TRA: Pikipiki (Bodaboda) kuanza kulipa Kodi ya Tsh. 65,000/- kwa mwaka

Akiba hawezi pata ila on daily basis anapata.

Wamama wanalipa ushuru wa 200 Kila siku masokoni
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku. Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu. Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Naungana nawe ila pia ela ya kodi kusikia inapgwa na wapigaji wapo tu si uzalendo
 
Twendeni tu, kila mtu yatamkuta, itafika hatua mtu mwenyewe anatoka nyumbani kwenda kupinga unyonyaji.

HAtupingi kulipa kodi, maisha yaemdane na kodi zetu, tunalipa kodi kisha pesa zinaingia kwa mafisadi, wanakula bata, gari za milioni 400.

Wanatunyonya mnoo, itafika hatua wao wanaenda chooni wanakunya kinyesi, sisi ni povu tu.😂
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku. Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu. Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
Kuna siku moja nilikuwa naongea na jamaa mmoja Mtanzania anakaa Finland siku nyingi sana, kuhusu kodi.

Akawa anasema, Watanzania si kweli kwamba hawapendi kulipa kodi. Watanzania hawapendi kulipa kodi ambazo hawaoni zinachofanya katika maisha yao. Yani kodi wanalipa, halafu zile huduma za kijamii zinazotakiwa kufanywa na hizo kodi hawazioni.

Akasema, Watanzania hawahawa wakienda kukaa nchi kama Finland, wanatozwa kodi kubwa kuliko Tanzania, lakini hawalalamiki.

Kwa nini? Kwa sababu kazi nzuri zipo, mishahara mizuri ipo, na hata kukiwa na kodi kubwa sana, wanaona kabisa kodi zetu zinafanya kazi gani, kuanzia shule nzuri, hospitali nzuri, zenye madawa na huduma tele, madaktari wazuri na wengi, mifuko ya jamii kuhudunia watu wasio na kazi ipo vizuri, wazee wakistaafu wanahudumiwa vizuri, nyumba nzuri, huduma kama zimamoto na ufagizi wa mitaa nzuri, barabara nzuri, takataka zinakusanywa vizuri, maji unapata vizuri, mtu unaona wachukue tu hiyo kodi, maana kazi ya kodi unaiona.

Sasa Tanzania mnaenda kuwaminya mpaka mapumbu kwa kodi hao bodaboda ambao hata kula kwao kwa tabu, halafu kodi zote mnaenda kununua ma VX na kujenga ma Ikulu kedekede, huku hospitali hazina dawa, takataka hamzoi, miji michafu, maji ya shida mpaka mjini, mnategemea vipi watu wafurahie kutozwa kodi?
 
Na kodi zilizowekwa kwenye mafuta inahesabika wapi, huu sio ubunifuti kwa kutafuta mapato
 
Hiyo kodi ya 65000 Kwa mwaka ni sawa na shilingi 200 Kwa siku. Ni kiwango kidogo mno lakini naamini wapotoshaji watakikuza sana na kuonesha uonevu. Uzalendo ni kuhamasisha watu kulipa Kodi Kwa maendeleo yao.
shida sio kulipa Kodi, shida ni matumizi ya hizo Kodi. kuchangia mafisadi kunakera sana hata kama ni mia mbili.

Yesu ni Bwana na Mwokozi
 
Ni sawa kwani serikali kuna wakati waliwa brand kwamba wao (bodaboda)ni ma-Afisa usafirishaji.
Ni sawa walipe kodi kwa maana hata wenzao ma-Afisa ubashiri wanalipa kodi ya asilimia 18 kwa kila mkeka.
Pili, Hawa bodaboda wamekua wakijinasibu kwamba wana maisha mazuri kuliko watumishi wa umma hasa walimu.
Ni hatua stahiki wakilipa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…