TRA walinipigia simu mwezi Julai na kuniambia kuwa nimechaguliwa kupitia database. Hadi sasa hawajapiga tena simu, licha ya kutuambia tuandike majina yetu. Na mimi si peke yangu, wapo vijana wengine walio katika hali kama yangu.
Tulielezwa kuwa vyeti vyetu haviendani na kada tulizoomba, jambo ambalo si kweli, kwa sababu vyeti vyetu vinaendana na kada hizo. Tulipofika makao makuu, tuliambiwa tuandike majina, kada tulizoomba na namba za simu, huku tukihakikishiwa kuwa tutapigiwa simu na tusiwe na wasiwasi. Hata hivyo, hadi leo hakuna aliyewasiliana nasi.
Jambo hili limeniletea madhara makubwa. Kwa mfano, mimi niliomba ruhusa kazini nilipokuwa nafanya kazi, lakini nikanyimwa. Nililazimika kwenda kuitikia wito wa TRA licha ya kukosa ruhusa, na hatimaye nikafukuzwa kazi kwa sababu hiyo. Mpaka sasa sina kazi.
Kwa kweli, hali hii ni kero kubwa na inatuumiza sana sisi vijana tunaopambana kujitafuta. Tunaomba TRA itoe ufafanuzi kuhusu suala hili ili tujue hatma yetu na tusibaki katika hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu maisha yetu.