Huo ni usanii tu, hakuna kipya cha maana. Ngoja nikupe shule kidogo hapa.
1. Thamani ya shilingi yetu imeshuka sana, hivyo tarakimu kubwa za mapato kwa kutumia shilingi yetu haziakisi uhalisia.
2. Mfumuko wa bei ni mkubwa sana na hilo litaakisi pia kwenye makusanyo ya kodi kuwa na tarakimu kubwa, lakini ukija kwenye uhalisia hayo mapato sio chochote kwenye kutumika kulipia huduma au manunuzi ya bidhaa.
3. Mfumo wa ukusanyaji mapato kwa TRA umejikita kumnyonya mlaji wa mwisho, na kitakwimu idadi ya watanzania inaongezeka kwa zaidi ya watu milioni moja kwa mwaka, hivyo automatically mapato ya TRA yataongezeka kufuata hilo.