Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 490
- 704
Naona lile zoezi la TRA la kamata wote kumbe kweli du, kumbe wapo kweli kazini naona matukio jana walikuwa Jangwani na Kariakoo yaani ukiwa hujatoa risiti au hujaomba risiti unao.
#TEGETA Maafisa wa TRA Mkoa wa kodi wa Tegeta leo 03/02/2022 wameendelea na zoezi la ukaguzi wa risiti za #EFD kwa Wafanyabiashara na wanunuzi ikiwa ni kampeni maalum ya #KAMATAWOTE yenye nia ya kuhamasisha utoaji na kudai risiti za EFD.
#MTWARA Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mtwara leo imeendeleza kampeni ya #KAMATAWOTE ambapo baadhi ya wateja wasiodai risiti za EFD walisisitizwa kudai risiti halali ikiwemo wauzaji kutoa risiti kulingana na mauzo walioyafanya kwa wateja wao.
#KARIAKOO Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Janeth Mtimba (kulia) akichukua taarifa za mzigo wa mfanyabiashara ambaye hakua na risiti za #EFD za mzigo alonunua na kupakia katika lori wakati wa kampeni ya #KAMATAWOTE Jangwani, jijini Dar es Salaam.