Abuu hanifa
JF-Expert Member
- Aug 17, 2021
- 256
- 275
Mimi ni miongoni mwa watu naopinga sana madalali kutaka kulipwa kodi ya mwezi mmoja kwani ni kuumiza wapangaji kwa kuwaongezea gharama za maisha. Kibaya zaidi, wako wenye nyumba hawapangishi mtu bila kupitia madalali wao hata kama inawezekana kupanga bila kupitia hao madalali.
Hivyo, nakubaliana na Lukuvi wenye nyumba wawalipe madalali na jambo hili litungiwe sheria na sheria itoe adhabu ya kifungo au faini au vyote kwa pamoja kwa atakaekaidi.
Wazo zuri. Hili naliandika ktk diary yangu bali litakuwa na marekebisho madogo. Nitagombea Urais 2025 tukiwa hai. Nikishinda urais kwanza nyumba zote zilizotaifishwa na Serikali nitazirudisha kwa wamiliki, nyumba zote zilizojemgwa na serikali wanasiasa wakauziana nitazitaifisha na kumilikiwa na sheirika la nyumba. Utaanzishwa sheria ya upangaji ili mpangaji alipe kodi kwa mwezi na isizidi kodi ya miezi miwili. Yaani mwezi mmoja na mwezi unaofata. Na mwezi unaofata utalipa mwezi mmoja mmoja. Na iwe sheria kutolipwa Kofi kwa siku 60 ni sawa na kumwambia mwenye nyumba kuwa hutoendelea kupanga na anahaki ya kuleta mpangaji mwengine. Ila kwa huruma yake anaweza kukuvumilia.
Usimamizi wa walipa Kofi utakuwa chini ya hamlshauri na wenyeviti wa serikali za mitaa badala ya TRA.
Moja ya Sera ktk chama nitakachogombea kitafata Serikali ya majimbo 10 (autonomous) yatakayopewa mamlaka zaidi ya kujiamulia mambo yao wenyewe sawa na mamlaka yaliyopo jimbo la Zanzibar ktk mfumo wa serikali ya ccm.
Na majimbo hayo 10 tutayapa mamlaka zaidi ya jimbo la Znz kwasasa