Mdogo wangu Mungu kakupa dhahabu mbili anataka uchague. Mimi ningekuwa wewe mingechagua huyo ambae hana Mke.
My dia mapenzi yana ukomo, ebu piga picha Mke mkubwa akijua? Duniani hakuna siri, utaenjoy kwa muda mfupi sana.ukishazaa Mme mapenzi anarufisha kwa mkewe.
Dia kabla hujaja hapa umemwambia mama yako? Hivi unajua Siku akijua nini kitatokea?
Mtu akishakuwa na title ya Mme wa mtu basi sio wako, usichezee hii bahati. Akikuoa vikwazo vitaanza, Mara watoto wanaumwa ndo maana sikuja, kumbe uongo.
Eti kuwa serious na maombi kwa Siku tatu. Fanya hivi.
Chukua vikaratasi viwili, andika majina yao kwenye karatasi hizo kila karatasi jina lake, weka kwenye biblia ( kwa imani yako) umwambie mungu kati ya hao akupe jibu sahihi, ongeea chochote umwambie wewe ni baba basi nioneshe njia nisipotee.
Baadae ya hapo kunja hivyo vikaratasi wakati umefumba macho, viweke chini, umwambie Mungu akuchagulie na okota kimoja fumbua macho urudi hapa unipe jibu.
Nb kuwa makini usipate mimba kipindi hiki ambacho huna maamuzi.