TRA wananiambia niingie VAT

Umemwambia sahihi
 
[emoji23][emoji23]
 
Kuanzia milioni 100 kwa mwaka VAT ni lazima, ila mkuu hongera kwa mauzo hayo na kwa mtaji ulionao unaupiga mwingi!

Ni mauzo ya 302,000/= wenye maduka ya simu wana simi za 400000 huko kuingia VAT ni kugusa mkuu
 
Muongo

TIN husajiliwa kwa alama za vidole au NIDA
TIN lazima uende kukadiriwa ili upewe ya biashara
TIN ya Msimbazi huwezi itumia Tegeta
 
Kwani shida iko wapi kwani unapocalculate vat unakua hujajua faida yako nachojua VAT analipa mnunuaji we muuzaji unaisaidia TRA kuikusanya
Usisahau unakusanya bila malipo na ww kuna gharama unaingia za kukusanya na kutuma ripoti. Ukichelewa tu kutuma hiyo faini hutaamini.
 
Mi nilikuwa natoa risiti nahakikisha haizidi 5mil kwa mwezi
Na risiti zinatolewa kwa Makampuni pekee, binafsi hupewi
Boss ni kuwa makini:

Shida ya huu mchezo baada ya miaka kadhaa Utajikaanga kwenye manunuzi na matumizi na siku wakikufanyia examination watakuumiza.

Sikia boss, unahitaji akili sana kuwadanganya TRA maana sio mafala. Unless ww sio mkubwa na mara nyingi hawaangaiki na examination ya data zako.

Kama unatoa risiti pungufu hakikisha na wewe unapokea risiti pungufu, una matumizi pungufu, faida pungufu sababu wanatumia mbinu ya kupima uwiano kati ya mauzo, manunuzi, faida na gharama za biashara.

Huwezi liona hili mpaka siku ukijifanyia analyis ndefu, miez m3 sita au mwaka na ukawa na jicho la kihasibu ndipo utaona hizo gapes.

Sasa sheria inawaruhusu TRA kufanya examination hata miaka 5 nyuma. Na wakikufanyia mtu wa aina yako watajiuliza tu haya maswali:

Kwann huyu mtu ana mauzo machache ila anafanya manunuzi kuongeza mzigo ambao upo stoo hauuzi?

Kama wewe ni smart kwamba hata manunuzi huchukui risiti linakuja swali la pili.

Kwanini huyu mtu ana manunuzi machache, mauzo machache ila gharama za uendeshaji ni kubwa?

Kama wewe ni smart kuficha manunuzi, mauzo na gharama, sheria inaaruhusu kuchungulia miamala yako na swali lingine linakuja

Kwann huyu mtu ana mauzo madogo, gharama sio kubwa, manunuzi madogo ila mzunguko wa fedha bank na mpesa,tigo pesa huko ni mkubwa?

Kama hupeleki pesa bank au tigo pesa huko mwonekano wa biashara yako unaweza ukakusaliti kutegemeana na eneo la biashara sababu serikali inaelewa nchi yake kila sehemu na mzunguko ulivyo.

Ukifanya kilakitu kwa 100% unaweza ukaumia na ukafunga biashara, ila ukiitafuna sana serikali basi uombe miaka 5 ipite bila ukaguzi otherwise watakutafuna wao.

TANZANIA MFANYABIASHARA WA DRS LA SABA ANA AKILI KULIKO GRADUATE WA DEGREE FIELD HUSIKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…