Tra na usumbufu wa road license

Tra na usumbufu wa road license

Fofader

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Posts
863
Reaction score
299
Unakwenda kwenye ofisi ya TRA ukiwa radhi kulipa kodi.
Unakutana na mlolongo wa ukiritimba. Unasimama foleni benki kwa masaa mawili ili kuwapa fedha. Mazingira ni mabovu na watu wamejazana kupita kiasi. Hakuna hewa ya kutosha. Hata hivyo hakuna meneja anayeonyesha kujali wala kudhibiti mambo. Inaonekana ni hali ya kawaida tu. Unatoka na unaambiwa rudi kesho au keshokutwa kuchukua leseni yako. Upotezaji wa muda na kukatishwa tamaa kwa hali ya juu!
Swali kama Ndesa alivyoouliza: hivi Tanzania hii hakuna watu wenye akili ya kutoa suluhisho la matatizo madogo kama haya?

Sent from my GT-P7500 using Tapatalk HD
 
Hiyo ndiyo raha ya madaraka. Ni kama wanasema " ukiona karaha kunywa sumu"
 
Back
Top Bottom