TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

Pamoja na mapungufu ya TRA Ila wachangiaji wengi hapa wanakimbilia kuleta Siasa. Wewe kama mtanzania unaweza kwenda uturuki au nchi yoyote hata Kenya bila mtaji wa kutosha ukitegemea benki zao zikukopeshe na ukaachwa tu!??, Hao sio wawekezaji ni wababaishaji tu Ila Kama ilivyo kawaida wale wanaoipinga serikali ya awamu hii tayari wataleta story za CCM na CDM. Naona kuna mpumbavu ameshaanza kutamka Lissu, sijui anaingiaje.
Unajua maana ya biashara?
 
Lazima ulipe makadirio ndo upewe Tax Clearance

Hiki kitu nakifahamu lakini ni unyanyasaji tunafanyiwa wewe haujaanza biashara ukajua faida yake halafu ukadiriwe kodi means wanakadiria kodi kwenye mtaji wakati uhalisia wanatakiwa kukadiria kodi kwenye Faida, unapokadiria kodi kwenye mtaji unaandaa mazingira ya kuua mtaji.
 
Pamoja na mapungufu ya TRA Ila wachangiaji wengi hapa wanakimbilia kuleta Siasa. Wewe kama mtanzania unaweza kwenda uturuki au nchi yoyote hata Kenya bila mtaji wa kutosha ukitegemea benki zao zikukopeshe na ukaachwa tu!??, Hao sio wawekezaji ni wababaishaji tu Ila Kama ilivyo kawaida wale wanaoipinga serikali ya awamu hii tayari wataleta story za CCM na CDM. Naona kuna mpumbavu ameshaanza kutamka Lissu, sijui anaingiaje.

Umesikiliza vizuri upande wa hao Waturuki?
 
Eee Mungu tunajua unayaona haya na unajua tunaloelekea, tunasubiri uamuzi wako.
 
Mwambe soma uzi huu kama Waziri wa Viwanda uingilie kati ingawa naamini siku hizi hata afisa mdogo tu humkomalia mkubwa
 
Kuna wimbo wa Vijana jazi

Ogopa tapeli
Unapo ona tajiri anawapunguza wafanyakazi kwa visa
Anaanza kuwaa

Ambia waliobaki nitawapunguzia mishahara
Ujuwe hata Wazabuni alio wapa miradi mikubwa atakuja kuwageuka either katika mikataba au kutafuta njia ya kutanchi malizao pawepo na mizozo ndio unakuwa mwisho wa utajiri wake Ndiyo maana
 
Kwa sababu ukusanyaji wa mapato unafanyika kikanda, kama ulichukulia TIN yako Dar na biashara yako ipo dar na unataka kuhamishia biashara yako tuseme Mbeya inabidi utoe taarifa ili waihamishie TIN yako huko na utalipa kodi huko ulikohamishia biashara yako
Huu nao ni upumbavu, unakusanya vipi mapato kikanda, halafu pesa hizohizo unazipeleka hazina zote!
 
Na wasiporudi hao Waturuki itakuwaje?....
Ona huyu.... chuki na husda ni mbaya kwa afya yako. Kama nyie ni wajanja si mngefungua aina hyo ya kiwanda. Umewaza hicho kiwanda kingefunguliwa hata kama ni vijana 10 si wangeajiriwa.

kodi si ingelipwa kwa maendeleo ya nyie wa TZ... haya wameshindwa kufungua je pesa n ajira vimehamia kwako? MATAGA sijui mnakula maharage ya wapi nyie. mfyuuuu
 
Hiki kitu nakifahamu lakini ni unyanyasaji tunafanyiwa wewe haujaanza biashara ukajua faida yake halafu ukadiriwe kodi means wanakadiria kodi kwenye mtaji wakati uhalisia wanatakiwa kukadiria kodi kwenye Faida, unapokadiria kodi kwenye mtaji unaandaa mazingira ya kuua mtaji.
MATAGA hawawezi kukuelewa.... ukienda kukadiriwa kodi hata mwezi wa 11 kwa mara ya kwanza unaambiwa ulipe kodi ya robo zote nne...yamenikuta haya
 
MATAGA hawawezi kukuelewa.... ukienda kukadiriwa kodi hata mwezi wa 11 kwa mara ya kwanza unaambiwa ulipe kodi ya robo zote nne...yamenikuta haya

Si bado upo ndan ya quarter? Sheria ndo inakutaka hivo. Kuepuka hayo nenda mwakani 1/1/2021
 
Nilifungua biashara nikapewa makadirio kama kawaida nikalipa awamu ya kwanza, biashara haikufanya vizuri kutokana na eneo awamu ya pili wakaendelea kunidai, biashara ikafa kwa kulipa mikodi na nadaiwa mpaka sahivi mapato mengine, nimefunga biashara, sijui kwanini TRA wasiwe USER FRIEND na walipa kodi, sahivi nataka kufungua biashara ingine mkoa mwingine naambiwa maliza kwanza deni la awali na uombe maombi ya kuhamisha TIN
Kabla hujafanya biashara ya halali, ufanye utafiti kwanza! Usishindwe wewe, ukaanza kulaumu TRA. Umesema biashara haikufanya vizuri kwa sababu ya eneo! Je! Na hilo ni kosa la TRA?
 
Jioni ya leo, TRA imevamia na kufunga ofisi moja ambayo ilikuwa bado haijaanza kufanya kazi wakidai kodi. Hii ni kampuni ya waturuki inayohusika na kutengeneza tiles za majengo. Mashine zililetwa lakini kwa bahati mbaya jamaa walishindwa kuanza kufanya kazi kutokana na mtaji kutokutosha.

Waturuki walitegemea kupata mkopo kwenye moja ya mabenki ya ndani, kitu ambacho kimechelewa. Mategemeo yao ilikuwa ni kupata mkopo mwezi wa 4 lakini hadi December mkopo ulikuwa bado haujapitishwa. Kwa maana hiyo hawakuwa na jinsi ya kuanza operations zao.

Hii kampuni hipo maeneo ya Mbezi Afrikana, na kwa bahati mbaya, magari ya TRA wamevamia jioni hii na kufunga ile ofisi na kumchukua mtu anayesimamia ile mali maana wengine inaonekana wako nje ya nchi. Na kwa sababu hakuna kazi, ni mmoja wao amebakia pale kulinda mali.
Mwingereza na habari ya Mturiki.
TRA hawanaga shida wakiwauliza maswali muwajibu tu na wakiwaomba docs na mahisabati ya biashara yenu wapatieni ila wakiwaomba rushwa muwaitie TAKUKURU.
 
Back
Top Bottom