Tanzania Railways Corp
JF-Expert Member
- Mar 23, 2018
- 251
- 595
TRC wakiwa kwenye ukaguzi wa Vichwa Nchini Korea Kusini wametoa ufafanuzi wa uwapo wa treni ambazo Vichwa vimechongoka kutokana watu kuhoji utofauti wa picha zilizopo kwenye matangazo ya TRC kutofautiana na Vichwa vilivyoonekana wiki iliyopita. Soma: Vichwa vya Treni za SGR vyawekwa hadharani
Zaidi ya hayo, Wataalamu na watengenezaji wameonekana wakiendelea kufanya matengenezo ya Vichwa hivyo pamoja na kutoa ufafanuzi wa namna Vichwa hivyo vitafanya kazi.
---
Muonekano wa maendeleo ya utengenezaji wa moja kati ya seti 10 za treni za Kisasa (EMU) kwa ajili Reli ya kisasa (SGR), zinazotengenezwa na kampuni ya Hyundai Rotem ya Korea ya Kusini, ambapo kazi za utandazaji wa nyaya za umeme, mfumo wa usambazaji hewa ndani ya treni na ufungaji wa vifaa vya kielektroniki zinaendelea.
Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa
Kampuni hiyo ilipewa zabuni na Serikali ya Tanzania ya kutengeneza vichwa 17 vya treni vya umeme na seti 10 za treni za kisasa EMU.
Pamoja na kazi za utengenezaji wa treni hizo za kisasa, Hyundai Rotem kwa kushirikiana na Wataalam kutoka TRC wanaendelea na majaribio ya mifumo mbalimbali katika vichwa vya treni vya umeme, mjini Changwon, Korea ya Kusini.