Trapped to a married man

huyu ni single mother mtarajiwa
Amchune vizuri ajitegemee kila kitu maana jamaa akija kufa hatatambulika popote na hivi ndoa ni ya kisiri Siri eti kuoga kumuumiza mke mkubwa ajiandae tu.
 
Hapa sasa umeanza kushusha vile vyenye inatakiwa, tena umfokee akiki imkae sawa. Asilete ubinafsi wake hapa khaaah.
Afu wake zao wakisaliti, kutwa kuimba mapambio km wenzao hawana moyo wa nyama.
 
Amchune vizuri ajitegemee kila kitu maana jamaa akija kufa hatatambulika popote na hivi ndoa ni ya kisiri Siri eti kuoga kumuumiza mke mkubwa ajiandae tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee dea unani vunja mbavu, kumuu miza mke mkubwa huku ikiwa siri, mbona hauwezekan hata, anajidanganya San huyu bibie.
 
Ndio kwani mumekatwaza kula mema ya nchi kila mtu na Uhuru wa mwili wake nashangaa mtu Hali maisha akijifanya mtakatifu woi Mimi siwezi

Cariha umalaya umekupofusha , na ww ni mkristo wa kuzaliwa ila majini ya kishetani ndio yalikutawala moyo wako na bora unyamaze kimya kuliko kuendelea kupotosha watu.

Mada zako zote unashadidia usingle mother , ubinafsi , kuchepuka , kudanga , kuwa huru , unasema wewe mkristo na unaongozwa na ndoa ya kikristo unalijua neno la Mungu wewe ?

Neno la Mungu linasema huna haki wala uhuru kwa mwili wako unapoolewa au kuoa , kwenye ndoa mke ni mume ndiye aliyeshika uhuru wako na mume ni mke ndiye aliyeshika uhuru wako , sasa nyie akina cariha kizazi kilichopotea kwa kukosa malezi na kuongozwa na tamaa zenu mmekuwa mstari wa mbele kupinga mpango wa Mungu aliounzisha kuhusu ndoa , mmejawa na mafundisho ya kishetani ni wepesi kutoa ushauri wa kishetani kama unavyomshauri binti huyu ambaye naye nafsi yake inaongozwa na tamaa kali inayozidi hata kweli na hofu ya Mungu .

Wanawake wote wanaofanikiwa kujenga ndoa ni wale wanaomtegemea Mungu kwa kufuata kweli ya neno la Mungu kwani mwanamke ( Hawa) ndiye aliyedanganywa na shetani na si mwanaume mpaka dhambi na mauti ikaingia ulimwenguni , wanawake wanaojitambua wanajua hilo na hupingana na shetani usiku na mchana na wengi wao ndio hao wenye ndoa imara , watoto wenye malezi bora na watoto wao huwa baraka katika jamii , akina cariha mkae mkijua hamtaweza kamwe kumshinda Mungu katika mipango yake, lakini Mungu atabaki kuwa Mungu wamwaminio wapo na nyie mnaomwamini shetani kwa mgongo wa ukristo wa kuzaliwa endeleenj na maisha yenu ya kipagani.

Hamjachelewa kumbukeni kumrudia Mungu kabla hamjaswaliwa , saidieni jamii sio kuipotosha .
 

[emoji28][emoji28][emoji28]hili lilikuwa wazo mara ya kwanza
Ila naogopa huko mbele mambo yanaweza kuishia sio pazuri
Wote wana uwivu sana
 
Kitu nilicho gundua, mpaka sasa hamjajishtukia kua nyinyi ndio wahusika wakuu alafu mnahadithiana situation zenu [emoji23][emoji23]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huyu sio bana
Japo wote ni wasukuma na seems kuna vitu vinafanana kwenye hizi situation
Nina uhakika si yeye
 

Nimesoma ushauri wako
Kuna mengi umeyaandika ni kweli I have to consider them
Najua hii mada inapelekwa in a very emotional way na wanawake wengi I understand na mnisamehe Kama nawakwaza
Kuna vingi sijavielezea hapa
Kwanza mimi sijamroga huyu mwanaume wala kutumia dawa yoyote atleast hapo am not guilty
Nimetambulishwa kwa ndugu zake,mama mkwe na mawifi,marafiki
Usiri ninao usemea hapa ni mke asijue maana hana kosa she doesn’t deserve kuumia kwasababu ya maamuzi yetu ila in future lazima atakuja kujua
All in all kuna vitu umeongea ni point sana
Bado sijafanya maamuzi I can still change my situation before it becomes complicated
 
Yani hujisikii vibaya hata kidogo kuwa mnafiki kwa mwanamke mwenzio..!!!?

Duh mkuu punguza hasira
Hii dunia haina usawa it will never be fair
Wewe mwenyewe kuna sehemu unafanya unafiki
All in all endelea kunipa facts bado sijafanya maamuzi naendelea kupokea mawazo
Asante
 

It’s hard but possible
Thank you
 
Halafu Maya ameacha tumshauri yeye kakumbatiana na msukuma, Maya mbinguni utapasikia

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimecheka
Dada angu unaweza kunikuta mbinguni who knows people change
 
Kuna mdada mmoja walimfumania anatembea na mme wa mtu, kilichomkuta hawezi kusahau. (hii ni chorus [emoji3][emoji3])

Ushauri wangu, achana na huyo mme wa mtu... Kama jamaa ameweza kuacha familia yake na kuja kwako na huenda amepunguza huduma kwenye familia yake so watoto wanalia njaa, atashindwa vipi kutokukuacha wewe wa ndoa ya mafichoni na kwenda kwa mwingine tena???
 

Sawa Asante sana huko mwishoni nimekuelewa
 

Aisee kumuacha siwezi
Bado sijapata mtu kama yeye,kwasababu hii sio mada yake ndio maana sijapata nafasi ya kumuelezea.Kama ningekuwa simpendi huu uzi usingekuwa hapa ninge jilipua na huyu jamaa mwenye mke
 
Mimi situmii mihemko kabisa.

Nakwambia tu ukweli, na mimi sipingi kabisa ndoa ya wake wengi, naipenda mno.

Tatizo wewe, kuna kikwazo cha dini, usiri, kuna hapo naona mali za jamaa ndio zinakuchanganya si pendo la dhati, naamini pia kwa maandishi yako na mahaba yake ndio yamekutia upofu.

Kuwa makini, usione wanawake tunakuonea wivu, labda tunaongea kutokana na experience za kuwa na uhusiano/ndoa na hao waliokuwa wameoa, hapa tunakusaidia tu kukupa black&white.

All in all maisha ni yako, chaguo ni lako
 
[emoji28][emoji28][emoji28]hili lilikuwa wazo mara ya kwanza
Ila naogopa huko mbele mambo yanaweza kuishia sio pazuri
Wote wana uwivu sana

Binti Maya Angelou humu wengi walichokushauri usiolewe na mume wa mtu wapo sahihi , maisha ya uke wenza utaishia kulogwa na kujitafutia laana na mikosi isiyo ya lazima kutoka kwa mke wake na watoto ambao watakosa huduma
bora kutoka kwa baba yao ingawa unajifanya umejiandaa kukabaliana na hali ya uke wenza na ndio upagani wenyewe huu tunaosema .Huyo kijana single humpendi kwa kuwa unamuona hataweza kufulfil your desired future life ukilinganisha na huyo married man ambaye kachuma na mkewe ndio maana unamuona kanawiri na mzoefu katika kuchepuka tofauti na huyo single , kwa kuwa mlishaanza mapenzi naye ukiwa binti mdogo yawezekana ndiye alifungua mlango , omba sana kwa kufunga na kumaanisha Mungu akuondolee kifungo cha kumkumbuka huyo mwanaume mme wa mtu kwani usipofanya hivyo hata ukija kuolewa na kijana single utajikuta kila akikuita for s.. unamfuata kama mbwa anavyofuta kuliwa na chatu .Usikubali mafundisho ya kura raha na wanaume za watu , kuchuna wanaume za watu hata maisha ya kudanga , hayo waachie wenyewe wanawake wengi walioamua mfumo huo wa maisha na angalia sana saloon unazokwenda na epuka marafiki wote wenye tabia hizo , nakutakia utulivu na upate wako mtayejenga maisha yenu uje kuwa na ndoa bora sio bora ndoa au bora kuzaa tu.
 
"Meanwhile upande wa pili kuna kaka ambae hajaoa anataka kuja kutoa mahali,well paying job we have a connection lakini hajafika level za yule mume wa mtu"

Vijana wenzangu tutafute hela tu si mmeona kinachoendelea.
 
Tamaa yako tu kama cheti ni makaratasi ulioa ili iweje? Ishi na huyo mchepuko wako pia kama ndoa ni makaratasi,unataka kuoa ndoa ya siri ya nini??

Mkishachoka wake zenu mbatafuta visingizio tu....ila hata yeye huyo mchepuko siku moja atakuja kuwa kama mkeo baada ya kuzaa atakosa mvuto kwako sijui utaoa wangapi???
 
Inawezekana ndio au hapana nimeshindwa kuifafanua situation hii vizuri
Lakini naomba tu nikwambie nipo wakati mgumu
Umeshawahi kupenda watu wawili kwa wakati mmoja?
Hakuna kupenda watu wawili kwa wakati mmoja hicho kiyu hakipo....

Ni kwamba umempenda mzee sababu ya pesa yake ila unaogopa ni mume wa mtu,huyu mchumba hujampenda upo nae tu sababu unataka mume tu nawe uonekane umeolewa.

Hata ukiolewa na mchumba wako bado utachepuka na mzee tu. Sasa jiulize unampenda nani100%,yupi unapenda kuwa nae karibu? Jibu unalo nadhani....so kupenda watu wawili kwa wakati mmoja hakupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…