TRC na Ajali ya Dodoma: Kuna tatizo la kiutendaji

Mkuu naona unamcchongea Kadogosa
Hili sio suala la Kadogosa jomba...hili lipo chini ya wajibu wa ma Station masters...nini wajibu wa Station masters au any group ambalo Lina husika na kuhakikisha usalama wa reli kwa ujumla kila siku...lazima wawajibishwe ili wengine waelewe maana ya uwajibikaji. Unataka kutuambia hakuna mtu alijua mvua imenyeesha kubwa...nani ali take trouble ya kucheki usalama wa reli wakati treni iliyobeba mamia ya watu inasafiri
 
Tazara mwaka 1970/75
Rail ya kati imegengwa na mjerumani wakat akitawala Africa mashariki.. Ndio maana nikasema IMECHAKAA
Mbona umeshafanyiwa ukarabati mkubwa sana na wataalam walijiridhisha pasina shaka kuwa kuna usalama wa kutosha...wa kufanya biashara ya reli iendelee...walipasisha
 
Mbona umeshafanyiwa ukarabati mkubwa sana na wataalam walijiridhisha pasina shaka kuwa kuna usalama wa kutosha...wa kufanya biashara ya reli iendelee...walipasisha
Aaahh wapi Niliona wale wachina walichokifanya reli ya kati ni kubadilisha mataluma na kutandaza reli zingine kwa baadhi ya vipande. ila tuta halikupandishwa Yaani ardhi na tuta la rail vinapishana kidgo sana
 
Leo tunajitokeza Kuwalaumu hivi TRC kutokana na Ajali iliyotokea ila sijui huwa tunakuwa wapi Kuwapongeza pale wakiwa wanazidhibiti hizi Ajali.

Unataka kila anaetekeleza wajibu wake ashukuriwe na kupongezwa?
Huo ni wajibu wao kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi ya kuhakikisha njia ya reli inakuwa salama.
 
Leo tunajitokeza Kuwalaumu hivi TRC kutokana na Ajali iliyotokea ila sijui huwa tunakuwa wapi Kuwapongeza pale wakiwa wanazidhibiti hizi Ajali.
Kwanini wapongezwe kwa kutimiza wajibu wao wa msingi? Upongezwe kwa kufanya kazi inayokulipa mshahara? Siku wakitengeneza vichwa vya treni tutawapongeza ila kukagua reli ili kudhibiti ajali tuwapongeze? Big NO.
 
Kwa hiyo tuseme usimamizi wa reli ya kati unasuasua kutokana na wahusika kuhamishia mawazo yao kwenye reli mpya? inakuwaje miaka nenda rudi maeneo ya reli yenye changamoto hayathibitiwi, mfano. kuna baadhi ya watu wanasema reli iliyopo ingeweza kufanyiwa ukarabati wa kutosha na kuokoa gharama za kujenga reli mpya kwa sababu na yenyewe ni SGR...
 
 
Tusiwe premptive kwenye suala hili. Tuache uchunguzi ufanyike na baada ya hapo tutakuwa na haki ya kujadili/kuuliza kuhusu chanzo halisi kama ni uzembe au la.
 
Leo tunajitokeza Kuwalaumu hivi TRC kutokana na Ajali iliyotokea ila sijui huwa tunakuwa wapi Kuwapongeza pale wakiwa wanazidhibiti hizi Ajali.
Kazi yao ni kusafirisha mizigo na Abiria, hiyo kazi ya kudhibiti ajali umewapa wewe!
 
Kuna uzembe wa haja, wafuukuzwe tu watumishi waliozembea
 
Kule wanakagua na viberenge vipo Always, sehemu korofi madereva wanajua na wanaenda kwa tahadhari sana,
Ajali ilipotokea napajua ni mteremko haswa madereva wengi huwa wanamanua tu mpk afike bahi,miaka ya mkapa lile treni lilipanda saranda kule likazidiwa nguvu na mabehewa breki zikafeli likapigwa rivasi mpaka hapo kigwe kabla ya Bahi walikufa watu wengi tu
 
kiukweli binafsi nimepanda treni kwa mara ya kwanza mwezi NOVEMBER toka Dar - Moshi. lakini kuna viashiria vilivyonitia wasiwasi juu ya usalama wa treni dhidi ya ajali

Nilishuhudia mara kadhaa treni ikisimama na nikasikia majani yameota sana ndani ya reli hivyo wanamwagia mchanga, kuna kipindi mpaka niliogopa maana treni lilisimama muda mrefu ili kupunguza adha hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…