TRA waunde kitengo cha upangishaji wa nyumba, kila mwenye nyumba aripoti TRA anapotaka kupangisha na iwe kwa mujibu wa sheria

TRA waunde kitengo cha upangishaji wa nyumba, kila mwenye nyumba aripoti TRA anapotaka kupangisha na iwe kwa mujibu wa sheria

Makamouni ya simu yanafanya biashara yenye kupata faida

Ulisikia wapi mwenye nyumba ya kupangisha kwa makazi anapata faida wewe?
Kwani mtumishi wa umma anaelipa PAYE anafanya biashara gani ya kupata faida kupitia hiyo kazi alioajiriwa na serikali?
 
Umekaa sijui chumba ca kupanga, Sijui kea shemeji yako.

Umeshiba kiporo Cha makande unaanza kuwadis walotoka jasho kugharamikia usingizini wako kiazi wewe.

Yaan,
Ungejua Ni jins gani ujenzi unaumiza Wala usingethubutu kuongea Ayo maneno yako mbofu mbofu.

Jenga nyumba yako afu uje Tena na huu utopolo wako humu.
Naunga hoja mkuuu. Unakuta mtu mpaka leo anaumri wa miaka45 bado anakaa kwa anakaa kwa shemeji yake atajuaje ugum na mateso ya ujenzi
 
Acha ujuaji babu kuna hoja za msingi za jamaa hujajibu, yaani kwa kutumia gharama zangu mwenyewe nitafute nyumba, nimepata mwenye nyumba kasema anapangisha kwa mwezi laki2 na nusu kwa mwezi, ila kabla sijafunga naye mkataba analazimisha dalali wake awepo na nimlipe laki2 na nusu huyo dalali kwa kazi gani aliyofanya? Huu ndo upumbavu tunaukataa sie.
Kama umetumia gharama zako kutafuta nyumba mguu kwa mguu.

Apo mwenye nyumba anakua hajakutendea Haki kabisa
 
Ndicho anachotaka TRA wawe wanazurura mitaani kutafuta Nani anapangosha chumba kina umeme au hakina ? Cha uani au Cha ndani?
Labda Kama anaongelea tra ya Burundi.

Hiyo kitu Ni impossible
 
Mtumishi wa umma mwenye mshahara wa shilingi 300,000 kwa mwezi, analipa kodi, halafu dalali anaepangisha na kulipwa kodi ya mwezi(shilingi 300,000, 400,000 na kuendelea) halipi chochote na tunaona sawa tu.

Tanzania nchi ya ajabu sana!
Sasa mbona unakua Kama vile unawaonea sana wivu madalali,

Basi acha huo utumishi wako na wewe ukawe dalali.

Au umezuiwa mkuu?[emoji2]

Ni Kama yule anayesema mlinzi BOT analipwa mil 10,
afu daktari wilayani analipwa laki 8 .

Basi na wewe acha udsktari ukawe mlinzi uko BOT[emoji12]
 
Sisi Wakazi wa TMK tumeshakaa na tunataka tufanye mambo yetu Online, Mkuu wetu wa Wilaya ndio haonekani kutupa baraka zake.
 
Mimi ni miongoni mwa watu naopinga sana madalali kutaka kulipwa kodi ya mwezi mmoja kwani ni kuumiza wapangaji kwa kuwaongezea gharama za maisha. Kibaya zaidi, wako wenye nyumba hawapangishi mtu bila kupitia madalali wao hata kama inawezekana kupanga bila kupitia hao madalali.

Hivyo, nakubaliana na Lukuvi wenye nyumba wawalipe madalali na jambo hili litungiwe sheria na sheria itoe adhabu ya kifungo au faini au vyote kwa pamoja kwa atakaekaidi.

Sambamba na hilo, TRA waanzishe kitengo cha upangishaji nyumba ambapo wenye nyumba watatakiwa kutoa taarifa TRA wanapotaka kupangisha, kisha jukumu la kutafuta wapangaji liwe la TRA, ila mwenye nyumba aruhusiwe kuweka mpangaji bila kupitia TRA mradi tu alipe kodi.

Utaratibu huu ukiwekwa kisheria, sio tu utaondoa unyonyaji wa madalali, bali uta-facilitate ukusanyaji wa kodi kupitia nyumba za kupangisha na ambao teyari upo kwa mujibu sheria.

Mwanachi yoyote anaetaka nyumba ya kupangisha, atakiwe(kwa mujibu wa sheria) kufika katika ofisi za TRA, na kisha TRA kupitia kitengo husika, watakuwa na jukumu la kuwapangisha wananchi na hapo hapo kukusanya kodi ya serikali.

Tena TRA wanaweza kufanya kazi hii katika mazingira bora zaidi kwa kuwapeleka wateja kwa kutumia magari yao, pikipiki au bajaji maalumu ziitazonunuliwa kwa kutumika fedha zitazokusanywa kupitia upangishaji wa aina hii.

Hakuna kinachoshindikana kama dhamira ipo. Kama kupata baadhi ya huduma tunalazjmika kwanza kupitia TRA, kwani hili la kupangisha kupitia TRA lishindikane?

Haingiii akilini hata kidogo kwa mtumishi wa serikali mwenye mshahara wa shilingi 300,000 kwa mwezi, alipe kodi(PAYE), halafu dalali au mwenye nyumba anaeingiza malaki au mamilion kadhaa anapopangisha, asilipe kodi(huu ni uwendawazimu kabisa).
Umesoma hadi darasa la ngapi?
 
Mifumo ikiwekwa vizuri hata nyumba iliyopo nyayoni mwa Tanzania ikipangishwa, kodi TRA watalipwa tu nielewe nimesema mifumo ikiwekwa vizuri. Aisee kuna nchi wana msemo wao kuwa ukikanyaga ardhi ya nchi yao kuna vitu viwili hakika huwezi kwepa hata ufanyeje ni suala la muda tu vitu hivi vitakupata kwanza ni kifo pili ni kulipa kodi. Hivi kwa mfano wabunge watunge sheria kuwa mpangaji akikwepa kupeleka kodi ya zuio toka kwenye kodi aliyomlipa mwenye nyumba atapata kifungo cha miaka kadhaa jela au let say atalipa faini ambayo ni sawa na kodi ya hiyo nyumba aliyopanga ya miezi sita au mwaka we unafikiri nan kweupeee atakwepa kupeleka hiyo kodi ya zuio?

Unajua nchi zilizoendelea sio kwamba wananchi wake wanapenda saaaaaana kulipa kodi but wamewekewa mifumo ambayo kukwepa kodi na kutokujulikana kabisaa ni ngumu sana so automatically wanajikuta kodi wanalipa tu.

Sawa, ila kaa ukijua TRA wenyewe ni moja ya taasi failure hapa nchini..
Sio kila kazi wafanye wenyewe, sema labda tungesajili madalali ili nao walipe kodi, maana kumbuka mwenye nyumba analipa kodi kupitia kodi ya majengo.
 
Ikiwezekana warasimishwe kabisa. Mm nauheshimu sana udalali.
kazi iyo vijana wengi wapo humo na wanamiliki nyumba na magari ni mwanangu kaoa juzi yeye kapanga nyumba nzima kama laki 4 na nusu kwa kazi iyo iyo
 
Kwani mtumishi wa umma anaelipa PAYE anafanya biashara gani ya kupata faida kupitia hiyo kazi alioajiriwa na serikali?
Kwanza nyie watumishi hizi nyumba zetu za mitaani sidhani Kama zinawahusu kabisa.

Nyie enzi za nyerere na mwinyi mlikua mnajengewa kabisa nyumba zenu za KOTA au kulipwa posho ya makazi afu mnatafuta nyumba uku mitaani.

Kwaiyo manung'uniko yenu iltakiwa muiambie serikali yenu ya CCM iwajengee nyumba za watumishi Kama zamani au wawape posho za makazi.

Na sio kama hivi kuleta Shari na wananchi wanyonge wasioujua huo mshahara wenu wa mwisho wa mwezi.
 
kazi iyo vijana wengi wapo humo na wanamiliki nyumba na magari ni mwanangu kaoa juzi yeye kapanga nyumba nzima kama laki 4 na nusu kwa kazi iyo iyo
Naelewa. Mtu yoyote aliyekulia mtaani anajua udalali unaweza kukutoa kimaisha. Esp kwenye property sales.
 
Nauli ya kuzunguka kukutafutia nyumba nzuri dalali huwa unamlipa wewe?
tuache kutetea ujinga.
huo upuuzi upo tanzania peke yake.
nairobi huwezi kusikia takataka inaitwa dalali wa nyumba.

kama nyumba ipo empty na inahitaji mpangaji mpya, ukipita tu nje ya geti, utaona kibao chenye namba ya simu ya landlord au caretaker(mtu aliyekabidhiwa jukumu la kuitunza nyumba), kinachoonyesha kwamba nyumba hii inahitaji mpangaji.

ukipiga simu inapokelewa haraka na unapewa ushirikiano wa kutosha. landlord au caretaker atakuchukua kwenda kukagua. huduma ya kukagua huwa ni bure. sio kama tanzania ambapo hata kwenda kukagua, madalali wanataka uwalipe ya usumbufu.

nairobi huhitaji kumtuma mtu akutafutie nyumba, wewe mwenyewe unaingia mtaani kujitafutia pa kuishi. halafu sio lazima ulipe rent ya miezi mitatu au sita. wenzetu inalipwa kwa mwezi.
 
Mimi ni miongoni mwa watu naopinga sana madalali kutaka kulipwa kodi ya mwezi mmoja kwani ni kuumiza wapangaji kwa kuwaongezea gharama za maisha. Kibaya zaidi, wako wenye nyumba hawapangishi mtu bila kupitia madalali wao hata kama inawezekana kupanga bila kupitia hao madalali.

Hivyo, nakubaliana na Lukuvi wenye nyumba wawalipe madalali na jambo hili litungiwe sheria na sheria itoe adhabu ya kifungo au faini au vyote kwa pamoja kwa atakaekaidi.

Sambamba na hilo, TRA waanzishe kitengo cha upangishaji nyumba ambapo wenye nyumba watatakiwa kutoa taarifa TRA wanapotaka kupangisha, kisha jukumu la kutafuta wapangaji liwe la TRA, ila mwenye nyumba aruhusiwe kuweka mpangaji bila kupitia TRA mradi tu alipe kodi.

Utaratibu huu ukiwekwa kisheria, sio tu utaondoa unyonyaji wa madalali, bali uta-facilitate ukusanyaji wa kodi kupitia nyumba za kupangisha na ambao teyari upo kwa mujibu sheria.

Mwanachi yoyote anaetaka nyumba ya kupangisha, atakiwe(kwa mujibu wa sheria) kufika katika ofisi za TRA, na kisha TRA kupitia kitengo husika, watakuwa na jukumu la kuwapangisha wananchi na hapo hapo kukusanya kodi ya serikali.

Tena TRA wanaweza kufanya kazi hii katika mazingira bora zaidi kwa kuwapeleka wateja kwa kutumia magari yao, pikipiki au bajaji maalumu ziitazonunuliwa kwa kutumika fedha zitazokusanywa kupitia upangishaji wa aina hii.

Hakuna kinachoshindikana kama dhamira ipo. Kama kupata baadhi ya huduma tunalazjmika kwanza kupitia TRA, kwani hili la kupangisha kupitia TRA lishindikane?

Haingiii akilini hata kidogo kwa mtumishi wa serikali mwenye mshahara wa shilingi 300,000 kwa mwezi, alipe kodi(PAYE), halafu dalali au mwenye nyumba anaeingiza malaki au mamilion kadhaa anapopangisha, asilipe kodi(huu ni uwendawazimu kabisa).
Wenye nyumba wanalipa kodi,inaitwa With holding Tax,mpangaji huwa analipa kwa niaba ya mwenye nyumba,inaitwa with holding tax(kodi ya zuio),halafu wanakatana kwenye kodi.
 
Naunga hoja mkuuu. Unakuta mtu mpaka leo anaumri wa miaka45 bado anakaa kwa anakaa kwa shemeji yake atajuaje ugum na mateso ya ujenzi
Kabisa mkuu,
Na Ndo maana mwenye nyumba anaheshimika sana.

Ujenzi unaumiza.
 
udalali ni ajira labda waweke regulation dhidi yao sio TRA kuchukua jukumu vijana wengi wamejiajiri huku acheni mawazo potofu ukilipa ya mwezi ni fresh kwani unalipa tena
Fanya kazi kijana nyie ndio mnaliwa mande kwa kutaka vitonga
 
Back
Top Bottom