Treasury Bonds/T-bonds/T-Bills/Bonds/Hati Fungani ni Uwekezaji "Kichaa"

Huwezi kukopa zaidi ya 50% ya T-Bond uliyoweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo inflation haiathiri faida ya hiyo biashara?
Na ndio maana ili soko la apa Tanzania wengi wanaogopa. Maana financially MTU kama anakopa kwa zaidi ya 80% ikitokea kashindwa kurejesha mkopo inakuaje na kashakaa na fedha kama miezi 6 au kutakuwa na term and condition ambazo wanaweza kucheki unamiliki assets gani nyingine
 
Mfano nimewekeza 700M maana yake kila mwaka nina 108M

Kwa miaka 20 nitakuwa nimetengeneza 108 kila mwaka

Swali je nikiwekeza 700M ninaweza tengeneza 108M?

Look kid

Ni bora niwekeze kwenye hizo Hati fungani

Sasa 108M nitaanzisha Ranch business

Mwaka wa kwanza 108M nanunua shamba lenye deed katavi huko lets say 50K per acre nanunua 2,000 acres natulia

Mwaka wa pili napata 108M napanda majani na irrigation system

Mwaka wa 3 napata 108M najenga nyumba na miundo mbinu ya kwenye ranch hiyo

Mwaka wa 4 nanunua ngombe sasa natafuta mbegu Bora naweza kuanza na ngombe 200

Mwaka wa 5 108M nunua eneo jingine la 2,000 acres

Yaani after 15 years

Nina mashamba ya acres 10,000 yenye ng'ombe 2,000

Sasa value ya kampuni ambayo inamiliki acres 10,000 na ng'ombe 2,000 kwa mwaka huo acha tu

Halafu 700 bado imetulia
 
Mzeee unaandika kirahisi sana ...yani kma unakunywa maji vile
 
Hapa kikubwa kinachowasukuma wafanyabiashara ni ule msemo wa "usiweke mayai yote kwenye kapu moja" mkuu..... BIASHARA ni wazo zuri ila kama una pesa ya ziada inabidi kuipeleka kwingine na sio tu kuitegemea hio biashara ulionayo Ili kuongeza mifereji yako ya kipato.
Lakini pia unaweza kutumia hati fungani kama dhamana ya mkopo(kwa kwetu Tanzania ni takribani 75% ya ulichowekeza kwenye hati fungani) ambayo inafaa zaidi kwa mtu asietaka kuweka mali zake rehani(nyumba n.k)
....Kuna mwingine pia anaweza akawa amepata hela nyingi kwa mkupuo(amestaafu n.k) na hana uzoefu wa biashara, uwezo wa kuhimili hatari za biashara(risk appetite) upo chini ama hana muda wa kutosha kuisimamia na kuifuatilia biashara yake.

ITAFAA ZAIDI KAMA UKIFUTA KAULI YAKO MKUU
 
Hii treasury bonds na mutual funds tofauti yake ni nini?
Treasury bonds ni hati fungani za serikali kwa maana kwamba unaikopesha serikali na yenyewe inakulipa taratibu kwa riba(kawaida huwa ni baada ya miezi sita au mwaka) ila mutual funds ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja(kwa kwetu Tanzania ipo UTT-Amis) ambao sasa wenyewe unasaidia sisi wenye vipato vya chini na vya kati kuweza kuwekeza sehemu mbalimbali ikiwemo hizo hati fungani(Treasury bonds), akaunti za muda maalum(fixed deposit accounts), hisa(stocks) kwa wepesi na pia kupata faida na gawio(ama kimoja wapo) zuri zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…