TRA waunde kitengo cha upangishaji wa nyumba, kila mwenye nyumba aripoti TRA anapotaka kupangisha na iwe kwa mujibu wa sheria

Mnataka kuingilia ajira za watu, kwani mpangaji kalazimishwa kutoa hela si katoa kwa hiari yake

Serikali kama umeshindwa kukidhi ajira za watu wake ikae pembeni
 
Bora kuwe na kitengo serikali za mitaa kwaajili ya kuratibu wapangaji na wapangishaji ambao watakuwa na full data za nyumba ambazo zinahitaji wapangaji na walipwe na serikali iwe ni ajira rasmi na walipwe mshahara kwa skeli za serikali
Issue sio kujua nyumba ipi inapangishwa Kuna swala la kumjua mpangaji

Mtu hawezi tu toka kigoma anafika dar anakuja direct kwKo mwenye nyumba kuwa nataka kupangisha chumba humo ndani humjui .Laweza kuwa jambazi toka burundi likakukaba usiku .Ndio maana Wenye nyumba hutaka mtu aletwe na dalali.Madalali ndio hubeba hiyo risk ya huyo anayemleta.

Ndio maana asilimia kubwa ya wapangaji huwa lazima wapitie kwa dalali kwa ajili ya KYC yaani know your customer.Madalali wako vizuri eneo Hilo

Hata iwe nyumba ya makuti mfano Dar sio rahisi ukaenda Moja kwa moja kwa mwenye nyumba akakupangisha hata awe na shida vipi hakupangishi anakwambia siwezi pangisha jitu silijui Laweza kuwa limefanya uhalifu huko linakuja kujiegesha kwangu
 
CC: Mwigulu Nchemba
 
JENGA YA KWAKO PANGISHA JIPELEKE TRA
 
Hao TRA wapangishe nyumba wasizozimiliki?
Unajua idadi ya Ofisi za TRA katika kila wilaya ziko ngapi?
Majukumu ya TRA unayafahamu?
Idadi ya watumishi wa hizo ofisi pia umezingatia?
 
Dawa ni wajumbe wa nyumba kumi wawe ni maajent wa tra huku tra ikiwachia 10/100 ya rent.formalities zitengenezwe vizuri
 
Udalali ni ajira labda waweke regulation dhidi yao sio TRA kuchukua jukumu vijana wengi wamejiajiri huku acheni mawazo potofu ukilipa ya mwezi ni fresh kwani unalipa tena
Alafu Kuna jambo watu hatujui,unajua serikali imewekwa na raia na inaishi kwa Kodi za raia wakazi,unajua ni jukumu la serikali kuhakikisha Kila raia wake anakula,anavaa na ana mahali pa kulala,hivyo basi wale wote wanapaswa kupewa motisha zaidi Ili nyumba zijengwe zaidi na si demotivate kwa kuziwekee Kodi na masharti mengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…