TRA na Wizara ya Fedha inatakiwa kupiga hesabu kwa maslahi ya taifa

TRA na Wizara ya Fedha inatakiwa kupiga hesabu kwa maslahi ya taifa

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Cc: TRA Tanzania, Dr. Mwigulu Nchemba

Kuchaji kodi ya Dungu 15M na magari 50 000 tu yakaingia kwa mwaka inapata Shs 750,000,000,000// bilioni 750 tu

Wakati kama itapunguza kodi na kuwa shs 5M kila Dungu 4×4 used na kwa kufanya hivyo sasa yakaingia mengi milioni moja kila mwaka na kusambaa hadi SOUTH SUDAN, UGANDA, DRC, RWANDA, BURUNDI, ZAMBIA, MALAWI, MSUMBIJI, COMORO, MADAGASCA, MAURITIUS, SEYCHELLES

TRA ingemake 1,000,000×5,000,000=5,000,000,000,000, yes trillions 5 kila mwaka kutoka bilioni 750 yaani karibu mara tano na hapo maana yake BANDARI NAYO IMEKUWA BUSY SAANA NA KUTENGENEZA PESA YA TOZO ZA MELI ZILETAZO MAGARI HAYO.

Wakati mwingine African countries mifumo yetu ya kodi TUNAJIKABA sisi wenyewe aisee yaani hatupigi hesabu nyepesi tu ambazo Dr Msukuma na darasa lake la 7 angepika kwa maslahi ya Taifa...

Unakaa unajiuliza kuna nini au ni wafanyabiashara wanaoingiza magari MAPYA ndio wana DICTATE kodi za used cars ziwe kubwa ???? Na je ni kwa maslahi ya nani?

Wa gari jipya atabaki wa gari jipya serikali ilitazame hili la kupunguza kodi ya magari used ili TANZANIA IWE HUB ya kuuzia used car kwa nchi za SADC na ukanda wa maziwa makuu lakini maana ni tija kwa pato la taifa kuanzia kwenye Vipuri car parkings road taxi maana unaweza kuweka kodi ya barabara kwa used car shs 50,000/= kwa mwaka pale tu linapouzwa hivyo hata kama Mkongoman analinunua kwenda nalo kwao lazima alipe hiyo kodi..hapo napo ume make money kama taifa.

Kodi kubwa kubwa huwa zina slow down business na kulipinguzia taifa mapato ukiachana nazo na badala yake ukaacha watu wawe na magari kisha wewe sasa ukaweka vikodi vidogo vidogo instead kama road taxi, fuel taxi, spare parts taxi utavuna hela nyingi kwa magari mengi kuingia kwanza halafu pia kwakuwa yapo tayari wenye nayo hawataepuka kodi ndogo ndogo zihusuyo magari nazo zinakuingizia pesa kama Taifa.

Shime TRA na wizara ya fedha kama mna uzalendo wa Taifa hembu lichukueni hilo.

Gari sio anasa kamwe dunia ya leo.

Hii isambae hadi iwafikie wahusika.

Copied from Mzalendo mpenda Kodi/kwa maendeleo.
 
Shida ilo hapa
20240904_122706.jpg
 
Uzalendo au kila mtu anajipambania kivyake vyake? Na kutumia mwamvuli wa uzalendo kwa Taifa? Unaposikia kila mwaka wananunua magaria ya bilion 500 na kuendelea, lazima ukae utafakari. Na kujua kama kweli tunamaanisha uzalendo au tuna mambo mengine
 
Kodi za TRA za ajabu sana na wao ndio chanzo kikuu cha ajali Tanzania kwa maana magari ya miaka ya karibuni kodi zipo juu tunaishia kununua Scraper za miaka ya nyuma na huko Tandale na Ilala yamejaa magari ya kuchinjwa ili kurekebisha hizi gari nyingi zenye uchakavu wa kutosha wakati huko Duniani magari mengi bei zake ni za kawaida tu..
TRA hawawezi kupunguza kodi wakiamini mapato yatapungua ingawaje walipunguza kodi magari mengi mazuri yataingizwa Nchini na kupunguza kiwango kikubwa cha mazingira ya Nchi.
TRA pana gari ya 2012 pick up kodi yake ni zaidi ya 20m wakati kwenye ununuzi ni Rand 90,000 tu sawa na Tsh 14,000,000.
Watanzania wamejibana kwenye vigari vidogo kwa sababu ya kodi kubwa kwenye magari mazuri ambayo huko nje bei zake ni za kawaida tu.
Utashangaa wapo busy kuongeza kodi ya Scania Tractor wakati tuna bandari ambayo ina uhitaji wa malori mengi ili kupunguza msongamano huko bandarini ila wao hakuna kitu wanajua zaidi zaidi ya kutengeneza task force tu za kula rushwa..
TRA hawatoi ushauri kufanya Ujenzi wa bara bara ya Tunduma au Custom kubwa yenye uwezo wa kuweka trucks za kutosha gari inachukua siku moja mpaka mbili kuvuka ule mpaka hata hatujui wanafikiria nini..
 
Back
Top Bottom