Ukweli mchungu ni kwamba
traditional media (TV, Radio, Magazeti) zipo kwenye kipindi cha mpito. Watu wengi wanahamia kwenye digital & on-demand content kwa sababu wanataka
control (wao ndio wadhibiti nini waone au wasione), freedom (uhuru kupata habari yoyote) na diversity (habari za maudhui mbalimbali).
Ngoja nikusanue kwa nini hizi media za kizamani zinaweza kufa (au kupoteza nguvu kubwa) miaka ijayo:
Sababu za Kuanguka kwa Traditional Media
- Udhibiti (control) wa Kisiasa & Serikali
- Watu wanachoka na maudhui ya upande mmoja (biased), mfano sera na Kampeni za CCM tu kwenye kila TV au kila Chaneli utakayoiweka.
- Watu wanahisi hawapati ukweli, bali propaganda zinazodhibitiwa na mamlaka au kundi la watu fulani (Doto Magari anawaita Watufudenge).
- Watazamaji/wasikilizaji wanakimbilia YouTube, Instagram, JamiiForums, Facebook, TikTok, Podcast mbalimbali, Twitter/X kupata alternative voices or news (kupata maudhui tofauti).
- On-Demand Generation
- Kizazi cha sasa hasa hawa Millennials & Gen Z hawataki kungoja "habari saa mbili usiku" au zile Miziki za Radio fulani inayopigwa mchana tu, mfano unakuta nyimbo imetoka usiku wewe inabidi ungoje Clouds Top 20 kesho mchana ndio usikilize.
- Wao wanataka instant updates (habari za papo hapo) kupitia simu.
- Youtube, Instagram, Netflix, Twitter, JamiiForum, Facebook, Spotify, na TikTok zinatoa content anytime, anywhere (muda wowote, mahali popote mchawi bundle tu), tofauti na TV au Radio ambazo ukiama Nchi au Eneo fulani uwezi kupata mawimbi yake hivyo uwezi kusikiliza au kutizama, mfano redio nyingi ukiama maeneo au mikoa hazisikiki tena kutokana na kukosa masafa ya umbali huo.
- Cost vs Accessibility (Gharama & Upatikanaji)
- Kuendesha TV & radio station ni ghali sana (leseni, mitambo, wafanyakazi).
- Digital media mtu mmoja na kamera yake au simu yake anaweza kufikia watu mamilioni.
- Wateja (audience) wanaona haina maana kutumia pesa nyingi kupata kitu ambacho wako nacho bure online, mfano kulipia kingamuzi au Cable TV kisa utazame taarifa ya habari ya saa mbili usiku.
- Monotony & Irrelevance
- Vipindi vya redio/TV vinarudia maudhui yale yale (muziki uleule, siasa zilezile), unakuta kama ni majira ya uchaguzi kila TV inamuinesha mgombea huyo huyo akinadi sera hizo hizo, Camera zote za TV tofauti tofauti zipo kwa kwa mgombea Urais kupitia chama cha CCM tu, vyama vingine chenga, au wasanii wanafanya interview wanaulizwa maswali yale yale ya kujirudia rudi kwenye kila media.
- Watu wanataka niche content, yani content wanazozitaka kwa muda huo tu (mfano podcast za afya, channels za kilimo, tech reviews, business mentorship).
- Traditional media mara nyingi haiwezi personalize content kwa kila mtu. TV station kubwa zenyewe zinarusha “programu za jumla tu” – muziki, siasa, michezo, habari za matukio), kumbe wakati huo wewe unataka habari za mapishi tu namna ya kukata kachumbari.
- Social Media Power
- Breaking news (Habari za punde) sasa zinavunjwa vunjwa kwanza na Instagram, Youtube, Twitter, Telegram au TikTok kabla ya kurushwa kwenye TV au Radio.
- By the time TV inatangaza, tayari watu wameshaona online.
- Mamlaka ya kusimulia story imehama kutoka TV kwenda citizen journalists (Watengeneza maudhui wa mitandaoni tu) & influencers.
- Advertising Shift
- Makampuni makubwa sasa yanawekeza zaidi matangazo yao kwenye digital ads (Google, Facebook, TikTok Ads).
- Kwa sababu wanapata analytics (takwimu za matangazo), target audience (watu wanaolengwa kupata matangazo), na matokeo ya moja kwa moja.
- TV na Radio zikipoteza ads → zinakosa nguvu ya kifedha ya kuendesha vipindi→ mwisho wa siku zina-collapse.
- Censorship vs Free Speech
- Traditional media mara nyingi hazina uhuru wa kuzungumza mambo "sensitive" (mfano scandals, ukosoaji wa viongozi), hakuna TV au Radio yoyote Tanzania inayoweza kuikosoa serikali au hata chama kilichoko madarakani.
- Lakini online platforms zina watu jasiri, independent creators (watengeneza maudhui huru au binafsi kama kina Mange Kimambi, kina Balozi Humphrey Polepole na wengineo).
- Watu wanakimbilia huko kwa sababu wanahisi wanapata raw truth (ukweli halisi).
- Generation Gap
- Vijana wengi wa miaka hii hawana tabia ya kununua gazeti au kukaa mbele ya TV masaa 2.
- Wana-scroll Instagram, TikTok, YouTube Shorts, au kusikiliza podcast huku wakifanya kazi, au wakiama eneo moja kwenda jingine, tofauti na TV ambayo itataka ukae hapohapo tu.
- Hii inauwa kabisa audience pipeline ya traditional media.
📉 Kwa ufupi:
Traditional media itapotea nguvu
kwa sababu audience wanataka uhuru, uhalisia na control ya content wanazozitaka wao. Digital media ina flexibility (unyumbulikaji), personalization (vitu binafsi upendavyo) na low cost (Gharama ndogo) – ambazo TV/Radio hazina.