Jana weekend mida ya jioni nikatoka ku cruise kidogo 😎. Sikuwa na wazo la kuvaa mkanda nikajisemea, leo matrafiki nao wamepumzika
Kioo wazi, upepo unaingia, starehe kabisa 😂.
Ghafla… huyo hapo! Akaniona tu kabla sijajua nini kinaendelea. Akaniuliza leseni nikampa kwa heshima zote. Akaenda ku check plate number kama nina deni… bahati nzuri niko safi.
Akarudi na kile kimashine chake, tayari anataka kunipiga faini ya 30,000 sijavaa mkanda.
mfukoni sina hata elfu 5, zimejaa nyekundu tu 😂.
Ikabidi nifanye nitoe japo roho iliuma nikijua kabisa njia hii hainaga chenji na kikienda hakiudi.
Nikamuacha mwenzangu niliyemkuta pale bado yuko kwenye kikao cha mazungumzo. Sijui alikuwa anaomba msamaha, sijui kama alitoboa kwa kubembeleza au alijiongeza kuzama mfukoni.