Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mimi ni miongoni mwa watu naopinga sana madalali kutaka kulipwa kodi ya mwezi mmoja kwani ni kuumiza wapangaji kwa kuwaongezea gharama za maisha. Kibaya zaidi, wako wenye nyumba hawapangishi mtu bila kupitia madalali wao hata kama inawezekana kupanga bila kupitia hao madalali.
Hivyo, nakubaliana na Lukuvi wenye nyumba wawalipe madalali na jambo hili litungiwe sheria na sheria itoe adhabu ya kifungo au faini au vyote kwa pamoja kwa atakaekaidi.
Sambamba na hilo, TRA waanzishe kitengo cha upangishaji nyumba ambapo wenye nyumba watatakiwa kutoa taarifa TRA wanapotaka kupangisha, kisha jukumu la kutafuta wapangaji liwe la TRA, ila mwenye nyumba aruhusiwe kuweka mpangaji bila kupitia TRA mradi tu alipe kodi.
Utaratibu huu ukiwekwa kisheria, sio tu utaondoa unyonyaji wa madalali, bali uta-facilitate ukusanyaji wa kodi kupitia nyumba za kupangisha na ambao teyari upo kwa mujibu sheria.
Mwanachi yoyote anaetaka nyumba ya kupangisha, atakiwe(kwa mujibu wa sheria) kufika katika ofisi za TRA, na kisha TRA kupitia kitengo husika, watakuwa na jukumu la kuwapangisha wananchi na hapo hapo kukusanya kodi ya serikali.
Tena TRA wanaweza kufanya kazi hii katika mazingira bora zaidi kwa kuwapeleka wateja kwa kutumia magari yao, pikipiki au bajaji maalumu ziitazonunuliwa kwa kutumika fedha zitazokusanywa kupitia upangishaji wa aina hii.
Hakuna kinachoshindikana kama dhamira ipo. Kama kupata baadhi ya huduma tunalazjmika kwanza kupitia TRA, kwani hili la kupangisha kupitia TRA lishindikane?
Haingiii akilini hata kidogo kwa mtumishi wa serikali mwenye mshahara wa shilingi 300,000 kwa mwezi, alipe kodi(PAYE), halafu dalali au mwenye nyumba anaeingiza malaki au mamilion kadhaa anapopangisha, asilipe kodi(huu ni uwendawazimu kabisa).
Tulipendekeza hili hakuna kilichiofanyika, hivyo TRA waingie kazini.
www.jamiiforums.com

Madalali wasajiliwe na walipee kodi
Wakati umefika tuwe na sheria ya kutaka madalali wasajiliwe na walipe kodi kwani licha ya kuingiza kipato kupitia udalali, wanaongezea watu gharama za maisha huko wao hawalipwi kodi. Dalali akikutafutia nyumba/chumba, unatakiwa umlipe kodi ya mwezi mmoja mbali na kodi unayopaswa kumlipa mwenye...