TRC kwanini siti iliyokatiwa tiketi ya Morogoro–Dar AU Morogoro–Dodoma ionekane imejaa tangu mwanzo wa safari?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Nimesoma taarifa ya gazeti la The Citizen kuhusu tiketi takribani 782,000 za treni za SGR zilizonunuliwa lakini hazikutumika kati ya Januari na Septemba 2026.

Katika ufafanuzi wake Bungeni, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, ameeleza kuwa baadhi ya siti zinazoonekana kuwa wazi ndani ya treni tayari zimehifadhiwa kwa ajili ya abiria watakaopanda katika vituo vinavyofuata.

Ametoa mfano wa siti iliyohifadhiwa kwa abiria anayesafiri kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam, ambayo inaweza kuonekana wazi kabla treni haijafika Morogoro, lakini isiweze kuuzwa kwa abiria mwingine.

HAPA NDIPO NINAPOONA KUNA TATIZO LA MFUMO WA UKATAJI TIKETI WA TRC LINALOHITAJI KUFANYIWA MABORESHO.

Kwa nini siti iliyohifadhiwa kwa safari ya Morogoro kwenda Dar es Salaam isitumike kwa abiria mwingine anayesafiri kutoka Dodoma kwenda Morogoro?

Vivyo hivyo, ikiwa abiria amenunua tiketi ya Morogoro kwenda Dodoma, kwa nini siti hiyo isiuzwe kwa abiria mwingine anayetaka kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro?

Kwa mantiki ya kawaida, siti inapaswa kuhifadhiwa kwa kipande cha safari ambacho abiria amelipia, badala ya kuonekana kuwa imejaa katika safari nzima wakati kuna vipande ambavyo haijatumika.
Mfano:
  1. Abiria A anasafiri Dar es Salaam–Morogoro.
  2. Abiria B anasafiri Morogoro–Dodoma.
  3. Abiria C anasafiri Dodoma–Tabora.
Abiria hawa watatu wanaweza kutumia siti ileile katika vipande tofauti vya safari, bila kuingiliana hata kidogo.

Huu si utaratibu mpya.

Mifumo ya kisasa ya uhifadhi wa nafasi za usafiri inaweza kuruhusu siti moja kuuzwa kwa abiria tofauti kulingana na vituo vya kupanda na kushuka (segment-based seat inventory management).

Mfumo mzuri unapaswa kutambua kuwa siti inaweza kuwa imeuzwa katika kipande kimoja cha safari lakini bado inapatikana katika kipande kingine.

TRC MNAPASWA KUBORESHA MFUMO WENU ILI KUONGEZA UFANISI WA MATUMIZI YA SITI.

Iwapo mfumo wa sasa hauruhusu jambo hili, basi kuna haja ya kuufanyia maboresho.

Vijana wa EGA wako vizuri kwenye mifumo they can help you with that, tayari wameshaunda mifumo complex ya e government kuzidi huo wa siti.

Lakini iwapo tayari unaruhusu, TRC wanapaswa kueleza kwa kina zaidi kwa nini bado abiria wanakutana na changamoto ya kuambiwa tiketi zimeisha wakati kuna siti zinazoonekana wazi.

Ukipanda treni ya Alfajiri kutokea Dodoma kwenda Dar siti nyingi huwa tupu na huja kujazwa Morogoro. Ni kwamba Dodoma Dar abiria ni wachache?!

Maboresho haya yanaweza kuongeza upatikanaji wa tiketi, kupunguza siti kusafiri bila abiria katika baadhi ya vipande vya safari, kuongeza mapato ya TRC na kuboresha uzoefu wa wateja.

Aidha, takwimu za tiketi zilizonunuliwa lakini hazikutumika zinapaswa kuchambuliwa kwa kutofautisha abiria ambao hawakufika kusafiri (no-shows) na siti ambazo zilikuwa wazi kwa sababu zilihifadhiwa kwa abiria wa vituo vinavyofuata. Haya ni masuala mawili tofauti yanayohitaji ufumbuzi tofauti.

Bwana Naibu Waziri na uongozi wa TRC, hili mlifanyie kazi. SGR ni uwekezaji mkubwa wa Taifa, hivyo tunapaswa kuhakikisha kila siti inatumika kwa ufanisi kadiri inavyowezekana.

Hatuwezi kuwa na abiria wanaokosa tiketi huku siti zikisafiri zikiwa wazi kwa sababu tu zimehifadhiwa kwa abiria watakaopanda vituo vya mbele.

Je, TRC mfumo wenu wa ukataji tiketi unaruhusu siti moja kuuzwa kwa abiria tofauti katika vipande tofauti vya safari? Kama hauruhusu, kwa nini?

Nawasilisha.

N'yadikwa
 
in short hawa jamaa hawajui watendalo! ukute ni mkakati ili wamuuzie ROSTAM SGR!
 
YAANI UKIFUATILIA KWA MAKINI WANAMAKOSA MENGI YA KIUFUNDI YANAYOCHANGIA
WAPATE FAIDA KIDOGO LAKINI PIA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA WAJANJA KUFANYA BIASHARA NDANI YA BIASHARA/WIZI....BILA KUINGIZA PRIVATE SECTOR HAPO, NI SUALA LA MUDA TU....
 
YAANI UKIFUATILIA KWA MAKINI WANAMAKOSA MENGI YA KIUFUNDI YANAYOCHANGIA
WAPATE FAIDA KIDOGO LAKINI PIA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA WAJANJA KUFANYA BIASHARA NDANI YA BIASHARA/WIZI....BILA KUINGIZA PRIVATE SECTOR HAPO, NI SUALA LA MUDA TU....
sema bila kuondoa uccm hapo, uccm umekumbatia kila aina ya ufisadi na uchawa. Uccm ni ukoma, kataa ukoma.
 
NDIVYO inavyofanyika siku zote. labda kama hujawahi kusafiri na Treni. Siti ikiwa imekatiwa kutoka Morogoro kwenda Dar kwa wewe mwenye safari ya Dodoma kwenda Morogoro unakata bila shidha na hata ukiingia kwenye mfumo kama safari yako ni ya Dodoma-Moro siti inaonekana ipo wazi. sawasawa na vituo vingine kutegemeana unapandia wapi na unashukia wapi.
 
Lengo ni kukwamisha miradi ya mandeleo ili wawape watu wao waendeshe hiyo miradi
 
Na mfumo ukikaa sawa utasikia umetengenezwa Korea kwa 2.5billion
 
Ukweli ni huu, kwamba ukikuta zimejaa unaweza kukata Kwa vipande say unatoka Dar unaenda Dodoma lakini training inaonekana imejaa. Unakata Dar moro siti A na Moro Dodoma siti B. Ila unapswa kuiscan hiyo receipt Morogoro Ili ionekane kwenye system vinginevyo utapigwa fine
 
Then kwanini itokee seats ziwe wazi kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho?!
 
Then kwanini itokee seats ziwe wazi kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho?!
Changamoto zipo lakini siyo kwa kiwango hicho. Inaweza kutokea kiti kuwa wazi kutokana mwanzo wa safari hadi mwisho pale ambapo aliyekata tiketi ameachwa na treni au ameahirisha safari dakika za mwisho, lakini ni mara chache sana kukuta seat iwe wazi kuanzia Dodoma hadi Dar es Salaam.
 
Ulishawahi kushudia hivo? kimsingi hali kama hiyo inaweza kutokea pale ambapo aliyekata tiketi ameachwa na treni au ameahirisha safari dakika za mwisho, lakini ni mara chache sana kukuta seat iwe wazi kuanzia Dodoma hadi Dar es Salaam.
Inatokea hivyo na ndivyo report ya The Citizen inavyosema according to Kihenzile, mimi pia nasafiri mara nyingi kati ya Dar na Dodoma there happen moments nyingi tu ambapo seats zinakuwa wazi hasa treni ya alfajiri, kwa hiyo tumuamini The Citizen na Kihenzile!? Au tukuamini wewe unaebishana na hizo published facts?! Au umeamua tu kubisha!!!. Haya tupatie facts tofauti na hizo zilizotajwa bungeni na kuandikwa na the Citizen
 
Abiria wenyewe ndio wana vichwa vigumu we ukiona Dar - Dom imejaa anza kutafuta route fupi mfano Dar - Moro halafu Moro - Dom maana kuna watu watashuka moro na kuna watu watapandia moro.
 
YAANI UKIFUATILIA KWA MAKINI WANAMAKOSA MENGI YA KIUFUNDI YANAYOCHANGIA
WAPATE FAIDA KIDOGO LAKINI PIA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA WAJANJA KUFANYA BIASHARA NDANI YA BIASHARA/WIZI....BILA KUINGIZA PRIVATE SECTOR HAPO, NI SUALA LA MUDA TU....
Hapa nadhani kuna kitu hatuelewani,abiria wa Dom-Mor ambaye hakutoa taarifa mapema kuwa hatasafiri,ni vigumu kuuza kiti chake kwani mpk dkk ya mwisho treni inapoondoka ndio inajulikana kuwa huyu abiria hayupo,hivyo italazimu siti yake iwe wazi mpk Mor ambapo abiria wa Mor-Dar atapanda,lakini kama alitoa taarifa kuwa hatasafiri siti yake inaweza kuuzwa.Kwahiyo siti nyingi zinazokuwa tupu ni zile ambazo abiria hawakutoa taarifa mapema kuwa hawatasafiri...
 
Kama tiketi zilinunuliwa kwamba nauli ililipwa, shida inakuaje tena ya TRC na si ya walipaji hiyo nauli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…