TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

TRA yazindua kodi ya kitanda kutoka kwa Watalii

Mimi sina tatizo na tozo ya kitanda ni ndogo sana tatizo gazeti la serikali lina orodha pungufu ya mahoteli na nyumba za kulala wageni nyingi zimeachwa kuorodheshwa kwenye gazeti hilo ili zilipe kodi. Baadhi zimerudiwa kuorodhshwa kimakosa mara mbili nyingine zimebadili umilki hivyo hazitalipa kwa mujibu wa notisi hiyo. Wapitie vizuri kuondoa lasoro hizo ili waziri apitishearekebisho hayo.
 
Hivi mnavyozitetea hizo hotel mnajua gharama zake zikoje, bei ya kitu unayopata mtaani kule bei yake ni maradufu wacha watozwe hiyo kodi
 
Bed Night Levy ni kodi iliyokuwepo tangu zamani. Sema tu ni kwamba kodi hii haikuwa maarufu sana kwa sababu inakusanywa zaidi kwenye mahoteli ya kati na makubwa
 
kusoma si kumaliza ujinga
salamu ziwafikie tato; Guide's, popote pale walipo
 
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwin Mhede amepokea orodha ya huduma za malazi iliyoboreshwa 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki ili kuiwezesha TRA kukusanya tozo ya Kitanda Siku kutoka kwa Watalii wanaotumia huduma za malazi.

View attachment 1641829

Hii ni katika harakati za kuongeza mapato
Kodi ya kitanda?!kwanini hiyo tozo isiwekwe kwenye tozo zilizopo tayari?
Yaani mijitu Tena yenye "PHD"inakaa ofisini,inaleta huu upuuzi wa kuongeza tozo kwenye utarii Ili kuongeza mapato?harafu inaona imefanya Jambo la maana,na la kitaharamu sana!inacheka cheka tu.
Mtaongeza Kodi kila eneo,Wala haitasaidia,maana hizo biashara zitakufa,sehemu pekee ambayo inabidi iangaliwe ni hizi nyumba za kupanga,hapa mjini,watu wamepanga,wenye nyumba wanapokea Kodi,na hawalipi Kodi ya mapato,
 
Tunasubiri na kodi za CHUPI....... Mijitahira kabisa. Unadhani ukimbana mtalii na kodi kubwa atakuja na hii hali ya uchumi?
 
Watalii wenyewe wangapi? Tena kipindi hiki cha korona! Hii ndio shada ya kuvisoma na kuvitekeleza vitabu vya Nyerere.

Tutaelewana tu! Mi- 5 tena!
 
Back
Top Bottom