TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

TRA yafungulia akaunti zote za Wafanyabiashara zilizokuwa zimefungwa kutokana na madeni ya kodi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi

Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.

Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.

Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.

"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo

"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo

Chanzo: NIPASHE
 
Ni vizuri maana wengine mkishika hapo ina maana kila kitu kinasimama ajira za watu hata kile kidogo cha kodi nacho kinapotea kabisa maana kama umefreeze acc...biashara itaendeleaje kwa kulipa kidogo kidogo wanaepusha mengi....hongera TRA
 
Wanufaika bado amajaamini tu mungu wenu hayupo

Truth be told, mazoea mabaya ya muda mrefu yamewafanya wafanyabiashara wengi wawe na kasumba ya kutoridhia kutii sheria bila shurti --- lugha ya kutoa kodi kwa hiari hawaielewi kamwe.

Wamejifunza njia ya mikato, ujanjaujanja, wiziwizi, rushwarushwa, dilidili and the like. Sasa wakiletwa kwenye mstari, by definition, wao wanadhani wanaonewa. What!???
 
utawala wa Awamu ya Tano ulikuwa utawala wa kibabe sana. Ahsante sana Rais wa awamu ya sita Mama Samiah Suluhu Hassan.
 
Back
Top Bottom