Trapped to a married man

Trapped to a married man

huyu ni single mother mtarajiwa
Amchune vizuri ajitegemee kila kitu maana jamaa akija kufa hatatambulika popote na hivi ndoa ni ya kisiri Siri eti kuoga kumuumiza mke mkubwa ajiandae tu.
 
Kila binadamu hutamani vitu tofauti tofauti na binadamu haridhiki na kitu kimoja hata wewe mkeo humridhishi Ila kspiga kimya tu, kutulia huwa Ni matter ya maamuzi na self control hyo ya kusema hamuridhiki Ni Mila potofu tu za zamani za wanaume kujipendelea, hata nyie wanaume huwa hamturidhishi Ila tunaacha kuhangaika. So inshort hata wanawake tunapenda vitu tofauti, pia binadamu kuridhika ngumu
Hapa sasa umeanza kushusha vile vyenye inatakiwa, tena umfokee akiki imkae sawa. Asilete ubinafsi wake hapa khaaah.
Afu wake zao wakisaliti, kutwa kuimba mapambio km wenzao hawana moyo wa nyama.
 
Amchune vizuri ajitegemee kila kitu maana jamaa akija kufa hatatambulika popote na hivi ndoa ni ya kisiri Siri eti kuoga kumuumiza mke mkubwa ajiandae tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee dea unani vunja mbavu, kumuu miza mke mkubwa huku ikiwa siri, mbona hauwezekan hata, anajidanganya San huyu bibie.
 
Ndio kwani mumekatwaza kula mema ya nchi kila mtu na Uhuru wa mwili wake nashangaa mtu Hali maisha akijifanya mtakatifu woi Mimi siwezi

Cariha umalaya umekupofusha , na ww ni mkristo wa kuzaliwa ila majini ya kishetani ndio yalikutawala moyo wako na bora unyamaze kimya kuliko kuendelea kupotosha watu.

Mada zako zote unashadidia usingle mother , ubinafsi , kuchepuka , kudanga , kuwa huru , unasema wewe mkristo na unaongozwa na ndoa ya kikristo unalijua neno la Mungu wewe ?

Neno la Mungu linasema huna haki wala uhuru kwa mwili wako unapoolewa au kuoa , kwenye ndoa mke ni mume ndiye aliyeshika uhuru wako na mume ni mke ndiye aliyeshika uhuru wako , sasa nyie akina cariha kizazi kilichopotea kwa kukosa malezi na kuongozwa na tamaa zenu mmekuwa mstari wa mbele kupinga mpango wa Mungu aliounzisha kuhusu ndoa , mmejawa na mafundisho ya kishetani ni wepesi kutoa ushauri wa kishetani kama unavyomshauri binti huyu ambaye naye nafsi yake inaongozwa na tamaa kali inayozidi hata kweli na hofu ya Mungu .

Wanawake wote wanaofanikiwa kujenga ndoa ni wale wanaomtegemea Mungu kwa kufuata kweli ya neno la Mungu kwani mwanamke ( Hawa) ndiye aliyedanganywa na shetani na si mwanaume mpaka dhambi na mauti ikaingia ulimwenguni , wanawake wanaojitambua wanajua hilo na hupingana na shetani usiku na mchana na wengi wao ndio hao wenye ndoa imara , watoto wenye malezi bora na watoto wao huwa baraka katika jamii , akina cariha mkae mkijua hamtaweza kamwe kumshinda Mungu katika mipango yake, lakini Mungu atabaki kuwa Mungu wamwaminio wapo na nyie mnaomwamini shetani kwa mgongo wa ukristo wa kuzaliwa endeleenj na maisha yenu ya kipagani.

Hamjachelewa kumbukeni kumrudia Mungu kabla hamjaswaliwa , saidieni jamii sio kuipotosha .
 
Wewe bana sikiliza..!

Kwanza, wengi wanaojidai kukushangaa hapa hasa wanawake, wao wenyewe wanatembea na waume za watu!!

Pili kama ulivyosema wewe, maisha ni mafupi haya, wanaosema ooh vumilia sijui usiipe nafasi furaha ya muda mfupi... wee usiwasikilize hao wana stress zao. Bora furaha ya muda mfupi kuliko kukosa kabisa furaha. Hakuna zawadi utakayopewa kwa kuishi maisha ya tabu. Maisha ni hayahaya usipoenjoy sasahivi ndio basi tena.

Ushauri: We chakufanya, olewa na hako kakijana kanakokupenda ila usiachane na yule mume wa mtu. Badala ya kufunga ndoa kisirisiri ambapo itakulazimu kuachana na yule kijana, wewe olewa na kijana huku ukiendelea kumfaidi mume wa mtu. Nina uhakika mume wa mtu hatakua na pingamizi katika hilo. Hii itakua ni win win situesheni.

[emoji28][emoji28][emoji28]hili lilikuwa wazo mara ya kwanza
Ila naogopa huko mbele mambo yanaweza kuishia sio pazuri
Wote wana uwivu sana
 
Kitu nilicho gundua, mpaka sasa hamjajishtukia kua nyinyi ndio wahusika wakuu alafu mnahadithiana situation zenu [emoji23][emoji23]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huyu sio bana
Japo wote ni wasukuma na seems kuna vitu vinafanana kwenye hizi situation
Nina uhakika si yeye
 
Hauruhusu, hivyo hiyo ndoa itakuwa ya siri milele na ataishi kama michepuko wengine tu. Na si hivyo tu, endapo lolote likimtokea huyu mumewe iwe kustaafu au kufariki basi hana haki yoyote kwa kuwa hatambuliki kama mke.

Na mume anaonekana anampenda sana mkewe ndio maana anataka ndoa ya siri.

Kingine nachokiona , mtoa uzi anadhani mahaba wanayopeana saizi yatadumu milele hivyo hivyo.

But kubwa ambalo kalirudia rudia ni hali nzuri ya kiuchumi ya mume wa mtu, kiasi anaonesha kinachomvutia si mapenzi bali uchumi wa huyo mume wa mtu.

Anasahau kuwa uchumi huwa unapanda au unaporomoka

Ila hajui kuwa wanawake tukishazaa tunaanza kutamani familia ikamilike, awepo baba, mama na mtoto/watoto waamke pamoja wafurahi pamoja. Ikifika hapa ndipo ataona kitu gani anakikosa pale mume wa mtu yupo kwa mkewe na hawezi kutoka, wakati huo yeye na mtoto/watoto wanamuhitaji pia.


Lakini watoto wataozaa watakosa haki ya kuwajua ndugu zao hadi mume atapofariki[emoji23][emoji23]watavyovamia msiba

So sad!!!

Nimesoma ushauri wako
Kuna mengi umeyaandika ni kweli I have to consider them
Najua hii mada inapelekwa in a very emotional way na wanawake wengi I understand na mnisamehe Kama nawakwaza
Kuna vingi sijavielezea hapa
Kwanza mimi sijamroga huyu mwanaume wala kutumia dawa yoyote atleast hapo am not guilty
Nimetambulishwa kwa ndugu zake,mama mkwe na mawifi,marafiki
Usiri ninao usemea hapa ni mke asijue maana hana kosa she doesn’t deserve kuumia kwasababu ya maamuzi yetu ila in future lazima atakuja kujua
All in all kuna vitu umeongea ni point sana
Bado sijafanya maamuzi I can still change my situation before it becomes complicated
 
Yani hujisikii vibaya hata kidogo kuwa mnafiki kwa mwanamke mwenzio..!!!?

Duh mkuu punguza hasira
Hii dunia haina usawa it will never be fair
Wewe mwenyewe kuna sehemu unafanya unafiki
All in all endelea kunipa facts bado sijafanya maamuzi naendelea kupokea mawazo
Asante
 
Apart from how unhealthy your relationship is, it will also result into heart aches and pain in the end. That married man might end up abandoning his family in the name of this new relationship, if you are a Christian, the Bible says, "....na alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe"

Usiwe chanzo cha machozi ya huyo mwanamke mwenzio kisa wewe.

Ushauri wangu kwako, distant yourself from him ukiweza hama huo mji na vunja huo uhusiano, its not too late to do that.

Usilopenda kutendewa usimtendee mtu mwingine

It’s hard but possible
Thank you
 
Halafu Maya ameacha tumshauri yeye kakumbatiana na msukuma, Maya mbinguni utapasikia

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimecheka
Dada angu unaweza kunikuta mbinguni who knows people change
 
Kuna mdada mmoja walimfumania anatembea na mme wa mtu, kilichomkuta hawezi kusahau. (hii ni chorus [emoji3][emoji3])

Ushauri wangu, achana na huyo mme wa mtu... Kama jamaa ameweza kuacha familia yake na kuja kwako na huenda amepunguza huduma kwenye familia yake so watoto wanalia njaa, atashindwa vipi kutokukuacha wewe wa ndoa ya mafichoni na kwenda kwa mwingine tena???
 
Uisilamu ni dini ambayo ipo very updated na asilimia 100% ya watu ktk maisha yao wanagusa ibada za kiislamu...
SINA MAANA KUISIFIA DINI YANGU LAA HASHA.

Ila hilo swala dada yngu ingekuwa inafuata dini ya kiislamu lingepata jawabu jepesi sana...coz ata hyo ndoa isingekuwa ya siri tena...

Wanaume wote tumeumbwa hvyo kupenda wanawake,watoto na mali...
Hakuna duniani mwanaume anae ridhika na mwanamke mmoja never,ndo mana tukapewa options ya wanne.

Ushauri wangu:-
Tatizo sio kukuoa mke wa pili Ila tatizo linakuja Kwenye uadilifu wa kuwahudumia wake wawili hasa baada ya kufunga ndoa...kaa ukijua maisha ya uchumba yanatofautiana Sana na maisha ya ndoa pia yanatofautia zaidi Sana na maisha baada ya kupata watoto.
Mwanamke unapokubali kuongezwa au kuongezewa mke mwenza embu angalia huyo mwanaume akili zake na misimamo yake ikiwemo na Imani yake.

Ndoa ya uke wenza inahitaji mwanaume mwenye akili,Imani na misimamo thabiti sio wa kuyumbisshwa au kupelekeshwa.

Nahitimisha kwa kusema huyu mwanaume si wakumuamini mchunguze vzur kabla hamjafunga hyo ndoa ya SIRI.

Sawa Asante sana huko mwishoni nimekuelewa
 
Speaking the honestly
Wew Dada unajidanganya unavo sema unawapenda wote wawili

Huyu Jamaa ambae yupo single humpendi, nakuomba muache na maisha yke akatafute wa kufanana nae

Life is too short Kama umeridhia kua na Mume wa mtu na moyo umekusuma nenda ( chochote kitakacho tokea ni your choice)

Ila single boy wa watu muache

Unaitaji ku enjoy maisha na kutafuta a truly love

Aisee kumuacha siwezi
Bado sijapata mtu kama yeye,kwasababu hii sio mada yake ndio maana sijapata nafasi ya kumuelezea.Kama ningekuwa simpendi huu uzi usingekuwa hapa ninge jilipua na huyu jamaa mwenye mke
 
Nimesoma ushauri wako
Kuna mengi umeyaandika ni kweli I have to consider them
Najua hii mada inapelekwa in a very emotional way na wanawake wengi I understand na mnisamehe Kama nawakwaza
Kuna vingi sijavielezea hapa
Kwanza mimi sijamroga huyu mwanaume wala kutumia dawa yoyote atleast hapo am not guilty
Nimetambulishwa kwa ndugu zake,mama mkwe na mawifi,marafiki
Usiri ninao usemea hapa ni mke asijue maana hana kosa she doesn’t deserve kuumia kwasababu ya maamuzi yetu ila in future lazima atakuja kujua
All in all kuna vitu umeongea ni point sana
Bado sijafanya maamuzi I can still change my situation before it becomes complicated
Mimi situmii mihemko kabisa.

Nakwambia tu ukweli, na mimi sipingi kabisa ndoa ya wake wengi, naipenda mno.

Tatizo wewe, kuna kikwazo cha dini, usiri, kuna hapo naona mali za jamaa ndio zinakuchanganya si pendo la dhati, naamini pia kwa maandishi yako na mahaba yake ndio yamekutia upofu.

Kuwa makini, usione wanawake tunakuonea wivu, labda tunaongea kutokana na experience za kuwa na uhusiano/ndoa na hao waliokuwa wameoa, hapa tunakusaidia tu kukupa black&white.

All in all maisha ni yako, chaguo ni lako
 
[emoji28][emoji28][emoji28]hili lilikuwa wazo mara ya kwanza
Ila naogopa huko mbele mambo yanaweza kuishia sio pazuri
Wote wana uwivu sana

Binti Maya Angelou humu wengi walichokushauri usiolewe na mume wa mtu wapo sahihi , maisha ya uke wenza utaishia kulogwa na kujitafutia laana na mikosi isiyo ya lazima kutoka kwa mke wake na watoto ambao watakosa huduma
bora kutoka kwa baba yao ingawa unajifanya umejiandaa kukabaliana na hali ya uke wenza na ndio upagani wenyewe huu tunaosema .Huyo kijana single humpendi kwa kuwa unamuona hataweza kufulfil your desired future life ukilinganisha na huyo married man ambaye kachuma na mkewe ndio maana unamuona kanawiri na mzoefu katika kuchepuka tofauti na huyo single , kwa kuwa mlishaanza mapenzi naye ukiwa binti mdogo yawezekana ndiye alifungua mlango , omba sana kwa kufunga na kumaanisha Mungu akuondolee kifungo cha kumkumbuka huyo mwanaume mme wa mtu kwani usipofanya hivyo hata ukija kuolewa na kijana single utajikuta kila akikuita for s.. unamfuata kama mbwa anavyofuta kuliwa na chatu .Usikubali mafundisho ya kura raha na wanaume za watu , kuchuna wanaume za watu hata maisha ya kudanga , hayo waachie wenyewe wanawake wengi walioamua mfumo huo wa maisha na angalia sana saloon unazokwenda na epuka marafiki wote wenye tabia hizo , nakutakia utulivu na upate wako mtayejenga maisha yenu uje kuwa na ndoa bora sio bora ndoa au bora kuzaa tu.
 
"Meanwhile upande wa pili kuna kaka ambae hajaoa anataka kuja kutoa mahali,well paying job we have a connection lakini hajafika level za yule mume wa mtu"

Vijana wenzangu tutafute hela tu si mmeona kinachoendelea.
 
Mimi mwenyewe mkiristo ila ndio hivyo nafsi yangu ndio imefikia maamuzi ya kuoa mke wa pili. Nimemwambia tutafunga ndoa hata kwa kujificha, kama ndoa haitawezekana basi tuishi bila ndoa. Cheti cha ndoa ni makaratasi tu wala hayachangii chochote kwenye kupendana.
Tamaa yako tu kama cheti ni makaratasi ulioa ili iweje? Ishi na huyo mchepuko wako pia kama ndoa ni makaratasi,unataka kuoa ndoa ya siri ya nini??

Mkishachoka wake zenu mbatafuta visingizio tu....ila hata yeye huyo mchepuko siku moja atakuja kuwa kama mkeo baada ya kuzaa atakosa mvuto kwako sijui utaoa wangapi???
 
Inawezekana ndio au hapana nimeshindwa kuifafanua situation hii vizuri
Lakini naomba tu nikwambie nipo wakati mgumu
Umeshawahi kupenda watu wawili kwa wakati mmoja?
Hakuna kupenda watu wawili kwa wakati mmoja hicho kiyu hakipo....

Ni kwamba umempenda mzee sababu ya pesa yake ila unaogopa ni mume wa mtu,huyu mchumba hujampenda upo nae tu sababu unataka mume tu nawe uonekane umeolewa.

Hata ukiolewa na mchumba wako bado utachepuka na mzee tu. Sasa jiulize unampenda nani100%,yupi unapenda kuwa nae karibu? Jibu unalo nadhani....so kupenda watu wawili kwa wakati mmoja hakupo.
 
Back
Top Bottom