Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Katika sherehe ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Mapya ya CCM yanayojengwa Mkoani Dodoma, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi alisikika akisema Kampuni yao ya JITEGEMEE Holdings inayochimba na kuuza madini ya Makaa ya Mawe Mkoani Ruvuma imelipa kodi kiasi cha Shilingi BIlioni 42 kwa mamlaka za Serikali tangu kuanza shughuli zake.
Kuna taarifa kuwa Kampuni ya Jitegemee inayomilikiwa na Chama cha Mapinduzi imekuwa ikifanya biashara kubwa ya Makaa ya Mawe kwa kuyachimba na kuyauza nchini kwa kiwango cha kutisha huku iliwa hailipi Kodi na tozo Stahiki inavyopaswa.
Pia kuna taarifa kuwa, fedha nyingi zinazopatikana kupitia biashara hiyo ya rasilimali za Watanzania zinakwapuliwa na Viongozi wa juu wa CCM huku Mkoa wa Ruvuma ukizidi kuwa masikini kila kukicha.
Hii ni tuhuma nzito sana juu ya Chama cha Mapinduzi. Tuhuma hizi ni uthibitisho wa Chama hiki kufuja rasilimali za Taifa kwa faida ya watu wachache huku Watanzania wengi wakizidi kuwa masikini na kukosa huduma za Msingi.
Tunaomba sasa Mamlaka ya Kodi na Te ya Madini watoke wazi watuambie Watanzania kwa vielelezo kama Kampuni hii ya Jitegemee imelipa kiasi hicho cha kodi kama ilivyodaiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Tunaomba pia TRA na TUME YA MADINI watubie hesabu za uzalishaji wa Kampuni hiyo zikoje na kama zinaendana na kodi Wanayolipa.
Watanzania tuamke
No Reform No Election ✊️✌️