TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?



Wewe si ndio ulisema tenda?
 
Pesa ya serikali ikishakusanywa inakaa bank yoyote nadhan wiki 1 tu then inaenda BOT so bank yoyote haikai na pesa ya serikali zaidi ya wiki 1 pesa yote inaenda BOT then this is automatic transfer kwenda BOT.
 
Pesa ya serikali ikishakusanywa inakaa bank yoyote nadhan wiki 1 tu then inaenda BOT so bank yoyote haikai na pesa ya serikali zaidi ya wiki 1 pesa yote inaenda BOT then this is automatic transfer kwenda BOT.

Tunaongea lugha moja Benki ndogo za kiTanzania na kiAfrika hawana ubavu wa kutoa huduma kubwa kwa serikali na ndiyo maana wanaziona ni za moto wanahamishia BoT.

Benki kama NMB au KCB ni kama maajenti wa M-Pesa kimtaji hawawezi kukaa na pesa nyingi zitawayumbisha ki-operesheni na kushindwa kutuhudumia sisi wateja wadogo tulio wengi.
 
Wee inamaana hujui tangu Magufuli akiwa hai, Mwingereza mwenye hisa na NMB Bank alichukua hisa zake kalala mbele?

NMB ilikuwa share ya Serikali na Mwingereza. Baada ya mwingereza kujitoa yawezekana ishashindwa kujiendesha.

Wee huoni hata mandege (ATCL) ya Serikali wameshashindwa kujiendesha? ni hasara tupu.
 
Mleta uzi hafahamu kwamba TRA inatumia mabenki karibia yote yaliyosajiliwa nchini kukusanya kodi kwa mfumo wa TaxBank. Hiyo payment order form uliyopost TRA wanakuprintia kulingana na wewe uko benki gani, ukitaka hata mwenyewe unajiprintia online.
 
Inapokuja suala la taasisi kama TRA, siyo suala la huduma. TRA haendi benki hata siku moja kutafuta huduma kama wewe unavyokwenda na kujaza vikaratasi na kuulizia salio. Huui ni uhusiano wa taasisi ya serikali na benki ambayo serikali pia ina hisa ndani yake. Huduma zao wanawasiliana kwa ngazi ya juu, siyo dirishani.

Hata hivyo naamini hili ni suala pana zaidi. BOT wanahusika. Iwe kwa sababu yoyote ile, huu ndo unafiki na bei ndogo ya maafisa wa serikali. Imefikia hata taasisi zinafanyakazi kwa kushawishiwa na watu, tena kwa kupewa chochote.
 
Hii ndo ideal situation kwa serikali ambayo ni ideal. Huwezi kusanya kodi ya nchi kupitia benki binafsi tena ya nje! That is stupidity of highest order. Kwa uzoefu wangu sitegemei hata siku moja Benki ya TZ ipate wateja kwenye nchi ya Kenya. Hata CRDB wamefanikiwa hapo Rwanda tu na wakijaribu Nairobi, wanabaguliwa kwa sababu tu ni ya TZ. Sasa leo TRA inafungua akaunti KCB!

Kwa ujumla ninaamini viongozi wetu wanakuwa ni watu wa bei ya chini sana! Wanavutiwa hata na mambo ya kipuuzi. Ukiuliza hapo, unaweza jibiwa waliahidi mkopo kwa waziri ili ajenge hotel, basi!
 
Kama sijakosea TRA ina accounts kwenye mabenki kibao ambazo zinapokea malipo halali ya Shirika hilo.
Suala siyo uhalali wa akaunti, tunajiuliza ni kwa manufaa ya nani? Yaani sisi kama nchi tuko tayari kunufaisha KCB na siyo NMB, CRDB, NBC, etc. our very homegrown banks?
 
Kazi Imeanza ?
 
Suala siyo uhalali wa akaunti, tunajiuliza ni kwa manufaa ya nani? Yaani sisi kama nchi tuko tayari kunufaisha KCB na siyo NMB, CRDB, NBC, etc. our very homegrown banks?
Ni ajabu na kweli, tutasikia mengi
 
Ili uwekezaji kwenye sekta binafsi uimarike, shurti ifanye kazi na serekali.
Ninaamini move hii ni kwa ajili kuwavutia zaidi wawekezaji kutoka nje ambao Magufuli aliwapiga pini pakubwa.

Kwa hili kama ni kweli nasimama na TRA!
 
Huu ni utawala wa upigaji tu hakuna namana.
R.I.P Magu.
 
Sure
 
Tra unawalaumu bure ndg yangu, wa kuulizwa na kutoa majibu ya haya mazongozongo yote yanayoendelea ni Rais. Yeye anapinduapindua kila alichokikuta wima ni sharti akilaze ili mumuone naye wamo
Waziri WA fedha kasema mini sababu ya kuanika mapato yeti nje ya nchi
 
We chizi! kwahiyo huku Tandahimba hamna KBC kwahiyo hatupati huduma!!!mimi nina akaunti ya NMB nalipia fresh tu.mukiambiwa muende Burundi munakasirika!nani alikuambia NMB yetu?benki ya Poster ndio yetu.
 
Labda Ndugu yetu Mfumo wa Malipo TRA huujuwi Vizuri, ukiwa unafanya malipo kuna wengine wanaenda TRA anaomba control, wanamtengenezea na kumwekea bank atakayo kwenda kulipia, hapa sasa inategemea TRA kakchagulia Bank gani, hii ndiyo system wengi wanayo tumia. Wengine wamekuwa registered na TRA jkwenye mfumo wa kutoa control Numba upo hivi. unaenda kwenye web site ya TRA unabofaya Payment registration unaweka details zaoko jina la kampuni, TIN numba kuna mahali unafika panasema TAXPAYER BANK NAME hapa zinakuja BANK zote ambazo zipo approved na BOT kwa kukusanya Mapato ya Serekali. mimi naona karibu bank zote zinazo operate hapa Tanzania zote zipo. kulingana na milipaji account yake amefungulia wapi. kwaiyo hizi bank ni collector to wa Mapato ya TRA na ikifika Jioni lazima wawkilishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…