BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Askari wa usalama wa barabarani 168 wamechukuliwa hatua zikiwamo kushtakiwa kijeshi, kuhamishwa vitengo na kufukuzwa kazi, kutokana na makosa ya kinidhamu ikiwemo rushwa katika kipindi cha kuanzia Juni 2023 hadi Juni 2024.
Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani, Deus Sokoni ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama wa barabarani, inayoambatana na sherehe za miaka 50 tangu kuanzisha kwa Baraza la Usalama wa Barabarani.
Sokoni ameyasema hayo baada ya kuulizwa maswali na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango wakati akikagua mabanda yaliyopo katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Dk Mpango alihoji ni askari wangapi na hatua gani wamechukua.Akijibu swali hilo, Sokoni amesema wamewakamata askari 168 ambapo wengine wameondolewa katika utumishi wa usalama wa barabarani, huku wengine wakichukuliwa hatua za kushtakiwa kijeshi na wengine wakipewa onyo.
Amesema askari wanane kati ya hao walifukuzwa kazi, 84 walionywa huku waliobakia wakihamishiwa katika vitengo vingine.
MWANANCHI