Nichangie
1. Hii ni kweli wapunguze, mule ndani ya treni TV yake inaonyesha Royal Tour tu from Morning to midnight 24/7 to and fro. Inachosha waweke vitu vingine pia.
2. Madirisha ya wahudumu huenda ni kweli ingawa foleni yake si kubwa kiasi hicho, na ndio maana unaambiwa ufike masaa 2 kabla ya safari utaepuka mengi.
3. Mji wa Serikali na SGR wapi na wapi bro? Hilo haliwahusu TRC, labda kwa baadae sana wakiona ipo haja ila kwa sasa big no, panda public transport, Bajaj, Boda nk utafika tu
4. Kupanda na chakula BIG NO. Hapana kabisa mtatuchafulia treni yetu. Treni ya alfajiri unataka upande na chakula ili iweje? Treni ya jioni upande na msosi ili iweje, huo ni ushamba, acha kula kula hovyo uanze kuharisha ndani ya SGR utachafua vyoo na harufu kali ya mavi
5. Unaweza ukawa upo sahihi kwenye issue ya Code. Hii inaitwa one time user verification code Kwa ajili ya kurerve siti, sisio ishu sana, maana hata muda wa registration unapata hiyo code, sijaona tatizo labda kama haupo kwenye network nzuri. Wakiweza hizo codes sio za umuhimu sana.
6. Bei ya vyakula ni standard zao bro, kwani kilo 1 ya korosho ukienda Shoppers au Mlimani City bei yake ni sawa na ukinunua soko la temeke? And still bei za wine au beer ni reasonable tu elfu 5 au elfu 8 tena usipoangalia hata haiishi mpaka unafika safari yako. Kama huezi kununua we lala tu kwenye behewa utafika.