N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Nimesoma taarifa ya gazeti la The Citizen kuhusu tiketi takribani 782,000 za treni za SGR zilizonunuliwa lakini hazikutumika kati ya Januari na Septemba 2026.
Katika ufafanuzi wake Bungeni, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ameeleza kuwa baadhi ya siti zinazoonekana kuwa wazi ndani ya treni tayari zimehifadhiwa kwa ajili ya abiria watakaopanda katika vituo vinavyofuata.
Ametoa mfano wa siti iliyohifadhiwa kwa abiria anayesafiri kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam, ambayo inaweza kuonekana wazi kabla treni haijafika Morogoro, lakini isiweze kuuzwa kwa abiria mwingine.
HAPA NDIPO NINAPOONA KUNA TATIZO LA MFUMO WA UKATAJI TIKETI WA TRC LINALOHITAJI KUFANYIWA MABORESHO.
Kwa nini siti iliyohifadhiwa kwa safari ya Morogoro kwenda Dar es Salaam isitumike kwa abiria mwingine anayesafiri kutoka Dodoma kwenda Morogoro?
Vivyo hivyo, ikiwa abiria amenunua tiketi ya Morogoro kwenda Dodoma, kwa nini siti hiyo isiuzwe kwa abiria mwingine anayetaka kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro?
Kwa mantiki ya kawaida, siti inapaswa kuhifadhiwa kwa kipande cha safari ambacho abiria amelipia, badala ya kuonekana kuwa imejaa katika safari nzima wakati kuna vipande ambavyo haijatumika.
Mfano:
Huu si utaratibu mpya.
Mifumo ya kisasa ya uhifadhi wa nafasi za usafiri inaweza kuruhusu siti moja kuuzwa kwa abiria tofauti kulingana na vituo vya kupanda na kushuka (segment-based seat inventory management).
Mfumo mzuri unapaswa kutambua kuwa siti inaweza kuwa imeuzwa katika kipande kimoja cha safari lakini bado inapatikana katika kipande kingine.
TRC MNAPASWA KUBORESHA MFUMO WENU ILI KUONGEZA UFANISI WA MATUMIZI YA SITI.
Iwapo mfumo wa sasa hauruhusu jambo hili, basi kuna haja ya kuufanyia maboresho.
Vijana wa EGA wako vizuri kwenye mifumo they can help you with that, tayari wameshaunda mifumo complex ya e government kuzidi huo wa siti.
Lakini iwapo tayari unaruhusu, TRC wanapaswa kueleza kwa kina zaidi kwa nini bado abiria wanakutana na changamoto ya kuambiwa tiketi zimeisha wakati kuna siti zinazoonekana wazi.
Ukipanda treni ya Alfajiri kutokea Dodoma kwenda Dar siti nyingi huwa tupu na huja kujazwa Morogoro. Ni kwamba Dodoma Dar abiria ni wachache?!
Maboresho haya yanaweza kuongeza upatikanaji wa tiketi, kupunguza siti kusafiri bila abiria katika baadhi ya vipande vya safari, kuongeza mapato ya TRC na kuboresha uzoefu wa wateja.
Aidha, takwimu za tiketi zilizonunuliwa lakini hazikutumika zinapaswa kuchambuliwa kwa kutofautisha abiria ambao hawakufika kusafiri (no-shows) na siti ambazo zilikuwa wazi kwa sababu zilihifadhiwa kwa abiria wa vituo vinavyofuata. Haya ni masuala mawili tofauti yanayohitaji ufumbuzi tofauti.
Bwana Naibu Waziri na uongozi wa TRC, hili mlifanyie kazi. SGR ni uwekezaji mkubwa wa Taifa, hivyo tunapaswa kuhakikisha kila siti inatumika kwa ufanisi kadiri inavyowezekana.
Hatuwezi kuwa na abiria wanaokosa tiketi huku siti zikisafiri zikiwa wazi kwa sababu tu zimehifadhiwa kwa abiria watakaopanda vituo vya mbele.
Je, TRC mfumo wenu wa ukataji tiketi unaruhusu siti moja kuuzwa kwa abiria tofauti katika vipande tofauti vya safari? Kama hauruhusu, kwa nini?
Nawasilisha.

- Abiria A anasafiri Dar es Salaam–Morogoro.
- Abiria B anasafiri Morogoro–Dodoma.
- Abiria C anasafiri Dodoma–Tabora.