Nkamu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2007
- 226
- 91
Habari zenu wajumbe wenzangu wa jukwaa hili adhimu!
Nimekutana na changamoto hii kwa mara tatu sasa. Unaingia kwenye mtandao wa kukata tiketi wa SGR kutoka Dar kwenda Dodoma unakuta treni zimejaa siku mbili mbele. Hivyo kama una safari ya ghafla kwenda au kutoka Dodoma huwezi kutumia treni sababu linakuwa limejaa siku mbili kabla ya safari.
TRC ni shirika la kibiashara ambalo msingi wake ni kucheza kati ya mahitaji ya huduma na upatikanaji wake (Demand and Supply) ili uweze kupata faida kubwa. Kinachonisikitisha ni kwamba mahitaji ya huduma yapo ya kutosha lakini mfanyabiashara anayetafuta faida analala badala ya kuchangamkia biashara.
Kama treni zinajaa siku mbili kabla ya safari, maana yake ni kwamba watu wanahitaji TRC waongeze treni kwa ajili ya safari hizo. Inasikitisha kuona treni inafika Dar saa 3 asubuhi inaegeshwa mpaka saa 12 jioni ili iende Dom. Muda wote huo, watu wanatafuta usafiri hawapati, wanaishia kupanda mabasi kwa safari ya masaa 7 mpaka 8! Kama TRC wangeongeza angalau treni moja ya mchana ingeweza kuongeza uzalishaji kwa shirika na pia kuwapatia huduma wananchi wanaotafuta usafiri wa haraka.
Naiomba managementi ya TRC na wataalamu wao wa biashara, waache kazi za mazoea wasije wakawa kama UDART. Biashara ipo na wateja wapo wa kutosha wa kuifanya treni isafiri kila baada ya masaa manne kutoka na kwenda Dodoma.
Naomba kuwasilisha kwenu wanabodi!
Pia soma: