Halafu waheshimiwa, nawaomba mtupunguzie usumbufu wa kuwafuata fuata kwenye ofisi zenu. Yaani ikiwezekana tukutane mara moja tu kwa mwaka; mwezi Machi, wakati wa makadirio.
Hivi haiwezekani kabisa kuwatumia wafanyabiashara control number za malipo ya kodi kupitia simu zao?
Hivi kina sababu ya msingi kweli ya mtu kuacha shughuli zake, na kufunga safari kuja kwenye ofisi zenu, kuchukua hiyo control number? Mbona mnapenda sana urasimu? Yaani hela ni ya kwangu, lakini bado natakiwa kuja kupanga foleni, na kuwalamba miguu kwanza! Ndipo nikalipie!! Badilikeni bhana.