TRC, TCB Wazindua kadi ya malipo ya tiketi usafiri wa SGR

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka TRC Bw. Fredrick Masawe (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bw. Jema Msuya wakionesha kadi ya malipo ya kabla ya tiketi ya SGR iitwayo TRC Prepaid Card wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika uuzaji wa tiketi za SGR na kumrahisishia mteja huduma mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi na huduma nyinginezo ndani ya Stesheni za SGR.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika jengo la stesheni ya SGR ya John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam Oktoba 10, 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TRC amesema kuwa dhamira ya TRC ni kuhakikisha kila msafiri anafurahia ufanisi, usalama na kuhamasika katika kila hatua ya safari kwa kufanya malipo kwa urahisi kupitia kadi hiyo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bw. Jema Msuya amesema kuwa kadi hiyo pia itatumika katika maeneo mbalimbali kama kwenye migahawa, hoteli na kumuongezea urahisi mtumiaji ambapo mtumiaji wa kadi hii kadri atakavyoitumia atapata pointi ambazo zitakuwa kama zawadi kwenye miamala atakayokuwa akiifanya, aidha kadi itaruhusu kuweka fedha na kutoa kwa usalama na wepesi wa matumizi.

Kadi hii ya malipo itatolewa bila ya malipo ya aina yeyote katika vituo vyote vya stesheni, kadhalika itapunguza msongamano wa abiria wakati wa kukata tiketi maeneo ya stesheni na kufanya malipo yawe kwa urahisi.
Uzinduzi wa Kadi 2025 1.jpg
 
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka TRC Bw. Fredrick Masawe (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bw. Jema Msuya wakionesha kadi ya malipo ya kabla ya tiketi ya SGR iitwayo TRC Prepaid Card wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika uuzaji wa tiketi za SGR na kumrahisishia mteja huduma mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi na huduma nyinginezo ndani ya Stesheni za SGR.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika jengo la stesheni ya SGR ya John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam Oktoba 10, 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TRC amesema kuwa dhamira ya TRC ni kuhakikisha kila msafiri anafurahia ufanisi, usalama na kuhamasika katika kila hatua ya safari kwa kufanya malipo kwa urahisi kupitia kadi hiyo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bw. Jema Msuya amesema kuwa kadi hiyo pia itatumika katika maeneo mbalimbali kama kwenye migahawa, hoteli na kumuongezea urahisi mtumiaji ambapo mtumiaji wa kadi hii kadri atakavyoitumia atapata pointi ambazo zitakuwa kama zawadi kwenye miamala atakayokuwa akiifanya, aidha kadi itaruhusu kuweka fedha na kutoa kwa usalama na wepesi wa matumizi.

Kadi hii ya malipo itatolewa bila ya malipo ya aina yeyote katika vituo vyote vya stesheni, kadhalika itapunguza msongamano wa abiria wakati wa kukata tiketi maeneo ya stesheni na kufanya malipo yawe kwa urahisi.View attachment 3486696
Mhii ni jambo jema. Kikubwa mtangulize uadilifu.kwennye pesa zetu
 
Mbona wametoa maelezo nusu, je kadi moja inaweza kukata tiketi mbili? Unakata tiketi kupitia hata mitandao ya simu au kwa app yao tu? Uwekaji wa pesa pia ukoje?
 
Back
Top Bottom