Mkuu, umeongea ukweli kabisa. Pamoja na tamaa zetu wanaume lakini wadada wamekuwa ni warahisi sana, sana kupita maelezo. Kuishinda tamaa ya uzinzi kunahitaji kujitoa, sio kitu rahisi lakini ukijiwekea nadhiri, ukiangalia familia yako unaona ya nini nitese wanangu kwa tamaa za kupita.
Siku hizi tunatongozwa, hatujisifu ilà wanakuja wenyewe, wanajilengesha wenyewe, hadi unaulizwa hivi wewe ni mwanaume kweli, huoni kama nakupenda, naelewa una familia lakini nitaiheshimu familia yako, nakuhitaji wewe tu! Unabaki 'hihihiiiii', unampotezea hadi aelewe. Sitaki kusema sana maana watu hawachelewi kusema tunajisifu ilà tunatongozwa sana kipindi hiki, it's sad!!!