TRA wananiambia niingie VAT


Nikipokea receipt Haina TIN namba nani anajua ni ya kwangu?
 
TRA wanaangalia mauzo tu,faida utajua wewe na Mungu wako!
Hii ni kwa sisi wafanya biashara wadogo, kampuni kubwa wanawasilisha hesabu zote za gharama ya uendeshaji na kiasi cha faida. Kodi inatoka kwenye faida wanayopata, na kuna wakati hawalipi kodi wanapowasilisha hesabu ya zero profit au minus profit kabisa
 
Service business haina manunuzi makubwa ati
 
Inamaana wanachukua 18% toka faida inayobaki baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji?
 
Ukifikia tu mauzo ya milioni 100 automatically unakuwa qualified kuwa Vat collector.
 
TRA wanamatatizo sana,
Tatizo kubwa hawatoi elimu kabisa watu wanahangaika kutafuta elimu wenyewe.Na hili wanalifanya kusudi ili wapate mwanya wa kuwatisha watu wawape rushwa.

Kikiubwa inapswa iwe wazi namna wanavyokokotoa 18% ya VAT,je wanapiga kwenye mauzo ama kwenye faida?

Kama VAT itakua inafanyiwa hesabu kwenye mauzo huu utakua ni wendawazimu,ila kama watakua wanafanya hesabu kwenye faida si mbaya.

Chukua mfano Mimi na Juma tuwe na biashara zinazo fanana kwa kila namna,Mimi niwe kwenye VAT na Juma awe kwenye kodi ya mapato,bidhaa ikiwa na thamani mf 10,000/=,nitalazimika kuweka 18% ya VAT ambayo ni 1800/=,nikiijumlisha kwenye bei nitalazimika niuze 11800,

Kwa mfano huo wa mimi na juma utaona kwamba Juma yeye kwakua hayupo kwenye VAT anauwezo wakuuza kwa 11,000 akapata faida ya 1000,je .Mimi nitapata wateja?

Hii ndio hofu ya mtoa mada na wafanyabiashara wengi.

Tatizo kubwa kwenye biashara, ni hizi mambo za kutengeneza makundi,kama ilivyosasa hawa wa VAT na hawa sio wa VAT.Hapa kuna leta unfair competition na hili ndio tatizo kubwa linaloua biashara za watu.

Kinachotakiwa watu wote wawekwe kwenye mfumo mmoja,mfano watu wote wawe kwenye VAT na wote wawe na EFD machine.Na hizi machine zitolewe bure TRA.

Unfair competition inaua sana biashara,naamini kama kila mfanya biashara akipewa EFD mashine inawezekana kabisa VAT ikashuka hata 5% na makusanyo yakawa maradufu kuliko ilivyosasa.
 
Technically ukiingia VAT serikali inakutumia wewe kuchukua kodi kutoka kwa wanunuzi. Hivyo sio kitu kibaya especially kama biashara yako ni Limited Liability Company
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…