Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

Mimi nakula pesa zangu,mimi sio nzi wa kijani kama wewe.
Subiria teuzi utapewa hata viti maalum uwt
 

Ya namba mbona madogo, kwani hata yanakuzwa?
Ngoma meno na mandongo, watapolima mazwazwa!
Kwani wala ni uongo, tuko kama tumeuzwa,
Ndiyo ukweli mchungu, wapora haki si watu.

Vipi tuafikiane, na wezi na wauaji,
Hata tubaki wanne, si mwenzetu mporaji,
Hata ipite karne, ipo siku tutahoji,
Senzighe utuelewe, tuna machungu moyoni.

Sefu ameweka wazi, ICC yawahusu,
Kule kunachapwa kazi, yasubirini ya Lissu,
Mlidhani sisi mbuzi, tutatishika kwa visu?
Hii ngoma bado mbichi, kwa sisi Sefu na Lissu!
 
Usitutishe lolote,hiyo court kangaruu
Hakuna kwenda popote,Lissu ni mwoga kunguru
Mtaimba nyimbo zote,mwishowe mtakufuru
Brazajei subiri,mitano ipite kwanza
 
Usitutishe lolote,hiyo court kangaruu
Hakuna kwenda popote,Lissu ni mwoga kunguru
Mtaimba nyimbo zote,mwishowe mtakufuru
Brazajei subiri,mitano ipite kwanza

Kutisha si hulka yangu, wala ya wapambanaji,
Watishaji wa marungu, si nyie wakamataji?
Tumeyaonja machungu, kote hadi kwenye paji,
Pelekeni taarifa, tuko imara kinoma!

Kangaruu ya dunia, siyo hizi Tanzania?
ICC waijua, au unaisikia?
Achana na vya dunia, hali yako pambania,
Wazitaka kangaruu, hizo zimejaa kwetu!
 
Leo nimekamatwa na traffic eti gar yangu Ina den imepigwa fain tar 31 wakat mwezi wa 11 wakat gar yangu ipo ndan sijaitumia now wiki Tatu natumia gar ya mke wangu
 
Mimi nimefanyiwa hivyo makosa matatu na penati laki na themanini uzuri trafiki alipiga faini kimakosa namuandama kila siku ayalipe yeye ameshalipa mawili bado moja
 
Nilishawah kukamatwa na zile mashine zao za kudai maden kimara pale jamaa wakanipa deni la 60000 na leseni sio yangu ila gar yangu na sijawah kumpa mtu gar jamaa walidandia pale mpka nikalipa ndo nikatoka yan upumbavu mtupu
 
Mnatishwa na vibwengo,vinakaa uholanzi
Zimepanda zao shingo,kazi yao makamuzi
Wamepanuka maungo,kusikiza upuuzi
Waende na Marekani,kukamata wauaji.
 
Umesema sahihi kabisa.

Polisi wa sasa wanakusanya fedha kwa njia halali na haramu.
 
Sasa we presha ya nini?

Namba ya leseni sio yako, basi tulia!

Presha inakuwapo kwani gari huwezi kutembeza wakisema inadaiwa.

Wanapenda kufunganisha leseni na magari kwani hayo kwao ni rahisi kupiga pesa kuliko leseni.

Kwao leseni hazina maslahi bali namba za magari.
 
Mnatishwa na vibwengo,vinakaa uholanzi
Zimepanda zao shingo,kazi yao makamuzi
Wamepanuka maungo,kusikiza upuuzi
Waende na Marekani,kukamata wauaji.

Wakoloni tumeona, weupe hata weusi,
Ubaya wanafanana, baba lao ni jeusi!
Bila Hague kuyabana, tungepumua je sisi?
Udumu sana beberu, mbona yangetumaliza!
 
Wakoloni tumeona, weupe hata weusi,
Ubaya wanafanana, baba lao ni jeusi!
Bila Hague kuyabana, tungepumua je sisi?
Udumu sana beberu, mbona yangetumaliza!
Hao ni watu laghai,wasumbufu Afrika
Wakisha kuvaa tai,hujiona malaika
Husingizia jinai,kuwalinda vibaraka
Na wakome wakomeke,kuifuata Tanzania.
 
Jamaa angu juzi kati kaandikiwa faini mara 4 sehemu tofauti mkoani na gari ipo ndani hapa Dar miezi mitatu haijatoka.

Alivyowafata wakamfutia wakasema walikosea
Me waligoma ikabidi nilipe nikawa mbia nileteyeni huyo dereva wakasema sio kazi yao tunapitia magumu sana 😭
 
Sasa we presha ya nini?

Namba ya leseni sio yako, basi tulia!
Atulie!!!?
wata mlipisha me nilienda adi kituoni nikawa mbia wanileteye mwenye leseni me simjui wakasema sio kazi yao tupo nchi ya kusadikika 😭
 
Hao ni watu laghai,wasumbufu Afrika
Wakisha kuvaa tai,hujiona malaika
Husingizia jinai,kuwalinda vibaraka
Na wakome wakomeke,kuifuata Tanzania.

Wakadumu Mabeberu, watupao kupumua,
Hamnaga kushukuru, hamtoki mtaua?
Bila yao Mabeberu, kwani mngejitambua?
Mnajiita majiwe, beberu saizi yenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…