TRC boresheni haya, nimepanda treni yenu ni nzuri ila tunahitaji maboresho zaidi

kwente ticket trc watumie mfumo wa mabasi uko efficient sana
 
Ndugu umenena safi kabisa, tatizo ni kuwa baadhi ya mapungufu yamewekwa kutengeneza fursa kwa watu fulani ili watengeneze pesa
 
Kupanda na vyakula ni BIG NO!
Msilete ushamba.
Na tukumbuke Express ni Express na siyo treni ya wafanyakazi wa serikali.
Hayo ni maoni yako nayaheshimu Mkuu. ila kumbuka ukipanda na chakula sio lazima ule. unanunua zabibu za elfu 5 upelekee familia Dsm unaambiwa haziruhusiwi. Think again
 
Kwenye ndege sato wanakuwa eneo la mixogo sasa mshamba anataka single na sato na vyakula eneo la abiria hiyo kiboko
Unaweza kuniita mshamba kwa sababu hatufahamiani. Ila ujue tu madege nimepanda mpaka ya kutoka nje hili bara letu kwenda mabara mengine na nimejifunza mengi sana.

Waweke sehemu ya parcels, treni ni yetu waboreshe. Huko kwa wenzetu imewezekanaje? Think on it
 
Nimeangalia wingi watanzania wanaosafiri kwenda kwenye mji wa serikali kutafuta huduma.
Tukiongeza consideration ya Hospital ya Benjamini mkapa bado ilipo stesheni ni mbali sana.
Badala ya kupinga pinga kila kitu, TRC watafanya analysis wenyewe. Ninachoamini inawezekana kuweka kituo eneo ambalo sio mbali na mji wa Serikali ili kurahisisha huduma kwa watanzania na wageni wote wanaosafiri kwenda kwenye hizo Wizara kupata huduma.
 
Kwenye ndege unaingia na ugali wako wa muhogo?
Katika fikira zako chakula ni ugali tu?
ukinunua zabibu zikafungwa vizuri kwenye kiboksi unatoka Dodoma unaenda Dsm ukazibeba kuna ubaya gani? na isitoshe zinauzwa pale pale stesheni.

Pointi ya msingi ni ku-regulate vyakula gani vipande kama mzigo tu wanaweza tenga sehemu maalumu.

Ndugu yangu unaweza kupanda Ethiopia Airline na ndoo ya samaki frozen, kwanini usipande na ndoo ya samaki frozen kwenye sgr? ni utaratibu tu.

Hata wewe unayepinga hapa siku Sgr wakiboresha hili utakuwa wa kwanza kubeba parcels kupelekea familia yako zawadi, Watanzania ndivyo tulivyo
 
Zikiwekwa standards of service, tusipende kuzi cheapen kwa sabababu zisizo na msingi.
Otherwise mabasi bado yapo, kapande kule.
 
Hivi ni sahihi kusema Treni yenu au Treni yetu? Ukizingatia kodi yetu ..
 
Umetoa mapendekezo mazuri sana na ya muhimu pia. Hilo pendekezo namba 1 kwa kweli lina chefua sana
 
Uko sahihi, upumbavu wa kuwekeana royal tour mwanzo mpaka mwisho wa safari unakera sana.
Alafu ile chai yao ni wizi, kikopo kidogo na bado wanakupa nusu! Unabaki unajiuliza hivi kuibia watu ni sifa?
 
Unaboa! Huu ni ukauzu tu
 
Hapo namba 01 umenikosha kiongozi..Yaani UCHAWA umekuwa tatizo kubwa kwa sasa..sijui ipo kwenye Job description ya kila Taasisi na wateule wote??..yaani kama miKASUKU..ujinga
Huu ugonjwa alituachia Mzee baba
 
Uko sahihi, upumbavu wa kuwekeana royal tour mwanzo mpaka mwisho wa safari unakera sana.
Alafu ile chai yao ni wizi, kikopo kidogo na bado wanakupa nusu! Unabaki unajiuliza hivi kuibia watu ni sifa?
Kumbe ile chai ya wizi ni kote hahaha nilijua ni mimi tu nimepigwa!!
Yani chai ya rangi ya buku kikopo kidogo na bado wakaweka nusu?? Nilishangaa sana

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
 
Safi sana, hii ndio maana ya think tank.
 
Tunatofautiana kwenye matumizi ya chakula kulingana na afya ya mtu, wapo wasiotumia chumvi, mafuta, sukari, nyama na wanga kwa wingi.
Kula nyumbani kwako kabisa kabla ya safari au nunuwa snacks na maji hakuna atakayekuzia.

Safari ya masaa machache unataka kula nini? Si utakula unachotaka ukifika?

Mimi hata safari ya masaa 12 bus likisimama sehemu ya chakula huwa nanunuwa clips na maji na juice tuz sili chakula njiani.
 
Mimi namba 1, hivi Watanzania tuna nini? Yaani kuanzia viongozi lazima wasifie Raisi, sasa kwenye usafiri wa umma mnaleta hayo. Niyeye katoa hela yake kutujengea hiyo SGR?
Mkitaka kusifia, tajeni kila jina la mlipa kodi katika hii nchi. Huyo mnayemsifia visivyosifika hauziki, msituchoshe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…