TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

Mwingereza

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
1,115
Reaction score
2,771
Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya Waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha.

Waturuki walitegemea kupata mkopo kwenye moja ya mabenki ya ndani, kitu ambacho kimechelewa. Mategemeo yao ilikuwa ni kupata mkopo mwezi wa 4 lakini hadi Desemba mkopo ulikuwa bado haujapitishwa. Kwa maana hiyo hawakuwa na jinsi ya kuanza operations zao.

Hii kampuni ipo maeneo ya Mbezi Afrikana na kwa bahati mbaya, magari ya TRA wamevamia jioni hii na kufunga ile ofisi na kumchukua mtu anayesimamia ile mali maana wengine inaonekana wako nje ya nchi. Na kwa sababu hakuna kazi, ni mmoja wao amebakia pale kulinda mali.
 
Nilifungua biashara nikapewa makadirio kama kawaida nikalipa awamu ya kwanza, biashara haikufanya vizuri kutokana na eneo awamu ya pili wakaendelea kunidai, biashara ikafa kwa kulipa mikodi na nadaiwa mpaka sahivi mapato mengine, nimefunga biashara, sijui kwanini TRA wasiwe USER FRIEND na walipa kodi, sahivi nataka kufungua biashara ingine mkoa mwingine naambiwa maliza kwanza deni la awali na uombe maombi ya kuhamisha TIN
 
Stupid move.
Hapo mnataka kuniambia kuna mturuki ataleta pua yake tena hapa TZ?
They will come when meko is gone
Kwa kweli mifumo ya ulipaji kodi ni ya kipuuzi, halafu kutwa tunaambiwa na kushauriwa jiajirini kujenga uchumi wa taifa, ajira itabaki kuwa tamu aisehh kuliko unajiajiri na kuacha ajira ukitegemea kujiajiri kutafanya vizuri unajikuta unakua masikini zaidi, serikali waliangalie hili.
 
Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha....
Nchi ya kijiima hii old stone age.
Banana Republic.
Forgive and forget it, to hell with it.
 
Nilifungua biashara nikapewa makadirio kama kawaida nikalipa awamu ya kwanza, biashara haikufanya vizuri kutokana na eneo awamu ya pili wakaendelea kunidai, biashara ikafa kwa kulipa mikodi na nadaiwa mpaka sahivi mapato mengine, nimefunga biashara, sijui kwanini TRA wasiwe USER FRIEND na walipa kodi, sahivi nataka kufungua biashara ingine mkoa mwingine naambiwa maliza kwanza deni la awali na uombe maombi ya kuhamisha TIN
Kiongozi ukifungua biashara alafu ikafa unaandika barua kuwajulisha kuwa biashara yako umeifunga hivyo wasiendelee kukudai tena kodi, lakini biashara ikifa alafu ukakaa kimya wao wanaendela kuhesabu tu kodi yao.
 
Hapo mnataka kuniambia kuna mturuki ataleta pua yake tena hapa TZ?
They will come when meko is gone
Na wasiporudi hao Waturuki itakuwaje?

READ! Taarifa inasema Waturuki wamekosa mkopo wa benki za ndani

Maana yake hawakuja na mtaji!

Ndio haya Marehemu Mengi alikuwa anayasema wakati ana bifu na Wahindi, walikuwa wanamwambia tumekuja na briefcase la makaratasi ya business plan za kutajirikia hapa hapa kwenu! Yani sisi ni vichwa panzi.

Magufuli fukuza hao Waturuki!

Thank God Almighty tumepata kichaa mzalendo Ikulu hapapatikii wazungu, hafagilii wageni!

ALHAMDULLILAH ALA KULLI HAAAL
HADHA MIN FADLI RABBI
 
Na TIN pia ni ya kuombea uhamisho kwanini sasa, wakati mtu ukiwa na TIN unaonekana kwenye system
Kwa sababu ukusanyaji wa mapato unafanyika kikanda, kama ulichukulia TIN yako Dar na biashara yako ipo dar na unataka kuhamishia biashara yako tuseme Mbeya inabidi utoe taarifa ili waihamishie TIN yako huko na utalipa kodi huko ulikohamishia biashara yako
 
Unalipaje kodi haujaanza biashara? Hua nasema TRA watakuja kutuua na kiharusi kodi idaiwe kwenye faida hapo sawa unadai vipi kodi kwenye mtaji?
Unaweza au tuseme inawezekana ukalipa kodi kabla ya kufanya biashara kwa kukadiria/ kukisia kuwa faida itafikia kiasi gani mwisho wa mwaka, halafu mwisho wa mwaka mkishafanya mahesabu, ama unalipa palipopungua au wao wanarudisha zilizozidi.
 
Uchumi wa kati wazidi KUPAA.
Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha.
 
Pamoja na mapungufu ya TRA Ila wachangiaji wengi hapa wanakimbilia kuleta Siasa. Wewe kama mtanzania unaweza kwenda uturuki au nchi yoyote hata Kenya bila mtaji wa kutosha ukitegemea benki zao zikukopeshe na ukaachwa tu!?

Hao sio wawekezaji ni wababaishaji tu Ila Kama ilivyo kawaida wale wanaoipinga serikali ya awamu hii tayari wataleta story za CCM na CDM. Naona kuna mpumbavu ameshaanza kutamka Lissu, sijui anaingiaje.
 
178909098.jpg
 
Back
Top Bottom