TRC boresheni haya, nimepanda treni yenu ni nzuri ila tunahitaji maboresho zaidi

Jamaa Umeongea Point Sana.Tatizo Mashaka ana Mashaka Sana
 
Nichangie
1. Hii ni kweli wapunguze, mule ndani ya treni TV yake inaonyesha Royal Tour tu from Morning to midnight 24/7 to and fro. Inachosha waweke vitu vingine pia.

2. Madirisha ya wahudumu huenda ni kweli ingawa foleni yake si kubwa kiasi hicho, na ndio maana unaambiwa ufike masaa 2 kabla ya safari utaepuka mengi.

3. Mji wa Serikali na SGR wapi na wapi bro? Hilo haliwahusu TRC, labda kwa baadae sana wakiona ipo haja ila kwa sasa big no, panda public transport, Bajaj, Boda nk utafika tu

4. Kupanda na chakula BIG NO. Hapana kabisa mtatuchafulia treni yetu. Treni ya alfajiri unataka upande na chakula ili iweje? Treni ya jioni upande na msosi ili iweje, huo ni ushamba, acha kula kula hovyo uanze kuharisha ndani ya SGR utachafua vyoo na harufu kali ya mavi

5. Unaweza ukawa upo sahihi kwenye issue ya Code. Hii inaitwa one time user verification code Kwa ajili ya kurerve siti, sisio ishu sana, maana hata muda wa registration unapata hiyo code, sijaona tatizo labda kama haupo kwenye network nzuri. Wakiweza hizo codes sio za umuhimu sana.

6. Bei ya vyakula ni standard zao bro, kwani kilo 1 ya korosho ukienda Shoppers au Mlimani City bei yake ni sawa na ukinunua soko la temeke? And still bei za wine au beer ni reasonable tu elfu 5 au elfu 8 tena usipoangalia hata haiishi mpaka unafika safari yako. Kama huezi kununua we lala tu kwenye behewa utafika.
 
Hiyo namba 3 kiboko yao.

All in all, unapoint usikilizwe.
 
Kwenye matangazo ya kumpamba Rais kwa kweli inafedhehesha sana ila angalizo tu wasiweke kabisa video/miziki iliyokosa maadili kama wanavyofanya wenye mabasi.

Hapo kwenye chakula kwa jinsi tulivyo watanzania ni bora waendelee kukataza.
 
Maoni yako nayaheshimu.
ila kile unachowaza sio ninachowaza mimi.

Unawaza chakula kama ugali na samaki? hapana, mi nawaza vitu kama parcels za vyakula ambavyo mtu anaweza kubeba kama zawadi akiwa anarejea home. Ingekua ni dhambi sana basi hata ndege watu wasingebeba vitu kama samaki.

Uhusiano wa Sgr na mji wa Serikali upo, mji wa Serikali ndio kuna Wizara zote zinazohudumia Watanzania. Sasa waza vema mtu ashuke stesheni ya sgr alaf asafiri zaidi ya 20km kwenda mji wa Serikali wakati kuna option ya mtu huyo kushuka sehemu ambayo ni karibu na mji wa Serikali akiwa anaenda Wizara X kufatilia mambo yake.
 
Zikiwekwa standards of service, tusipende kuzi cheapen kwa sabababu zisizo na msingi.
Otherwise mabasi bado yapo, kapande kule.
Hakuna sababu zisizo za msingi na bado nikaziweka hapa. Tuwe na exposure mbona nimetoa mifano mingi tu.
kumtangaza Rais kwa masaa manne ya safari is nonsense, hata wenzetu hawafanyi ivo tembeeni duniani Watanzania wenzangu.

kuzuia kila kitu is nonsense, waweke utaratibu mtu anaweza kusafiri na parcel ya chakula sio kwa ajili ya kula yeye wakati wa safari. TRC iandae eneo la parcels kama kwenye ndege inawezekana why treni yetu wenyewe isiwezekane?
 
Unaboa! Huu ni ukauzu tu
umetembea sana ni Mwananyamala utajua wapi dunia ndugu yangu.
Tunatoa maoni kuboresha kadri tulivyoona wenzetu duniani wanafanya maana hata treni tumenunua kwa wenzetu hatujaunda wenyewe, reli tumejengewa na wenzetu hatujajenga wenyewe. Kimsingi tunajifunza kwa aliyefanikiwa.
 
Hapo namba 01 umenikosha kiongozi..Yaani UCHAWA umekuwa tatizo kubwa kwa sasa..sijui ipo kwenye Job description ya kila Taasisi na wateule wote??..yaani kama miKASUKU..ujinga
Yangejua yanavyokera haya ma mba.
 
Id yako inasema una PhD? labda ni Id tu. Nakukumbusha chakula sio lazima kile kilicho tayari kuliwa.
Ukibeba parcel ya mihogo mibichi imefungwa vema nacho ni chakula, ukibeba zabibu kwenye boksi nacho ni chakula ila TRC haitaki.

Haya mambo yanawezekana, TRC iandae utaratibu tu na wanaweza kuongeza mapato kwa kulipisha nauli ya mzigo kulingana na uzito. watenge sehemu ya parcels tu mbona ndege tunalipa kusafiri na samaki kutoka Mwanza? mi sielewi mkisikia chakula kwanini mnawaza wali na ugali nyama🤣🤣
 
No 1 ni sawa. Ungeachia hapo ningekuona wa maana. ila namba 4 inaonesha ulivyo na uelewa mdogo. Unataka ishushe kila pahala? No. 5 umeonesha uzumbukuku, je uliona wapi Train watu wanafungua migogo iliyochacha au kiporo cha uji. Si upande basi. No. 6. sasa unajifanya mtaalam wa IT acha wafanye yao maana kuna kuhakiki. No. 7 acha kununua vitu kama huna uwezo. Panda basi ununue dirishani.
 
Ulala hoi kubebea viporo
 
Naona umekazania chakula chakula, ni chakula unataka kusafirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…