TRA Wakanusha taarifa zilizoandikwa JamiiForums kwamba Mtandao wao Unasumbua, Waziita uzushi

Sawa, si ndio za ukweli zitolewe sasa.....
Kwani ripoti mbona waliacha kitambo hata kabla mwendazake hajaenda zake hata hatukuelezwa sababu labda baada ya akaunti walizochota mapesa ya wenyewe kukauka basi biashara ikaisha...
 
Sawa..Hilo tumewaelewa...Mbona siku hizi hamtangazi pesa mlizokusanya kama mlivyokuwa mnafanya zamani? Tutajuaje kama mnaendelea kuvuka malengo, au mko palepale au mmeshashuka chini?
Hamna mtandao, watatangaza aje?
 
Kulinda heshima ya JF, huyo aliyeleta taarifa za uzushi bila ya ushahidi wowote asiachwe bila kuwajibishwa kwa njia inayofaa watakayoona inafaa.

JF isifanywe kuwa kituo cha majungu na habari zisizokuwa na ukweli wowote.
Na waongo wa TRA nao watasafisha aje jina la JF.
 
Lawson wenyewe "nasikia" "umesizi" madaraja ya watumishi mjiandae kucheleweshwa kwa namna moja ama nyingine kama kweli taarifa hiyo ya mfumo kushindwa kufanya kazi ni sahihi
System ya Lawson ni majanga ni mwezi sasa hamna kinachofanyika ni aibu iko huko hazina na utumishi awamu hii ni kupopoma tu.
 
Huu ni utopolo kuna ofisi za TRA watu wanajibiwa majibu ya mtandao hakuna bila cctv camera ufanisi ni vibanda mchambawima na mwanamkate
 
Michadema ya JF ni wazushi hakuna mfano
Wee nae kwa kukurupuka hujambo 🤣🤣 fuatilia mamb kwanza humu, kundi lile ndilo lilikua na propaganda hizo ili tu ionekana utawala huu haufai.
 
System ya Lawson ni majanga ni mwezi sasa hamna kinachofanyika ni aibu iko huko hazina na utumishi awamu hii ni kupopoma tu.
Huu Uzi wako nzuri sana utengenezewe kichwa chake.Lawson inalalamikiwa sana hii wiki ya tatu benki zote zinalalamikia tatizo hili.
 
Huu Uzi wako nzuri sana utengenezewe kichwa chake.Lawson inalalamikiwa sana hii wiki ya tatu benki zote zinalalamikia tatizo hili.
Hakika naamini wadau wa headings walione hili ili Mchengerwa na Mwigulu walione kwa ukubwa wake.
 
Mbona sioni sign ya mwandishi wa tangazo

Taarifa hii ni gushi
 
Nadhani awamu hii ya sita inatakiwa kuwa na viongozi wakali SANA hata kuliko awamu iliyopita ya JPM.Ukweli no kwamba system zao including Used motor vehicle valuation system zilikuwa down. I was browsing and couldn't succeed. Hii ni changamoto kubwa SANA kwa wasiadizi was Mh.Rais kumpa genuine feedback ili afanye maamuzi. *Kwa nchi ambazo zinataka kupiga hatua KUBWA za mawndeleo people oriented dictatorship is inevitable coz Kuna wapigaji wengi wanaosoma upepo na kutafuta ma Gap kupiga.
 
Kwepa kodi tens weka tin yako ndiyo utajua kama ukweli au uongo mtandao Hanna.mbona kodi ya gari nimelipia Jana??
Si unabambikiwa tu, unafikiri ni mpaka ukwepe?
 
Siku moja baada ya kusambaa katika mitandao ya kijamii taarifa niliyochapisha hapa ikihusu tatizo la mtandao wa TRA nchini, TRA Makao Makuu wamekanusha taarifa hiyo. TRA wamesema kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na uzushi yenye kulenga kupotosha na kuleta taharuki miongoni mwa walipa kodi. Kwamba, katika nchi hii sasa taarifa yenye kuonesha mapungufu na kuhamasisha marekebisho inafikiriwa kuwa uongo, uzushi na uchonganishi. Tumefika mbali sana kwa muda mfupi, JPM amekwenda na mengi.

Taarifa ya TRA ya ukanusho ni ya uongo, imejaa kiburi na dharau kwa Rais wa nchi. Ni taarifa iliyofula ulevi wa madaraka, watu waungwana wangekiri udhaifu wakaomba radhi badala yake TRA wameleta jeuri. Ujumbe mahsusi unaotolewa na taarifa hiyo ya TRA ni kwamba wanamdharau Rais Samia Suluhu Hassan kwa kiwango cha juu sana. Watu waliokosa huduma siku hizo na kabla watamtazama vipi Rais wao akikubali kudanganywa kirahisi namna hii. Kama Rais Samia anataka watu wa kuonesha mfano kwamba yeye ndie Rais wa nchi aanze na TRA. Kama kuna watu wameonesha kuidharau mamlaka ya Urais wa nchi kwa kiwango cha juu kupita vyote katika nchi hii ni TRA. TRA wameonesha bila tashwishwi kwamba Rais hawezi kuwafanya lolote, hafuatilii taarifa yoyote zaidi ya kungoja za kuletewa mezani zilizopikwa na wao . Hii ni dharau yenye kupitiliza, kumdanganya Rais wa nchi nzima ni dharau kubwa kupita zote katika nchi. Ni kashfa kubwa isiyovumilika!

Nimejiuliza; kama TRA wanaweza kumdanganya Rais wa nchi katika jambo hili ambalo liko wazi, lililoonekana na kuathiri ratiba za watu, basi yako mambo mengi makubwa wanamdandanya Rais bila hofu. Tofauti kubwa kati ya Hayati Rais Magufuli na Rais Samia ni kwamba, Rais Magufuli alikua hadanganyiki kijinga na kirahisi namna hii. Angalikua Rais Magufuli huyo alieandika barua (takataka) hiyo kama ni ya kweli angalikua hana kazi hadi muda huu. Ndio maana hata barua yenyewe haina jina la mwandishi wala cheo zaidi ya Idara, mchezo uleule uliotumika kuiba hela BOT. Si ajabu mambo yaliyotokea BOT yanaweza kuwa yamefanyika kwa kiwango kikubwa zaidi TRA. Rais anakwamishwa sana!!

Watu wamenitaka nithibitishe taarifa ya kwamba TRA palikua na tatizo la mtandao kwa siku za hivi karibuni ikiwamo tarehe 26 na 27. Nimesema, sifanyi lolote katika mambo hayo wanayotaka. Siwezi kufanya kazi ya kijinga kiasi hicho. Wakati wa JPM tulipotoa taarifa za matatizo ya Serikali yake alifuatilia mwenyewe kuhakikisha na akachukua hatua hakudai ushahidi au uthibitisho. Na U-CCM wangu huu niichafue TRA ili iweje!! Nonesense.

Rais wa nchi anaweza kupata taarifa yoyote wakati wowote akitaka. Aghalabu ninaweza kumuonesha Rais namna ya kupata taarifa zenye msaada wa kuthibitisha tatizo hilo la mtandao. Akitaka kuthibitisha, Rais aombe taarifa za TRA za tarehe 26 kwa nchi nzima na tarehe 27 kwa Kimara, Mwenge na Tegeta. Achukue sample chache, aangalie kazi iliyofanyika kwa siku hizo (mahsusi), siku za nyuma na siku za baada ya taarifa yangu kwa kila afisa wa TRA hasa wenye kutoa hati za malipo (control number), makadilio (assesment), TIN na vibali vya kodi (Tax Clearence).

Endapo Rais atakuta kazi za TRA zilifanyika kama kawaida kama ambavyo taarifa ya TRA inasema, anihukumu mimi kwa kupotosha umma. Ikiwa taarifa zitaonesha kazi za TRA hazikufanyika kama kawaida, kwa tofauti itakayoonekana, Rais atajua cha kuwafanya TRA. Katika yote niliyojifunza kwa taarifa ya TRA, ni kwamba, TRA wanamdharau Rais wa nchi kupita kitu kingine chochote. Hili limeniumiza zaidi kuliko tatizo la mtandao!! Rais wa nchi nzima anapodharauliwa hadharani namna hii, tumedharauliwa wengi na nchi inabaki bila Rais.
#JesusChrist!!
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…