TRA Portal, ni mfumo mpya unaohitaji Elimu ya kutosha na maandalizi ya mwaka mzima

TRA Portal, ni mfumo mpya unaohitaji Elimu ya kutosha na maandalizi ya mwaka mzima

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Habari ,

Nimepata taarifa kuwa, T.RA inawatangazia Watu kuwa Kuna mfumo mpya unatakiwa kuanza matumizi mwezi February 2025,

Mfumo huu unampa access ya Moja Kwa Moja mteja mwenye tin namba kuweza kubadili umiliki wa chombo chake direct kupitia mfumo mpya wa T.RA Portal .

Pia upatikanaji wa leseni, kurenew lesseni, kupoteza Kwa kadi za magari, mteja mwenyewe aweza fanya hayo KUPITIA access ya mfumo wa TR.A kupitia tin namba.

Mfumo huu ni mzuri Kwa wananchi sababu utaondoa urasimu na upotevu wa muda.

Changamoto za mfumo huu mpya ni Elimu kuwa ndogo Kwa wananchi wengi Hasa katika matumizi ya mifumo, Hasa vijijini na mijini.

Ushauri: Jambo hili liongezwe muda, mwaka huu 2025 uishe Kwa Kutoa Elimu Kwa wananchi Kisha matumizi sahihi yaanze January 2026,

Hii itaondoa upotevu wa mapato ya Serikali Kwa kuharakisha uanzaji KAZI wa mfumo huu mnamo February 2025.

Karibuni 🙏
 
Malengo ya kuandaa mifumo kama hii huwa ni mazuri. Changamoto za mfumo ni kuchukua muda mrefu kuchakata taarifa halafu mwisho wa siku ngoma inasoma "REJECTED"
 
Vishoka mnataka kuendelea kukandamiza wananchi , poleni sana
Mfumo una lengo nzuri ila unahitaji marekebisho makubwa mpaka sasa lazima utumie vishoka kwani ukijaza taarifa zako mwisho wa siku unaambiwa REJECTED, na unapigiwa simu uwasiliane taarifa zako manually.
 
Umesoma mada?
 
Sasa Fazili mbona mfumo wenyewe mleta mada kasema unaanza Feb na wewe unasema lazima utumie vishoka mara Rejected wewe umejuaje mkuu hebu tuambie maana mfumo bado haujaanza.
 
Sasa Fazili mbona mfumo wenyewe mleta mada kasema unaanza Feb na wewe unasema lazima utumie vishoka mara Rejected wewe umejuaje mkuu hebu tuambie maana mfumo bado haujaanza.
Majaribio yameshaanza,

Tarehe 20 walisema watazima mtandao uliopo, waanze majaribio UPYA, ambapo afisa wa TRA hataweza kukuhudumia Hadi mteja mwenyewe uingie kwenye mfumo uitwao Tra portal, uatach kiambatisho kupitia tin Yako, mtendaji wa TRA atapitia na kupitisha, wewe utaprint kwenye mfumo, kadi au lessen utaifuata. Sasa taona hapo watu wenye uwezo kuingia kwenye mfumo kufanya hayo yote Si Rahisi, ndipo watakimbilia Kwa agents mitaani au stationery kupata usaidizi.

Ndio maana nimeshauri Elimu itolewe mwaka huu mzima,

Mfumo uliopo uendelee, usizimwe, mifumo yote iwepo Elimu ikitolewa Hadi hapo wote tutakapoweza kuzoea.

Hii itaondoa kupoteza mapato ya tra sababu ya kutojua mfumo mpya uloletwa Kwa haraka bila maandalizi ya kutosha.
 
Sasa Fazili mbona mfumo wenyewe mleta mada kasema unaanza Feb na wewe unasema lazima utumie vishoka mara Rejected wewe umejuaje mkuu hebu tuambie maana mfumo bado haujaanza.
Mfumo huo upo tayari TRA nami niliutumia kuregister TIN number na ulikataa kwa kuleta REJECTED, na wakaniambia nimtumie mtu flani (kishoka) na anaendelea na kazi. Bado nafikiri mfumo haujakamilika na hawasemi wazi.
 
Muda zaidi unahitajika Ili Kutoa Elimu Kwa watumishi Ili kuondoa usumbufu na kuondoa uwezekano wa kupoteza mapato ya Serikali.
 
Mfumo huo upo tayari TRA nami niliutumia kuregister TIN number na ulikataa kwa kuleta REJECTED, na wakaniambia nimtumie mtu flani (kishoka) na anaendelea na kazi. Bado nafikiri mfumo haujakamilika na hawasemi wazi.
Wa Tin una afadhali, na Inawezekana kufanya online, hapo hapo unaweza kuhudumiwa Ofisini, lakini huu mpya wa magari wanasema ni tofauti, Kila kitu afanye mteja kupitia tin yake na finger print.

Ila wa kubadili umiliki wa magari, ni very complicated, Kuna kuscan documents,receipts nk nk,

Na ukikosea kidogo inagoma,

Ni jambo jema, ila linagitaji muda, na Elimu ya kutosha.
 
Sasa Fazili mbona mfumo wenyewe mleta mada kasema unaanza Feb na wewe unasema lazima utumie vishoka mara Rejected wewe umejuaje mkuu hebu tuambie maana mfumo bado haujaanza.
Wa kupata lesseni umeshaanza KAZI,

Ila wa kubadili umiliki wa magari na wa kurenew na Kutoa lesseni ndio unataka kuanza.
 
Wamezima,

Kodi kiasi Gani imepotea tangu ijumaa?

Maandalizi ni muhimu Kwa mfumo wowote mpya,

Si vyema kukurupu..
 
Mtandao umekuwa tatizo,

Wiki nzima sasa Serikali haiingizi Kodi sababu ya mfumo mpya.

Sasa tulishauri ,

Tatueni tatizo hili Hasa upande wa magari. Control number hazitoki.
 
Mfumo mbona upo poa Sana nawebsite Sasa Ina mwonekano mzuri..vitu vidogo vidogo havijakaa poa leo tu unataka kubadili umiliki wa Hari wakati walitoa tangazo...subiri waset vitu vikae poa...
 
Back
Top Bottom