Trafic amegoma kumchukulia hatua dreva wa lori la jeshi

Trafic amegoma kumchukulia hatua dreva wa lori la jeshi

Elimu itolewe kwa wananchi na askari wote wasiojielewa.
Tatizo hasa sio elimu. Wengi wanaelewa sana wanachofanya - kwamba si sahihi. Lakini wamejengewa saikolojia kuwa wao ni “watu special” hawatakiwi kubanwa na sheria na taratibu za nchi. Ndivyo watawala wa nchi hii wanavyotaka. Kwamba kuna watu maalum walio juu ya sheria na kuna umma wa “wanyonge”.

Watawala wanapenda kutumia vyombo vya dola kutishia wananchi ili wao wafanye yao bila bugdha. Hadi hali hiyo itakapobadilika ndipo wanajeshi na vyombo vingine vitakapoheshimu sheria. Mwanzoni jeshi letu na wanajeshi waliheshimika sana uraiani. Hakukuwa na huu ujinga na ushamba unaoonekana siku hizi.
 
Police wetu wanaogopa mabaka baka sijui kwann?Yani ni Bora wakumbane na Simba na Sio jW
 
Kwa uelewa wako ni Mali ya nan
Ya watanzania. Jeshi linawatumikia watanzania. Kuzuia huduma bila sababu ya msingi sio kazi ya jeshi. Hili Jeshi lina heshima kubwa sana na limefanya mambo mengi makubwa.
Ukosefu wa nidhamu usitumike kuhalalisha kujifanyia vitu tunavyotaka. Ukosefu wa nidhamu sasa hivi ukiachiwa utaleta matabaka ambayo hayana tija wala afya.
Kumbuka leo mtumishi wa umma, kesho umekaa pembeni. Utaenda barabarani au sokoni na kukutana na hizo kadhia.
Turudi kuheshimu sheria na taratibu. Kuna mambo ya haraka na lazima yafanywe kwa haraka. Ila kwa utaratibu mzuri na unaoeleweka. Sio kama tunavyoona sasa hivi
 
Back
Top Bottom