TRA kwenye kodi ya magari wanafanya "wizi" wa wazi kabisa

TRA kwenye kodi ya magari wanafanya "wizi" wa wazi kabisa

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,560
Reaction score
15,864
Hebu leo tuwaangalie hawa jamaa,

Mifumo yetu ya kikodi ni mibovu mno yaani hakuna namna ambayo kodi itatoa ahueni kwa mwananchi wa kawaida hilo halipo. Angalia ukiagiza gari iliyotumika iwe Japan, Dubai, Thailand au Afrika Kusini yaani kodi unayolipa tena isiyo na mantiki tena kodi ya kuudhi.

Angalia kwa mfano unanunua gari dollar 2500 unalipa tozo na kodi zao dollar karibu tena 2000, kwa ufupi ukinunua gari ya milioni kumi nje andaa kodi milioni 7 au 8 au 9.

Ukiangalia vyema calculator yao hawa TRA ni formular ya ujanja ujanja ya kuumiza wananchi na wabunge walikaa wakapitisha kodi hiyo ya mchongo ambayo haiendani na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Ifike hatua nao wajistukie kanuni wanazotumia kama sio kupitwa na wakati basi TRA wao wenyewe wamepitwa na wakati.

Pamoja na kukusanya mapato lakini TRA ni moja ya taasisi zinazorudisha nyuma maendeleo ya nchi hii.
 
Gari sio kwa kila mtu kama unalalamikia Kodi ya 9m TZS (4000 USD) elewa hujafikia hadhi ya kumiliki gari hangaika na Guta, SANLG au FEKON ndo size yako. Asante.
Akili yako ni yazamani sana. Dunia ya leo unashindwa kujua gari ni kitu cha kawaida. Dunia ya leo gari sio ufahari au maisha mazuri bali ni huduma kama huduma zingine.
 
Hebu leo tuwaangalie hawa jamaa,

Mifumo yetu ya kikodi ni mibovu mno yaani hakuna namna ambayo kodi itatoa ahueni kwa mwananchi wa kawaida hilo halipo. Angalia ukiagiza gari iliyotumika iwe japan, Dubai, Thailand au Afrika Kusini yaani kodi unayolipa tena isiyo na mantiki tena kodi ya kuudhi.

Angalia kwa mfano unanunua gari dollar 2500 unalipa tozo na kodi zao dollar karibu tena 2000 , kwa ufupi ukinunua gari ya milioni kumi nje andaa kodi milioni 7 au 8 au 9.

Ukiangalia vyema calculator yao hawa TRA ni formular ya ujanja ujanja ya kuumiza wananchi na wabunge walikaa wakapitisha kodi hiyo ya mchongo ambayo haiendani na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Ifike hatua nao wajistukie kanuni wanazotumia kama sio kupitwa na wakati basi TRA wao wenyewe wamepitwa na wakati.

Pamoja na kukusanya mapato lakini TRA ni moja ya taasisi zinazorudisha nyuma maendeleo ya nchi hii.
huku ulimwengu wa tatu kumiliki gari ni anasa!
Siku wakichukulia gari kama usafiri wa kumsaidia mtu azalishe zaidi ndio wataweza kupunguza kodi
 
Akili yako niyazamani sana.dunia ya leo unashindwa kujua gari ni kitu cha kawaida. Dunia ya leo gari sio ufahari au maisha mazuri bali ni huduma kama huduma zingine
Point ya Jamaa ni valid mkuu, gari pamoja na umuhimu ambao umeusema bado hajafikia kuwa essential item inayohitajika kwenye maisha;

Hivyo kwangu mimi kitu kama gari Kuwekwa kodi hiyo unayosema ni sawa kabisa; Mpaka umewaza hivyo inamaana bado haukuwa na uwezo thabiti kuwa na gari.

Mfano, ukiona unalalamika kwamba Mcdonald, KFC kwamba wanauza vyakula bei juu, its obvious bado hujafika uwezo wa kutumia vyakula vya hapo na sio dhambi usiwachukie wanaomudu hapo au kuwalaumu, vivyo hivyo kwenye gari ungekuwa na uwezo mkubwa kabisa hiyo kodi usingeiona kama kikwazo kabisa, ingekuwa kikwazo kwa watu wengine ila sio kwako.

SO mkuu nimeielewa point yako, ila kimsingi ni kwamba wakati mwingine uwezo wetu ndio unaleta mitazamo fulani inapokuja suala la matumiz ya pesa.
 
Wanafanya hivyo kuzuia dumping, bila hizo kodi hii nchi ingekuwa jalala la hayo magari used mbaya zaodi miundo mbinu yetu haiwezi himili magari mengi.

Tafuta pesa
Mawazo ya kizamani,sio kwamba gari zote ubakia Dar,hoja ya ant dumping ni haina mashiko kwa zama hizi.
Kwani gari zote chakavu ukatwa screpa hio hoja ilifaa zamani ambapo biashara ya screpa haikuwepo watu waliyaacha tu magari yakioza.
 
Back
Top Bottom