) National Microfinance Bank Limited.
Initially NMB Bank could only provide payment services as well as offer savings accounts, with limited lending capabilities, before becoming a fully-fledged universal retail bank.

In 2005, the Government of the United Republic of Tanzania privatized the bank when it sold part of its shareholding (49%) to a consortium led by the Coöperatieve Centrale Raiffeisen-Boerenleenbank B.A. (‘Rabobank Group’).
Subsequently, there was further divestiture in 2008 when the Tanzanian Government off loaded another 21% of its shareholding to the Tanzanian public through an Initial Public Offering (IPO). The listing of the bank’s stock on the Dar es Salaam Stock Exchange has led to a diversified ownership structure.

bofya link hapo chini

Wanaoilipa TRA ni watanzania au makampuni yenye akaunti zao KCB, benki hiyo ya kigeni iko kihalali na inawezekana ina ufanisi mkubwa ukilinganisha na benki zetu za kizalendo.

Benki zetu zinashindwa kwenye huduma kwa wateja na hasa huduma kupitia mtandao. Kama uzalendo ni lazima uanze kwa kuwashawishi wananchi wasiweke pesa zao kwenye benki za kigeni ikiwemo KCB..... Je inawezekana ?.
 
Inawezekana Serikali ilichukua credit facility (Bank overdraft)kulipa madeni au wadai wake wa SGR au Nyerere dam Rufiji.Mara nyingi credit facility Kama hizi zinaenda na makubaliano ya kuwa unaweka(deposit) fedha kwenye benki hiyo kupungaza riba.
Nadhani Serikali itakuja na ufafanuzi,juu ya suala hili la kuweka fedha kwenye benki ya nje wakati tunazo benki za ndani,labda Kama TRA wanazo account kwenye benki zingine local.
 
Na wewe? Yaani hujui kuwa serkali ina zaidi ya aslimia 30 ya hisa huko?

soma hapo chini nionyeshe hiyo 30% inatoka wapi

Back
Top Bottom