Trafic amegoma kumchukulia hatua dreva wa lori la jeshi

Trafic amegoma kumchukulia hatua dreva wa lori la jeshi

Ndo maana mimi huwa napenda kupanda hizo gari haswa za wanajeshi kama wana safari zao kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine

Kuna siku nakumbuka nilipanda gari ya mwanajeshi ilikuwa kutoka Tanga kwenda Moro tukatumia Masaa matatu tu badala ya masaa sita

Wanajeshi usiwashobokee kama wanasafari zao acha wenyewe wampe kazi mpiga debe awatafutie abiria utaenjoy safari yako

Mkifika sehemu ya kula au kuchimba dawa mtaulizwa kabisa mnunue misosi kisha muendelee na safari kama hakuna mnaendelea na safari

Traffic akiipiga mkono akiona gwanda tu anaipigia saruti kisha utasikia, "Muheshimiwa unakimbia sana naomba upunguze sipidi kidogo"
Hii nilikutana nayo wiki iliyopita kwenye yale mataa ya mbuyuni kama unatokea mjini kuitafuta Morocco. Ilikuja coaster SU/STL sikumbuki vizuri. Tukiwa tumesimamishwa na Traffic,jamaa alijipenyeza akapita akaenda zake.
 
Hii nchi imelaaniwa
Huwa siamini mambo ya laana. Lakini nchi zinapishana sana. Tanzania nidhamu ya jeshi uraiani ni zero kabisa. Na wajinga wanashabikia. Naona hata madereva wa serikali nao wameendekezwa sana kufanya ujinga barabarani. Ni aina fulani ya ushamba. Tunafiti kabisa maelezo ya banana republic.

Ajabu sasa ukienda nchi nyingine hapa hapa Afrika kama Ethiopia utaona jinsi jeshi na wanajeshi walivyo na adabu na nidhamu ya hali ya juu mitaani. Kwanza kuwaona mitaani na uniform zao ni jambo la nadra sana labda kuwe na kazi maalum. Magari yao yanakaa foleni kwa adabu kabisa. Hakuna kutanua wala kupita kwenye taa nyekundu. Madereva wao wako vizuri sana kuliko jamaa mitaani. Ikitokea dereva wa jeshi kafanya faulo barabarani polisi wa trafiki wanaweza kumuweka pembeni na hata kuchukua funguo za gari. Uraiani polisi ndio wanaoogopwa kuliko wanajeshi.

Jeshi moto wake ni kwenye uwanja wa vita sio uraiani. Kwetu ni tofauti.
 
Wanajeshi ni waelewa sana, ungemsalimu tu na kumuomba asogeze gari ili watu waweze kupita, angekuelewa.
 
Hii nilikutana nayo wiki iliyopita kwenye yale mataa ya mbuyuni kama unatokea mjini kuitafuta Morocco. Ilikuja coaster SU/STL sikumbuki vizuri. Tukiwa tumesimamishwa na Traffic,jamaa alijipenyeza akapita akaenda zake.
Hakuna nidhamu mpaka levels za chini. Mtu anavuruga magari yanavuka kwenye mataa sababu anaendesha SU. na hana la maana analoenda kufanya.
Nini kimepelekea hali hii? Nidhamu ni kitu cha msingi kwenye kitu chochote. Imagine you are a commander of the army which doesn't follow orders or instructions? You will doom into nothing
 
Ndiyo wenye nchi hao

Wana polisi wao

Wana mahakama zao

Wana Sheria zao

Wana hospitali zao

Gari ya jeshi inapita popote na hawahitaji kutoa maelezo yoyote sababu ndiyo wenye nchi
 
Ndiyo wenye nchi hao

Wana polisi wao

Wana mahakama zao

Wana Sheria zao

Wana hospitali zao

Gari ya jeshi inapita popote na hawahitaji kutoa maelezo yoyote sababu ndiyo wenye nchi
-Nchi ni ya wananchi wote
-Hata Kama wanasheria zao lakini Sheria za nchi zinawahusu pia, ndio maana wiki2 zilizopita Kuna wanajeshi wameshitakiwa kwa kesi ya murder, na kwa Sasa wako Remand prison, na kabla ya kwenda Remand prison walikaa mahabusu ya police Tena kwa adabu na kutii amri zote za police.
 
Kipindi DCP,Mohammed Mpinga akiwa Mkuu wa usalama barabarani Tanzania, alikuwa anawakemea Hadi JWTZ,magari ya taasisi za serikali kuacha kukiuka Sheria za barabarani.
 
-Nchi ni ya wananchi wote
-Hata Kama wanasheria zao lakini Sheria za nchi zinawahusu pia, ndio maana wiki2 zilizopita Kuna wanajeshi wameshitakiwa kwa kesi ya murder, na kwa Sasa wako Remand prison, na kabla ya kwenda Remand prison walikaa mahabusu ya police Tena kwa adabu na kutii amri zote za police.
Hii ni theory kwamba nchi ni ya Wananchi wote

Lakini kiuhalisia nchi ni ya watu wachache sana, siyo wote
 
hapo ulikosea sana ungemfuata yule mwanajeshi umwambie asogeze gari,

angekataa ndiyo ungeenda kushtaki kwa afande trafiki uone angesema nini
 
Hapa sokoni lori la jeshi limepaki kwenye ukingo wa zebra sehemu ya sisi waenda kwa miguu kuvukia. Kwa ufupi lori limebrok zebra na dreva yupo mle kapiga usingizi.

Kwa hiyo nikamfuata trafic ili aje amshughulikie yule mwanajeshi kwa mujibu wa sheria maana waenda kwa miguu wanashindwa kupita pale.

Trafic kaniambia ile sio kazi yangu. Nikaingia sokoni mpaka natoka muda huu nusu saa ile gari bado ipo.

Sheria za nchi hazihusu JWTZ?
Wavaa magwanda ya mabaka mabaka wengi wao ni washamba malimbukeni hapa kajilaza tu hili tarafki amguse wapigane hiyo ndio akili yao washamba sana hawa jamaa
 
Hapa sokoni lori la jeshi limepaki kwenye ukingo wa zebra sehemu ya sisi waenda kwa miguu kuvukia. Kwa ufupi lori limebrok zebra na dreva yupo mle kapiga usingizi.

Kwa hiyo nikamfuata trafic ili aje amshughulikie yule mwanajeshi kwa mujibu wa sheria maana waenda kwa miguu wanashindwa kupita pale.

Trafic kaniambia ile sio kazi yangu. Nikaingia sokoni mpaka natoka muda huu nusu saa ile gari bado ipo.

Sheria za nchi hazihusu JWTZ?
Eneo Gani
 
Back
Top Bottom