TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

Watumishi wanatunyonya Sana, yaani karibia nusu ya pato kwa mwezi wanachukua wao, na bado wanadai nyongeza,

Sioni kama Taifa namna tunaweza fanya maendeleo kama kipato almost chote tunalipana mishahara tu.
Lakini inasaidia pesa kurudi kwenye mzunguko

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Lakini inasaidia pesa kurudi kwenye mzunguko

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Haileti maana kuwa fedha yote iishie kwenye mishahara tu,

Litakua taifa la ajabu Sana lisilo na vision yeyote,

Ni sawa na kuwa na familia ambayo kipato chake chote ni kwaajili ya chakula tu.
 
bil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
Mkuu unataka warudi kuwa jobless
 
WIZI NA UPORAJI MTUPU dhidi ya maskini wa Kitanzania na makampuni ya wawekezaji.
Leo 01/01/2021 mamlaka ya mapato Tanzania kupitia kwa waandishi wa habari, imetangaza makusanyo ya mwezi Disemba 2020 kuwa ni takribani trilioni 2, hii ni rekodi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hii mwaka 1996


Hi ni hatua ya kupongezwa sana kwa watanzania wote walipa kodi na mamlaka ya mapato nchini, kukusanya trilioni 2 kwa mwezi( Disemba) ni jambo lenye kutia moyo sana kwa sisi wananchi

Nilikuwa napitia mapitio ya uchumi ya kila mwezi( Monday Economic Review) kutoka benki kuu yetu( BOT) kwa mwezi Disemba 2020

Ripoti hiyo ya Disemba, inaonyesha kwa mwezi October pekee, 2020, serikali ilikusanya takribani trilioni 1.682, hii ni jumla ya makusanyo yote ya kikodi( Tax Revenue) na yasio ya kikodi ( Non Tax Revenue)

Ambapo kwa mwezi huo wa October 2020, makusanyo ya kikodi( Tax Revenue) pekee yalikuwa ni trilioni 1.295 , na makusanyo yasio ya kikodi( non tax revenue) yalikuwa ni bilioni 282.2 na makusanyo kutoka local government ( own source ) yalikuwa ni bilioni 51.2

Lakini tukienda kwenye matumizi ( Government Expenditure) kwa mwezi October 2020, ripoti hiyo( Monthly Economic Review) inaonyesha kuwa serikali ilitumia takribani trilioni 1.854

Ambapo matumizi hayo yalikuwa ni kama ifuatavyo, kwenye matumizi ya kawaida ( Recurrent Expenditure) ilikuwa ni trilioni 1.282 na matumizi kwenye miradi ya maendeleo ( Development Expenditure) ilikuwa ni bilioni 571

Ambapo matumizi makubwa zaidi kwenye serikali yanakwenda kwenye mishahara( wages bills) za watumishi wa umma, kwa mwezi October serikali ilitumia takribani bilioni 601.7 kulipa mishahara kwa mwezi mmoja tu

Na pesa nyingine inatumika ku service madeni yetu( Debt expenses), ambapo kwa mwezi October pekee, serikali ilitumia takribani bilioni 192.4 kulipia interest ya madeni yetu ya nyuma na sasa

Kwa maana hiyo kwa mwezi October 2020, serikali ilitumua fedha nyingi zaidi( trilioni 1.854) kuliko pesa tulizoingiza(trilioni 1.628) kwa mwezi( budget deficit)

Kwa hatua ya leo ya mamlaka ya mapato kukusanya trilioni 2, kama itaendelea hivi hivi kila mwezi, maana yake ni kwamba serikali tunakwenda kuwa tunaingiza/ kukusanya fedha nyingi zaidi kuliko matumizi yetu kwa mwezi

Hii itasaidia sana kwa nchi yetu kupunguza mzigo wa kuendelea kukopa mikopo ya bei nafuu( concession loan) kutoka kwenye multilateral lending institutions au mikopo ya kibiashara( non concession loan) kutoka kwenye mabenki ya kibiashara duniani

Kongole kubwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania 👏👏👏

Ngamanya Kitangalala Mwaswala [email protected]
0756 669494
 
Ipo haja ya serikali ama kupunguza mishahara ama kupunguza wafanyakazi pesa zinazotumika kulipia mishahara tu ni nyingi Sana.
 
bil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
Kumbe inaweza kupungua fedha ya mishahara?
 
Hoja yako hapa ni ipi??
Hoja ni kwamba kama ulikwepa umande hilo siyo tatizo la walioajiriwa, hao watumishi kudai mishahara bora ni haki yao, hata na wenyewe wanakatwa kodi kwenye mishahara yao na pia wakifanya manunuzi hukatwa VAT. Kwa hiyo wao wanakamuliwa kodi mara mbili na mishahara yao hairidhishi, sema jingine..
 
Zamani local government na taasisi nyingine za serikal zilikuwa zikikusanya na kutumia fedha zake kulingana na mahitaji ya eneo/mamlaka husika na hivyo kuboresha huduma na miradi kwa wakati.

Siku hizi TRA inazikusanya na inazitangaza kama sehemu ya mapato yao.Alafu Kuna urasimu kuzirudisha toka hazina kwenda kwa wamiliki na hivyo kusababisha huduma,malipo,madeni,miradi n.k kukwama. Alafu TRA inajisifia!
Nimekusoma mkuu..!!
 
Hoja ni kwamba kama ulikwepa umande hilo siyo tatizo la walioajiriwa, hao watumishi kudai mishahara bora ni haki yao, hata na wenyewe wanakatwa kodi kwenye mishahara yao na pia wakifanya manunuzi hukatwa VAT. Kwa hiyo wao wanakamuliwa kodi mara mbili na mishahara yao hairidhishi, sema jingine..
Ni kweli mkuu nimeishia la saba ila hiyo haimfanyi mtumishi kuwa bora zaidi kuliko Mimi mfanyabishara ambaye nakimbizana na TRA na halafu mwisho wa siku akaneemeke tu mtu ambaye sioni umuhimu wake kwani huduma anayoitoa ni mbovu kupita maelezo na bado anafanya ufisadi wa fedha za uma ukiachilia mbali kunidai rushwa kwa huduma ambayo anapaswa kunipa na nimeshailipia kupitia mshahara wake.
 
Sasa kama hujaenda shule, hilo linamhusu nini mtu anayedai haki yake?

Wafanyakazi wao hawana pa kukwepea kodi afadhali wewe hadi unafukuzana na TRA.
 
Hakuna muujiza wowote ule. Kilichofanyika sasaivi ni hela zote za serikali zinakusanywa na TRA.

Kama hadi mamlaka za Ngorongoro na Tanapa na uhamiaji zimenyang’anywa kukusanya mapato ya utalii na imepelekewa TRA hizo figures wala hazishangazi.

Tena utalii ukirudi kwenye hali yake tutakuja kutangaziwa imefikia hata trillion 4 na washamba wakashangaa kumbe hizo hela zilikuwepo tangu zamani.
 
Back
Top Bottom