Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
AhahahahahahaaaUnanipangia? Naongea experience yangu huwezi kunipangia. Sijakulazimisha ukubaliane na nilicho-experience.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AhahahahahahaaaUnanipangia? Naongea experience yangu huwezi kunipangia. Sijakulazimisha ukubaliane na nilicho-experience.
Hebu waambie waje wakanushe pia kuvamia wafanyabiashara kama majambaziMichadema ya JF ni wazushi hakuna mfano
Hii taarifa ya ukanushaji imelenga nn, maana huko kwenye mitandao convetor za tra hazifanyi kazi. Maana yake ukitaka makadirio lazima uende physically ofisi za tra? Hata wenye biashara za kuagiza magari wameshindwa ku kutumia mtandao kupata makadirio na Hata muda huu nimeingia najibiwa huduma hiyo kwa sasa hapatikani. Labda nakosea naomba maelekezo plseSiku moja baada ya kusambaa katika mitandao ya kijamii taarifa niliyochapisha hapa ikihusu tatizo la mtandao wa TRA nchini, TRA Makao Makuu wamekanusha taarifa hiyo. TRA wamesema kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na uzushi yenye kulenga kupotosha na kuleta taharuki miongoni mwa walipa kodi. Kwamba, katika nchi hii sasa taarifa yenye kuonesha mapungufu na kuhamasisha marekebisho inafikiriwa kuwa uongo, uzushi na uchonganishi. Tumefika mbali sana kwa muda mfupi, JPM amekwenda na mengi.
Taarifa ya TRA ya ukanusho ni ya uongo, imejaa kiburi na dharau kwa Rais wa nchi. Ni taarifa iliyofula ulevi wa madaraka, watu waungwana wangekiri udhaifu wakaomba radhi badala yake TRA wameleta jeuri. Ujumbe mahsusi unaotolewa na taarifa hiyo ya TRA ni kwamba wanamdharau Rais Samia Suluhu Hassan kwa kiwango cha juu sana. Watu waliokosa huduma siku hizo na kabla watamtazama vipi Rais wao akikubali kudanganywa kirahisi namna hii. Kama Rais Samia anataka watu wa kuonesha mfano kwamba yeye ndie Rais wa nchi aanze na TRA. Kama kuna watu wameonesha kuidharau mamlaka ya Urais wa nchi kwa kiwango cha juu kupita vyote katika nchi hii ni TRA. TRA wameonesha bila tashwishwi kwamba Rais hawezi kuwafanya lolote, hafuatilii taarifa yoyote zaidi ya kungoja za kuletewa mezani zilizopikwa na wao . Hii ni dharau yenye kupitiliza, kumdanganya Rais wa nchi nzima ni dharau kubwa kupita zote katika nchi. Ni kashfa kubwa isiyovumilika!
Nimejiuliza; kama TRA wanaweza kumdanganya Rais wa nchi katika jambo hili ambalo liko wazi, lililoonekana na kuathiri ratiba za watu, basi yako mambo mengi makubwa wanamdandanya Rais bila hofu. Tofauti kubwa kati ya Hayati Rais Magufuli na Rais Samia ni kwamba, Rais Magufuli alikua hadanganyiki kijinga na kirahisi namna hii. Angalikua Rais Magufuli huyo alieandika barua (takataka) hiyo kama ni ya kweli angalikua hana kazi hadi muda huu. Ndio maana hata barua yenyewe haina jina la mwandishi wala cheo zaidi ya Idara, mchezo uleule uliotumika kuiba hela BOT. Si ajabu mambo yaliyotokea BOT yanaweza kuwa yamefanyika kwa kiwango kikubwa zaidi TRA. Rais anakwamishwa sana!!
Watu wamenitaka nithibitishe taarifa ya kwamba TRA palikua na tatizo la mtandao kwa siku za hivi karibuni ikiwamo tarehe 26 na 27. Nimesema, sifanyi lolote katika mambo hayo wanayotaka. Siwezi kufanya kazi ya kijinga kiasi hicho. Wakati wa JPM tulipotoa taarifa za matatizo ya Serikali yake alifuatilia mwenyewe kuhakikisha na akachukua hatua hakudai ushahidi au uthibitisho. Na U-CCM wangu huu niichafue TRA ili iweje!! Nonesense.
Rais wa nchi anaweza kupata taarifa yoyote wakati wowote akitaka. Aghalabu ninaweza kumuonesha Rais namna ya kupata taarifa zenye msaada wa kuthibitisha tatizo hilo la mtandao. Akitaka kuthibitisha, Rais aombe taarifa za TRA za tarehe 26 kwa nchi nzima na tarehe 27 kwa Kimara, Mwenge na Tegeta. Achukue sample chache, aangalie kazi iliyofanyika kwa siku hizo (mahsusi), siku za nyuma na siku za baada ya taarifa yangu kwa kila afisa wa TRA hasa wenye kutoa hati za malipo (control number), makadilio (assesment), TIN na vibali vya kodi (Tax Clearence).
Endapo Rais atakuta kazi za TRA zilifanyika kama kawaida kama ambavyo taarifa ya TRA inasema, anihukumu mimi kwa kupotosha umma. Ikiwa taarifa zitaonesha kazi za TRA hazikufanyika kama kawaida, kwa tofauti itakayoonekana, Rais atajua cha kuwafanya TRA. Katika yote niliyojifunza kwa taarifa ya TRA, ni kwamba, TRA wanamdharau Rais wa nchi kupita kitu kingine chochote. Hili limeniumiza zaidi kuliko tatizo la mtandao!! Rais wa nchi nzima anapodharauliwa hadharani namna hii, tumedharauliwa wengi na nchi inabaki bila Rais.
#JesusChrist!!
MenukaJr,
Da'slam-TanzaniaView attachment 1801131
Mbona mm nimetapaHii taarifa ya ukanushaji imelenga nn, maana huko kwenye mitandao convetor za tra hazifanyi kazi. Maana yake ukitaka makadirio lazima uende physically ofisi za tra? Hata wenye biashara za kuagiza magari wameshindwa ku kutumia mtandao kupata makadirio na Hata muda huu nimeingia najibiwa huduma hiyo kwa sasa hapatikani. Labda nakosea naomba maelekezo plse