Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

sasa unalipaje faini kama hiyo

Labda uwe na muda mwingi wa kupoteza. Kwenye mitano mingine mabazazi wana mamlaka ya kushikilia gari lako wakakupa halina matairi mwisho wa shauri.
 
Tena wazidishe kubambika
Unafikiri wao wataishije
Ongezeni dozi matrafik

Ova
 
Sasa we presha ya nini?

Namba ya leseni sio yako, basi tulia!
Mimi hua nikicheki kwny web yao nakuta gari imeandikiwa fine wkt gari iko ndani tu hata haijatoka lkn baada ya siku kadhaa nikichek nakuta tena sina deni,sijui hua kinatokea kitu gani hapo.
 
Habari hizi zimfikie gwiji wa chama tawala, almaarufu "Senzighe wa Senzighe ."

Lissu kuweza mwelewa, namba tuisome haswa!
Kwamba si bazazi hawa, wangapi wamewauwa?
Muda wote wamelewa, dereva awapa vichwa,
Yeye dereva wa Lori, asikilize la nani?

Hapa chini yalikuwa ya mleta mada kabla ya kibao kugeuka:

View attachment 1645164
Hahah kumbukumbu kutoka maktaba.
 
sasa unalipaje faini kama hiyo

Wakadumu Mabeberu, watupao kupumua,
Hamnaga kushukuru, hamtoki mtaua?
Bila yao Mabeberu, kwani mngejitambua?
Mnajiita majiwe, beberu saizi yenu!

Wakadumu Mabeberu, watupao kupumua,
Hamnaga kushukuru, hamtoki mtaua?
Bila yao Mabeberu, kwani mngejitambua?
Mnajiita majiwe, beberu saizi yenu!
Hivi kweli mwafurahi,beberu kuwarubuni ?
Tuseme Inna lillahi,wa inna illaihi raj"uni
Huu msiba wallahi,Uhuru wetu wa nini ?
Nalia nasikitika,mwahusudu mashetani.
 
Tena wazidishe kubambika
Unafikiri wao wataishije
Ongezeni dozi matrafik

Ova
Mrangi unachemka,na mawazo ya kichawi
Roho yako ni ya paka,yataka kupigwa kiwi
Dua lako bila shaka ,litaishia Misungwi
Ya Rabi pindua hila,abambikwe babu yake.
 
Hivi kweli mwafurahi,beberu kuwarubuni ?
Tuseme Inna lillahi,wa inna illaihi raj"uni
Huu msiba wallahi,Uhuru wetu wa nini ?
Nalia nasikitika,mwahusudu mashetani.

Iweje mtafurahi, baunsa wetu kudumu?
Vipi msimkebehi, na hata kumshutumu?
Awatia kashi kashi, hakuna kumwaga damu!
Undugu si kufanana, nduguyo ni kufaana!
 
Unamtetea Mrangi,mwenye roho ilopinda
Dua zake mbaya nyingi, inshallah zitadunda
Ataomba mara nyingi,hadi domo litapinda
Simtetee Mrangi,utarithi roho mbaya
Kama tulivyo wengine, hamuhitaji wakili,
Labda yawe mengine, haya Mrangi jabali,
Awahimiza wavune, haramu na vya halali,
Dereva yake ni pesa, vyanzo vyake si muhimu!
 
Waache mabeberu waishi maisha yao na sisi tuishi ya kwetu. Mabeberu hawakufika hapo walipo kwa kutegemea misaada, walipambana km sisi tunavyojaribu kufanya sasa hivi. Hata km kuna sehemu tunakosea kosea ni swala la mda tu mambo yatakua sawa tu.
Kantalambaz umenena,ya kweli na ya hakika
Wanataka kutubana,huko kwao patashika
Korona inawakuna,bado wanahangaika
Mabeberu hayawani,Ngo'mbe kasoro mikia

cc : brazaj
 
Mrangi unachemka,na mawazo ya kichawi
Roho yako ni ya paka,yataka kupigwa kiwi
Dua lako bila shaka ,litaishia Misungwi
Ya Rabi pindua hila,abambikwe babu yake.
Hapana Nna swahiba wangu trafik
Ananipaga sana ofa za biaaaa
Hapa ynyw msg yke imeingia tukatane sehemu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Hapana Nna swahiba wangu trafik
Ananipaga sana ofa za biaaaa
Hapa ynyw msg yke imeingia tukatane sehemu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Duuuh,umetisha mrangi.Kalichune hilo 🤣🤣🤣🤣🤣!!!!!!!! usijali ndugu yangu haya ni malumbano tu ya kuongeza vitamini mwilini na kukuza lugha yetu ya kiswahili.
 
Duuuh,umetisha mrangi.Kalichune hilo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]!!!!!!!! usijali ndugu yangu haya ni malumbano tu ya kuongeza vitamini mwilini na kukuza lugha yetu ya kiswahili.
Hamna jnsi maana sahv kila mtu anaona kama anachelewa,kila mtu anakula kwenye nafasi yake....

Ova
 
Kantalambaz umenena,ya kweli na ya hakika
Wanataka kutubana,huko kwao patashika
Korona inawakuna,bado wanahangaika
Mabeberu hayawani,Ngo'mbe kasoro mikia

cc : brazaj

😂😂😂😂😂😂

Wao kasoro mikia, sisi ming'ombe kabisa!
Ben ametokomea, kauchuna mambosasa,
Azory amepotea, ni visa juu ya visa!
Wale wasojulikana, kwetu ni waajiriwa!

Acheni kumzodoa, Beberu katupa kinga,
Beberu katuokoa, na huu wenu ujinga,
Nia yenu kukomoa, kuuwa au kufunga,
Amewavuta mikia, kisha kawapiga munda!

😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom