TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

TRC yatangaza kurejesha huduma za treni ya abiria kutoka Dar kwenda Moshi

Daraja la kwanza linabeba watu wanne tu hivyo kwa safari fupi hailipi ni ghali sana, Fanya 23,500 x 80 = 1,880,000 /4 unapata 470,000 utampata nani
 
hizo hapo nauli zao
IMG-20191121-WA0045.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Shirika la Reli Tanzania, TRC linawatangazia watu wote kuwa safari za treni la biria kutoka Dar kuelekea Moshi zitarejea rasmi mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2019

Nauli Dar - Moshi inategemewa kuwa ifuatavyo:
- Daraja la tatu Tsh. 16,500
- Daraja la pili kukaa Tsh. 23,500
- Daraja la pili kulala Tsh. 39,100

================================

Dar es Salaam. Ikiwa tunaelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kanda ya Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi itaanza Desemba.

Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.

Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.

Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.

“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema

Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.

Wakati kuhusu uwezo wa kusafirisha abiria, amesema itategemea na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) itakavyowapangia japokuwa uwezo wa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kimoja cha treni kikiwa na uwezo wa kubeba mabehewa 20.

“Katika idadi ya abiria tutakaobeba tutasubiri Latra watuambie kwa kuwa wenyewe ndiyo wataalam wa usafiri lakini uwezo wetu kwa behewa moja ni kubeba abiria 80 huku kichwa kikiwa na nguvu ya kubeba mabehewa 20,”amesema.

Treni hiyo itakayopita Korogwe mkoani Tanga, TRC imetangaza nauli zake ambapo Dar es Salaam hadi Korogwe daraja la tatu itakuwa Sh10,700, daraja la pili kukaa Sh15,300 na daraja la pili kulala Sh25,400.

Wakati kwa abiria watakaotoka Dar es Salaam kwenda Moshi daraja la tatu itakuwa Sh16,500, daraja la pili kukaa Sh23,500 na daraja la pili kulala Sh39,100.
View attachment 1267371
Daraja la tatu ni la kusimama ? Maana daraja la pili kukaa na la tatu kulala !

All in all bado bei ni kubwa licha ya kwamba sijajua litatumia muda gani.

Bei yA kulala kwanini isipunguzwe ikawa 25,900/- ili kuwalizimisha wenye mabasi yao kushusha nauli hasa mwezi huo unafuata..?

Kwa hiyo ya 39 elfu na ushee haifai....what the point kutumia kiasi hicho cha fedha kwa masaa 24 labda au zaidi wakati unaweza kutumia only 30,000/- kwa only 9-10 hours uko moshi via buses ??
 
[emoji1][emoji1][emoji1]analysis za ufipa ni vichekesho ..... wako busy kutafuta namna ya kukosoa tu
 
Hizo treni zinatumia muda gani kumaliza safari ? Isije ikawa mtu unalipa 39 yako halafu unatumia zaidi ya masaa 12. Utakuwa ni mtu wa ajabu kwa kutotumia Bus.
 
Wameboresha kwa sasa inatembea kwa speed yA 70km/hr sasa sijajua hadi Moshi ina cover KM ngapi ukujua hapo unafanya zile hesabu za velocity unapata masaa

Unachukua Umbali unagawa na Speed ya Chombo utapata Jibu.
 
Hii si ndio December? Hizo train zinafanya kazi? Na zinatumia muda gani hadi moshi?
 
Mnapenda shukurani mbona nyie hamshukuru kwa mazuri yanayofanywa na serikali?

Kwani Pesa inayo tumika ni ya nani Mkuu ?.Unaona kama vile Serikali imetusaidia wakati ni wajibu wake kufanya zaidi ya haya.Halafu Treni walizotumia kuvunia Mikonge ndio mnakuja kubebea Binadam?.Na hayo mnaona ni Maendeleo !?

Acha Ujinga na Ushamba.
 
Si vibaya ila kama unajali muda na una hela ya kutosha kwea pipa. Kama u mnyonge (obvious utakua na muda wa kutosha) kwea treni.
Sijaona sababu ya kumkosoa na wakati kauliza swali ambalo wengi wangependa kujua, muda kitu kizuri sana kuzingatia, watu wanataka kuangalia gharama za usafiri na muda utakao chhkua
 
Kwanza napenda kutoa pongezi kwa kurejeshwa kwa huduma hii, japokuwa sio jambo geni au jipya, treni ilikuwepo miaka ya nyuma, na changamoto zake zilikuwa nyingi kupita maelezo. Hapa nitatoa ufafanuzi.
Taarifa za awali zilizo rasmi sana zinasema kuwa Treni hii

1/Itatumia zaidi ya masaa 14 kutoka Dar-Moshi. Huo ni muda mrefu sana ukilinganisha na usafiri wa aina nyingine.

2/Treni hii haitakuwa inafanya safari zake kila siku kuja na kurudi Moshi. Hivyo uhakika wa kusafiri wakati wowote bado itakuwa ni changamoto.

3/Treni hii sio mpya, mabehewa na baadhi ya vichwa ni vile vya zamani. Changamoto zinazoonekana kila siku katika reli ya kati kutoka Dar-Kigoma zinategemewa kuibuka pia katika njia ya Dar-Moshi.

Hivyo pia wasafiri wajiandae.
 
Hivi ile 'Treni ya Mwakyembe' inayopiga route za daladala hapo Dar inaendeleaje?
Wanachi wangapi wanaipanda na kuipenda?
Imefanikiwa kwa kiasi gani kuua biashara ya daladala?
 
December hii nataka kusafiri kutoka Arusha hadi Dar es salaam. Baada ya kusikia usafiri wa treni upo kutoka Moshi hadi Dar nimepatwa na shauku ya kusafiri kwa maana itakuwa mara yangu ya kwanza kusafiri kwa njia ya treni.

1. Je, ili nifurahie safari ni pande daraja gani?

2. Na nauli yake ni kiasi gani? (Tupo wawili mimi na baby mama wangu)?

3. Ikiwa natokea Arusha nafikaje hio station ya hapo moshi?

Ushauri wenu JF members, Asante.
 
Back
Top Bottom