Lakini inasaidia pesa kurudi kwenye mzungukoWatumishi wanatunyonya Sana, yaani karibia nusu ya pato kwa mwezi wanachukua wao, na bado wanadai nyongeza,
Sioni kama Taifa namna tunaweza fanya maendeleo kama kipato almost chote tunalipana mishahara tu.
Hoja yako hapa ni ipi??Wengine akina nani? au unafikiri kila kilaza anaweza kuajiriwa kufanya kazi serikalini...
Haileti maana kuwa fedha yote iishie kwenye mishahara tu,
Mkuu unataka warudi kuwa joblessbil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
Leo 01/01/2021 mamlaka ya mapato Tanzania kupitia kwa waandishi wa habari, imetangaza makusanyo ya mwezi Disemba 2020 kuwa ni takribani trilioni 2, hii ni rekodi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hii mwaka 1996
Hi ni hatua ya kupongezwa sana kwa watanzania wote walipa kodi na mamlaka ya mapato nchini, kukusanya trilioni 2 kwa mwezi( Disemba) ni jambo lenye kutia moyo sana kwa sisi wananchi
Nilikuwa napitia mapitio ya uchumi ya kila mwezi( Monday Economic Review) kutoka benki kuu yetu( BOT) kwa mwezi Disemba 2020
Ripoti hiyo ya Disemba, inaonyesha kwa mwezi October pekee, 2020, serikali ilikusanya takribani trilioni 1.682, hii ni jumla ya makusanyo yote ya kikodi( Tax Revenue) na yasio ya kikodi ( Non Tax Revenue)
Ambapo kwa mwezi huo wa October 2020, makusanyo ya kikodi( Tax Revenue) pekee yalikuwa ni trilioni 1.295 , na makusanyo yasio ya kikodi( non tax revenue) yalikuwa ni bilioni 282.2 na makusanyo kutoka local government ( own source ) yalikuwa ni bilioni 51.2
Lakini tukienda kwenye matumizi ( Government Expenditure) kwa mwezi October 2020, ripoti hiyo( Monthly Economic Review) inaonyesha kuwa serikali ilitumia takribani trilioni 1.854
Ambapo matumizi hayo yalikuwa ni kama ifuatavyo, kwenye matumizi ya kawaida ( Recurrent Expenditure) ilikuwa ni trilioni 1.282 na matumizi kwenye miradi ya maendeleo ( Development Expenditure) ilikuwa ni bilioni 571
Ambapo matumizi makubwa zaidi kwenye serikali yanakwenda kwenye mishahara( wages bills) za watumishi wa umma, kwa mwezi October serikali ilitumia takribani bilioni 601.7 kulipa mishahara kwa mwezi mmoja tu
Na pesa nyingine inatumika ku service madeni yetu( Debt expenses), ambapo kwa mwezi October pekee, serikali ilitumia takribani bilioni 192.4 kulipia interest ya madeni yetu ya nyuma na sasa
Kwa maana hiyo kwa mwezi October 2020, serikali ilitumua fedha nyingi zaidi( trilioni 1.854) kuliko pesa tulizoingiza(trilioni 1.628) kwa mwezi( budget deficit)
Kwa hatua ya leo ya mamlaka ya mapato kukusanya trilioni 2, kama itaendelea hivi hivi kila mwezi, maana yake ni kwamba serikali tunakwenda kuwa tunaingiza/ kukusanya fedha nyingi zaidi kuliko matumizi yetu kwa mwezi
Hii itasaidia sana kwa nchi yetu kupunguza mzigo wa kuendelea kukopa mikopo ya bei nafuu( concession loan) kutoka kwenye multilateral lending institutions au mikopo ya kibiashara( non concession loan) kutoka kwenye mabenki ya kibiashara duniani
Kongole kubwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania 👏👏👏
Ngamanya Kitangalala Mwaswala kngamanya@yahoo.com
0756 669494
Kumbe inaweza kupungua fedha ya mishahara?bil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
Hoja ni kwamba kama ulikwepa umande hilo siyo tatizo la walioajiriwa, hao watumishi kudai mishahara bora ni haki yao, hata na wenyewe wanakatwa kodi kwenye mishahara yao na pia wakifanya manunuzi hukatwa VAT. Kwa hiyo wao wanakamuliwa kodi mara mbili na mishahara yao hairidhishi, sema jingine..Hoja yako hapa ni ipi??
Nimekusoma mkuu..!!Zamani local government na taasisi nyingine za serikal zilikuwa zikikusanya na kutumia fedha zake kulingana na mahitaji ya eneo/mamlaka husika na hivyo kuboresha huduma na miradi kwa wakati.
Siku hizi TRA inazikusanya na inazitangaza kama sehemu ya mapato yao.Alafu Kuna urasimu kuzirudisha toka hazina kwenda kwa wamiliki na hivyo kusababisha huduma,malipo,madeni,miradi n.k kukwama. Alafu TRA inajisifia!
We want to feel this imaginary statistics on our empty stomachs.
Too much blah blah!
Ubunifu sasa ni kutuibia hata mabando tunazojiunga ilmradi makusanyo zaidi.Kumbe inaweza kupungua fedha ya mishahara?
Ni kweli mkuu nimeishia la saba ila hiyo haimfanyi mtumishi kuwa bora zaidi kuliko Mimi mfanyabishara ambaye nakimbizana na TRA na halafu mwisho wa siku akaneemeke tu mtu ambaye sioni umuhimu wake kwani huduma anayoitoa ni mbovu kupita maelezo na bado anafanya ufisadi wa fedha za uma ukiachilia mbali kunidai rushwa kwa huduma ambayo anapaswa kunipa na nimeshailipia kupitia mshahara wake.Hoja ni kwamba kama ulikwepa umande hilo siyo tatizo la walioajiriwa, hao watumishi kudai mishahara bora ni haki yao, hata na wenyewe wanakatwa kodi kwenye mishahara yao na pia wakifanya manunuzi hukatwa VAT. Kwa hiyo wao wanakamuliwa kodi mara mbili na mishahara yao hairidhishi, sema jingine..
Well said [emoji106], I second youbil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu...