TRA ya USA waruhusiwa kuua ikibidi kukusanya kodi ya Serikali

TRA ya USA waruhusiwa kuua ikibidi kukusanya kodi ya Serikali

Kwa uchumi wa Tanzania,,TRA INGEKUWA INAKUSANY TRILLION 30..WANJISIFIA KWA KUJIWEKEA TARGET KIDOGO
Ingekuwa inakusanya wakati hamtaki kudai risiti mkienda kufanya manunuzi hadi mlazimishwe?

Mimi wakati wote nimekuwa napenda kuwepo task force kubwa ya ku enforce jamii idai risiti Kwa kila manunuzi badala ya kukadiriana makodi makubwa..
 
Hakuna TRA Marekani,tafuta jina la Revenue Authority ya Marekani ndipo uandike.
Huwa mnawahi kuandika posti bila kujipanga.

Labda wewe ndiyo haujajipanga kusoma na kuelewa kilichoandikwa, kwani TRA ni nini nan kazi yake ni nini?
 
Nchi inajengwa kiharamia??!!, kweli Wahenga walisema; "Usione utajiri wa mtu ukautamani kwani huwezijua undani wake".

Amerika licha ya kujidai kwamba inalinda haki na demokrasia za watu na Raia lakini wakati fulani inashindwa kufuata njia za kimahakama kuwahukumu watu wake bali inawakung'uta risasi Kwa ajili ya utajiri !!, utajiri unayo thamani kubwa kuliko utu!!!--- yawezekana ni katika muktadha huo huo ndivyo alivyofanyiwa George Floyd na ni katika muktadha huo huo Amerika wamekuwa wakivamia nchi mbalimbali na kuua raia kwa kisingizio cha kuleta Demokrasia kumbe ni kwa ajili kupora mali kwa njia ya; "kukusanya kodi/mapato popote hata ikibidi kuua", The USA is a satanic bloody hands rich country.
Don't be naive,hakuna nchi isiyoua,katika kulinda maslahi makubwa ya wananchi na vizazi vijavyo.
Hata hapa bongo,ccm inaua kila leo Ili ibaki Madarakani,walijaribu kumuua Tundu lisu mchana kweupe,Utawala wa Mwinyi ulimuua stanslaus katabalo baada ya kugundua wizi wa dhahabu uliokuwa ukifanywa na familia ya Mwinyi.
Umeishawahi kujiuliza kwa nini US haiivamii Japan,South Korea,Austaria,South Afrika,Philippine,India,Pakistan!?
Dunia ya leo lazima ulinde maslahi yako,lazima ufanye ujasusi wa kiuchumi,wengine wafe,wewe upone.
Kiwanda chetu Cha General tyre kiliuliwa kijasusi na Kenya,wao wakafungua kwao kinaitwa Yana tyre!unalijua Hilo?mpaka kesho Kenya watahakikisha Hiki Cha kwetu hakiponi.
Usiwalaumu US,wanalinda maslahi yao na siku zao za usoni.
Ukikutana na Simba,ukamwambia "Simba Mimi ni mnyonge usiniue,wafate wengine"kwanza atakushangaa,lazima akulalue!!
Ukitaka heshima,usisubili kupewa,itafute kwa lazima,kama anavyofanya Iran,Urusi,North Korea,Palestine Authority,nk.
 
Mnyonge gani ambae anakuwa na account bank? Pili kwenye miamala ya simu tozo ni 42% tuu..

Jingine mapato ya mnyonge wako yameongezeka mara dufu kufuatia kuongeka Kwa bei ya Mazao ambayo mliharibu..

Kamuulize leo mnyonge WA kijijini kwamba anataka kipi Bei ya Mazao iwe mbaya au iwe juu atakujibu.

Kwenye kilimo Cha mnyonge kafuta tozo 52 na katoa ruzuku juu..Wewe si unajua kusoma haya niambie hapa chini pameandikwaje👇
Sasa haya maswala ya kujiandikisha Ili upewe mbolea ya ruzuku ya nini?mbolea kama ina subsides,iuzwe tu,watu wanunue huko walipo walime,mambo ya kujiandikisha ni kuturudisha kwenye ujamaa,
 
Trump forma USA president, yupo kikaangoni tuhuma Kampuni zake kukwepa Kodi!
Kiukweli wenzetu wapo serious na mambo ya Msingi, tuna mengi Mazuri ya kujifunza, mbali ya machache ya kupuuza Kama ushoga.
 
"To use deadly force,if necessary"hii haimaniishi kuua,hii idara ni zaidi ya idsra ya mapato,hawa wanabeba siraha,TRA bongo sio polisi Wala hawana mafunzo ya kutumia siraha kama takes la kazi,
Be willing to arrests,execution of warrants,Hili ni takwa kama la takukuru,sio TRA,
Hawa kazi yao sio kukusanya mapato,kazi yao ni kuzuia magendo,utakatishaji pesa,wanafanya kazi kama polisi,kwa hapa bongo ni Sawa na kikosi Cha KMKM,kikosi maalum Cha kuzuia magendo,kule Zenj,na kule Zenj idara ya mapato ni ZRB,ZRB hawabebi siraha,Wala hawaenendi kama idara ya polisi,ni civilian entity,kwenye majukumu yao huwa na polisi,lakini KMKM Hawa Wana vaaa combat Wana mafunzo ya kijeshi,Wana zuia magendo na pesa haramu,Sawa sawa na IRS,
IRS sio idsra ya mapato,kwa sababu ni law enforcement entity,Wana haki ya kubeba siraha,na kukamata kipolisi,Hawa ni Sawa na KMKM sio kama ZRB,Zanzibar revenue bureau,au TRA ya bara.

Eti IRS sio idara ya mapato! Huu ni uvivu wa kufikiria au uvivu wa kutafiti? Unajua hata kirefu cha IRS kweli?

Sema, kwa Marekani, federal government agencies na levels zote za serikali (state na local) zina law enforcement units zake. Hawana utamaduni wa kutegemea police force moja nchi nzima!
 
Don't be naive,hakuna nchi isiyoua,katika kulinda maslahi makubwa ya wananchi na vizazi vijavyo.
Hata hapa bongo,ccm inaua kila leo Ili ibaki Madarakani,walijaribu kumuua Tundu lisu mchana kweupe,Utawala wa Mwinyi ulimuua stanslaus katabalo baada ya kugundua wizi wa dhahabu uliokuwa ukifanywa na familia ya Mwinyi.
Umeishawahi kujiuliza kwa nini US haiivamii Japan,South Korea,Austaria,South Afrika,Philippine,India,Pakistan!?
Dunia ya leo lazima ulinde maslahi yako,lazima ufanye ujasusi wa kiuchumi,wengine wafe,wewe upone.
Kiwanda chetu Cha General tyre kiliuliwa kijasusi na Kenya,wao wakafungua kwao kinaitwa Yana tyre!unalijua Hilo?mpaka kesho Kenya watahakikisha Hiki Cha kwetu hakiponi.
Usiwalaumu US,wanalinda maslahi yao na siku zao za usoni.
Ukikutana na Simba,ukamwambia "Simba Mimi ni mnyonge usiniue,wafate wengine"kwanza atakushangaa,lazima akulalue!!
Ukitaka heshima,usisubili kupewa,itafute kwa lazima,kama anavyofanya Iran,Urusi,North Korea,Palestine Authority,nk.

Mimi sielewi umeandika kitu gani!!, mimi nasema; America aache kujipachika cheo cha polisi wa dunia katika kulinda the so called Haki za kiraia na Demokrasia duniani ilhali kwake mwenyewe hakuna haki hizo. Aache undumilakuwili na kwanza ajishughulishe na mambo ya nyumbani kwake.
 
Back
Top Bottom